Iphone wame'surrender, sasa wanakuja na simu ya line mbili (dual sim)

Iphone wame'surrender, sasa wanakuja na simu ya line mbili (dual sim)

thamani sio ya i phone hiyo..

hiyo ni thamani ya kampuni ya apple.

apple wanapiga sana hela kwenye pc.. computer zao ndio zinauzika sana sababu ni za kazi.. video editor na photographer karibu wote duniani wanatumia apple...

tukiongelea simu kama simu.. techno anamzidi mauzo i phone sana kwa soko la africa... na kwa soko la dunia samsung anamzidi iphone kuuza simu..

ila tukiongelea computer za apple ambazo ni mac .. hapo anauza sana na kupiga mafaida hayo ya kampuni kufika matrillion... ila sio i phone
We huijui iPhone mkuu,
 
Ni laini moja kwa mtandao mmoja
Serikali yetu wajanja sana. Hapo wamefikiria namna ya kuongeza wateja wa ttcl. Wakaona waweke sharti la line moja kwa mtandao mmoja ili wenye line zaidi ya tatu, wawe na line za ttcl. Yaani unalazimishwa kutumia mitandao yote hata kama huduma ni mbovu
 
Mnaposema Tecno amekamata soko la Africa mnazungumzia Africa gani?Labda tuanzia hapo maana kuna nchi zingine za Africa ukiwa na Tecno utapata tabu saaana kuuza
 
Hapo Sasa Hawana Namna Maana Upepo Huu Umewafanya Waungane Na Dual Ila Siyo Kushindana
 
Hii habari inaonesha kabisa mleta mada ni hater wa iphones.

Jambo la kufurahisha ni kwamba mleta mada namimi tuko kundi moja.

Wale waliozoea jela za iPhones kutwa kuzinadi sasa wanaanza kutuheshimu sisi waumini wa android sana sana dual sim.

Msipende madharau nyie team iphones
Kwanza ni kama mnaishi jela ya kujitolea[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sent from My iphone X using jamiiforums App, niliinunua jana pale karume karb na duka la mapajama.
 
Mnaposema Tecno amekamata soko la Africa mnazungumzia Africa gani?Labda tuanzia hapo maana kuna nchi zingine za Africa ukiwa na Tecno utapata tabu saaana kuuza

elewa kwanza maana ya market share..

mfano idadi ya watu wanaotumia simu africa yote wapo bilion moja..

unakuta nusu yao wanatumia tecno.. na wanaobaki nusu wengine ndio wanatumia mchanganyiko wengine iphone, wengine samsung, wengine huawei..

hapo kitaalamu wanasema tecno ana 50% market share in africa

so haijalishi nchi gani.. mradi ni africa tecno anakuwa king wa mauzo.. hata kama kuna nchi hajauza hata simu moja... ila zile nchi alizouza tecno nyingi zinambeba.. na kumfanya apige hela kuliko wenzake kwa soko la africa
 
Kitu pekee ambacho iphone anacho kizuri ni iCloud. Na yenye nguvu inaanzia iPhone 5.

Ukiachilia iCloud hakuna chochote bora cha kusema itastand out kama beast.
 
elewa kwanza maana ya market share..

mfano idadi ya watu wanaotumia simu africa yote wapo bilion moja..

unakuta nusu yao wanatumia tecno.. na wanaobaki nusu wengine ndio wanatumia mchanganyiko wengine iphone, wengine samsung, wengine huawei..

hapo kitaalamu wanasema tecno ana 50% market share in africa

so haijalishi nchi gani.. mradi ni africa tecno anakuwa king wa mauzo.. hata kama kuna nchi hajauza hata simu moja... ila zile nchi alizouza tecno nyingi zinambeba.. na kumfanya apige hela kuliko wenzake kwa soko la africa
Hiyo Tecno ina soko Tanzania na Malawi,hata wenzetu wakenya hawatumii sana ujinga huu
 
Kipindi hicho natumia simu ya line moja nilikua naona radhi niwe na simu mbili ili kila moja ikae na line yake ila baada ya kupata simu yenye line 2, Samsung aisee hauniambii kitu kwenye simu za line mbili? Naona Iphobe itakua wanapumulia shida sasa hivi hahaha walianza kwenye masimu makubwa 4.7 inches na 5.5 inches aisee naona soko la dunia si mchezo
 
Back
Top Bottom