Introducing the new Galaxy S4 (live)

Introducing the new Galaxy S4 (live)

galaxy s-iv ni failure sjaona kipya hata kimoja wamecopy kila kitu. Nimeangalia event very boring.

Ngoja tusubirie mauzo yatakayovunja rekodi sasa
 
boring event, even more boring S IV. while siwezi fork over money for flagship devices (wasted money IMO), ningechukua HTC ONE over hii anyday
 
CHANZO: Gajetek - Gajet na Teknolojia
Twitter: @gajetek
15/03/2013


Samsung Galaxy S IV Yazinduliwa Rasmi

Samsung imezindua Galaxy S IV, uzinduzi huo umefanyika usiku huu (kwa saa za Afrika Amshariki katika jiji la New York. Awali tutazungumzia mambo mapya katika simu hiyo, kwanza Samsung wametoa kitu kinachoitwa S - Health kwa mara ya kwanza kwenye simu zao. S health inafanya kazi na sensa aina ya pedometa iliyomo kwenye S4. Hivyo inakupa taarifa za kiafya kama vile umeunguza kaloris ngapi, umetembea au kukimbia masafa gani, S Health itachanganya taarifa utakazoziingiza kwenye simu yako kama vile urefu, na uzito kisha itakupa ripoti kamili ya maendeleo yako ya kiafya. Hii itakuwa ni kivutio kizuri kwa wamamichezo na wafanyao mazoezi.

S-Health si jambo jipya kwenye simu kilicho kipya ni kuwemo kwa sensa ya pedomita, ingawa simu nyingine hutumia sensa mbili kufanya kazi hii yaani akselerometa na GPS na kuweza kukupa taarifa za kiafya kama hizi , au wengine hutumia Fuel Band inayovaliwa mkononi kama saa na fuel band hutoa taarifa sawa na za S Health kwenye simu yako. Walichoweza kufanya Samsung ni kukupunguzia gharama za kununua fuel band ambayo inafika TSh 250.000
Kivutio kikubwa zaidi ni kwamba Samsung wametumia prosesa mpya kabisa ijulikanayo kama Exynos 5 Octa chipset. Prosesa hiyo ina core NANE. Samsung wamedai kuwa exynos 5 octa hiyo itaiongezea nguvu simu lakini pia ina uwezo mkubwa wa kubana matumizi ya betri kwa vile huengeza nguvu na kutumia core zaidi pale tu core hizo zinapohitajiwa, tofauti na quad core ambapo ina core 5, hutumia nne au moja ya ziada pale unapofanya mambo yasiyohitaji nguvu kubwa ya prosesa. Hivyo simu hii kwa upande wa games na graphics bila ya shaka itafanya viuri mno.

Samsung wameingiza manjonjo mengi mno kwenye kamera yenye megapiksel 13. Kwanza kabisa inauwezo wa kupiga picha kwa kamera zote mbili, ya mbele na ya nyuma kwa wakati mmoja. Pia wameendeleza sifa ya "drama shot" ambapo kamera hupiga picha nyingi mfululizo na kupendekeza kwa mtumiaji ipi imetoka vizuri zaidi. Pia kama ilivyo Lumia 920 na HTC One inachukua "live photo", kwa lugha nyepesi hii ni video ya sekunde chache mno, ila walichoongeza Samsung tofauti na HTC One na Lumia 920 ya Nokia wao wameipa uwezo wa kuchukua na sauti. Vile vile unaweza kuchukua video kwa kamera zote mbili kwa wakati mmoja.

Jengine jipya ni kwamba iwapo unasoma kurasa za mtandao au kitabu cha elektorniki (EBook) utaweza kufungua kurasa kwa kuitikisa simu yako badala ya kusugua skrini. Vile vile Samsung Galaxy S4 inatambua kama mtumiaji anaangalia skrini hivyo kwa mfano iwapo unaangalia video utakapogeuka na kuacha kuiangalia skrini basi video inasimama wenyewe, utakaporudisha macho kwenye skrini video inaendelea kucheza yenyewe.

Wakati Nokia Lumia 920 ndio inayosifika kwa utiifu wa skrini mguso (responsiveness) Samsung wameenda mbele zaidi, yaani wameweza kuifanya simu hiyo utumie ukiwa umevaa gloves, lakini zaidi unaweza tu kuupeleka mkono ukakaribia skrini na kuanza kufanya mambo mkono ukiwa karibu bila ya kuigusa skrini.

Maumbile ya S4 ukilinganisha na S3 ni kwamba kuna mabadiliko mawili makubwa, imeongezwa ukubwa kufikia 4.99" na pia imezungushiwa kwa sehemu za ubavuni juu na chini aluminiam, ingawa ufuniko wa nyuma bado ni wa plastiki. Pia Samsung wametoa gamba waliloliita S View Cover ambalo huhitaji kufungua ili kumjua aliyekupigia simu kwa vile linaonyesha (transparent) sehemu ambayo namba hutokea.


Samsung wametangaza kuanza mauzo ya simu hii mwezi wa nne, na kauli mbiu ya kibiashara iliyopewa simu hiyo ni "life companion". Katika uzinduzi huu Samsung wamefanya manjonjo ya aina mbali mbali kama vile kuwepo kwa bendi inayotumbuiza, na kufanya aina fula ya maigizo huku wakitumiwa wanawake warembo kuonyesha jinsi simu hiyo inavyotumika.

Kwa mtazamo wa haraka Samsung Galaxy S4 haikubadilika sana, au tuseme haikutoka na jambo lolote la ziada la kuubadili ulimwengu wa simu. Lakini tunapata hisia kwamba simu hii bado itavutia wateja wengi. Hata hivyo tutaizungumzia tena simu hii wakati tutakapoitia mkononi na kuyafanya yaliyoelezewa wenyewe kisha tuichambue zaidi.
 
Hakuna jipya kwenye hii simu, mambo yote lumia 920!
 
Walikuwa na vipya kama duel video recoding kwa kutumia front and back camera, stopping video when u look away feature, S- translator looks good if it is going to work because the s voice thing from sumsung has never worked. Atlist apple they tell their siri supports like American,uk, Australia, Japanies na chines voices hawa jamaa wakorea wanababaisha tuu sijui hats kama hiyo S-voice inasupport wakorea all the time.. lol

the presentation was kituko you cant take it serious and some features were not showing demo as usual so i thing they wont work they were just filling time.
 
mKuu??? Quad Core N core Nne au Tano????
tofauti na quad core ambapo
ina core 5, hutumia nne au moja ya ziada pale unapofanya mambo yasiyohitaji nguvu kubwa ya
prosesa.
 
Duh! Minataka simu ya ku download hela bado haijazinduliwa?
 
Walikuwa na vipya kama duel video recoding kwa kutumia front and back camera, stopping video when u look away feature, S- translator looks good if it is going to work because the s voice thing from sumsung has never worked. Atlist apple they tell their siri supports like American,uk, Australia, Japanies na chines voices hawa jamaa wakorea wanababaisha tuu sijui hats kama hiyo S-voice inasupport wakorea all the time.. lol

the presentation was kituko you cant take it serious and some features were not showing demo as usual so i thing they wont work they were just filling time.

mkuu kitu ambacho sina uhakika nacho ni ile s health lakini vyengine vyote najua wamecopy wapi.

Blackberry wa watu simu yake haina innovation nyingi hizo chache alizo nazo pia zimekopiwa. then wanaiga sana apple samsung naona kila kitu chao wameeka s au smart nyuma. Smart story ndio kitu walichokua bb wanajidai nacho kwenye z10.

Mkuu double shot pia imezinduliwa before na lg ipo na samsung nae kairudia ngoja sasa uskie kesi mahakaman maana nao hawa hawapendan
 
mkuu kwenye screen responsiveness sidhani kama wameipita 920 maana niliskia wakipresent walisema moja ya sababu ya kutumia hio technology ya kupeleka mkono karibu na screen na kuswipe ni kua na kucha ndefu. Na nnavyofahamu mimi kucha zinakubali kwenye screen ya 920. Nafkiri screen ya samsung ni kama ya sony inakubali gloves za leather tu. (tusubiri review na comparison tutajua ukweli).

Then chengine hawa jamaa walichoniudhi jana sijalala halafu kumbe ilikua sio live demo. Watu walikua wanaongea then wakifanya testing wanaeka recorded video na images ambazo zishafanywa mda. Live demo ilikua kwenye s translator tu. This is cheating na mi skufurahi kabisa
 
si mchezo, ndo nayajua haya mengine. ngoja tusubiri hilo la s health reference yake. 😀
afterall, nitaelekea nexus
 
Unajua theres a difference between Apple and Samsung kwa kweli!
The new Samsung is all about Gestures nothing more, nothing new there! I am pretty sure a developer can create an app for the available camera of any of a smartphone to read the movements!

Nimeona video ya Cnet katika youtube yaani mtu ugeuze bichwa zima ndio next photo ije, i thought ni eye movement alon is enough . Then kuna jamaa anatumia Hand gesture kubadili photos, iko Laggish. The same boring OS with nothing new! I call it a TOTAL FAILURE! Jus imagine the the phone has a quad core processor and scrolling between images is like havin 1 processor with less than 1GHZ! Mi nawaambia wenzangu kuwa hawa jamaa Apple sio kwamba wanashindwa kuport high Specs hardware katika simu yao, ama includes top features, the thing is, ARE YOU GOING TO USE IT IN YOUR DAILY LIFE? Apo ndio apple anapotizama. Usishangae iphone 5s/6 ikawa haina high specs za kuifikia samsung but everything it have is used in a daily life activities!

Samsung you fail!
 
kwangu mie, sijaona kipya au kikubwa kwa S IV, tena nimeiona as a failure. natoa sababu zangu kama hivi
  • kwanza, kuendelea kwa kutumia plastiki on their premium phones ni a huge failure by Samsung. hata kama wanasema kwamba ni polycarbon (or something poly), plastic ni plastic and will it always feel cheap. wangetumia glass au aluminium kama wapinzani wao. mimi sio mpenzi wa iPhones, ila nakumbuka mara ya kwanza nilishika iPhone 4, nilivutiwa sana na kutamani kuwa nayo. in fact mpaka leo naitumia simply coz ina that feel ya worth.
  • cha pili ni utumiaji wa processa nane yaani Exynos 5 Octa. ukweli ni kwamba Android kama OS haitumii processor zaidi ya mbili na zingine zinakuwa waste, coz hata apps na games nyingi haziwezi take advantage of the extra processors. hili limekuwa jambo kubwa hata kwa PCs (my speciality) ambapo wanajaza cores nyingi kama hizi mpya za AMD zinazoitwa Bulldozer ambazo zina processor 16 lakini ukifanya comparisons, zinapigiliwa mbali na quad cores za intel xeon core. :focus: tusubiri benchmark comparison ila mi sioni S IV ikiziacha the likes of HTC ONE, Xperia Z na especially Lenovo K900 (ambayo ina duo core atom processor). hizi core nane zitafanya tu bei ya S IV kuwa kali zaidi
  • kuzidisha kwa pixels. while hili ni jambo linanichosha kwa smartphone manufacturers wote, sikudhani Samsung watazidisha ppi kiasi hichi ( 441). ppi iliyozidi 300 is not discernible to the human eye (yaani hutaona tofauti pixels zinavyopanda na ulipotoka) na hizi ppi kubwa zitakuwa tu za kunyonga battery life. usimcheke Apple na Retina display, hawa washikaji wanajua.
  • 1080p. again something smartphone manufacturers wanaweka ambacho sijapenda. hizi HD resolutions while ni nzuri, on a 5" screen, hazina la maana kivile. wangefunga 720p tofauti isingekuwepo. resolution kubwa hutaka screen kubwa ndo maana mtu aliye na a 40'' TV tu ndo anaweza kusema tofauti kati ya movie iliyo na resolution ya 720p/ i na 1080i samsung baada ya kuweka all these, bado wameamua kufunga battery ya 2600mAh. Huawei Ascend P2 walionyesha ni possible kuongeza battery power, kwanini S IV na upgrades za size na resolution na PPi wasiweke battery ya unafuu zaidi
conclusion yangu ni kwamba Samsung wanaenda style ya apple ya kurecycle an old model na kuongeza a few features then kupiga label ya a new phone, a failure in my eyes
 
Back
Top Bottom