Interview ya TPDC utata mtupu!!!

Interview ya TPDC utata mtupu!!!

Unamaanisha mtoto wa Huyu Mbunge: Rita Louise Mlaki - Wikipedia, kamusi elezo huru au? Anaitwa Moureen Mlaki Julius. Aliitwa hadi kwenye amplitude test pspf. Ila kielimu yuko njema, si amesoma Moi Univ Master of Banking & Finance, grad wa 2012.

Ebu tufunulie zaidi mkuu.

Yes..ni kijana mdogo hivi mwembamba..jina ntaliweka hapa nikikumbuka..kwa ufupi kilichotokea ni hivi....Jana pale Msimbazi center baada ya zengwe walokutana nalo wenzetu waloambiwa majina yao hayaonekani, interview iliendelea na baada ya hapo tukaelekezwa majibu ya watakaoitwa kwenye oral interview yatabandikwa kwenye saa kumi na moja jioni jana ile ile..sasa basi kweli namba zilibandikwa maana majina hayakutumika..now i understand why...wakasema wafuatao waje kufanya oral interview pale TPDC mikocheni kesho saa tatu asubuhi (yani leo) na walikuwa wengi tu. Cha ajabu leo watu tumeamkia pale tukiwa bado tunashangaa maana ni pale brajec..kajamaa kakatokea kamevalia suti safi kabisa na briefcase tena katokea ndani ya mjengo na sio magetini walikopita wengine..kwa ufupi kila mtu akawa attention..maana hakuonekana kama mwenzetu..mara akaitwa kule ndani alikotokea..wewe ndo umekuja na taxi? unaitwa...akaenda huko ndani..baada ya muda zengwe likaanza..panel walikuwa washakaa (changa la macho) kisha watu wakaanza kuuliza what now..mbona muda unayoyoma..kwenda kumuuliza receptionist aliyekuwa anafanya registration..ikaonekana wote waliokuwa wamefika pale hakuna hata mmoja anayetakiwa kuingia interview...isipokuwa kale kajamaa tu...akaja huyo mmoja wa panelist akasema wamepigia watu 3 tu simu ambao ndo wanatakiwa kufanya oral interview..cha kusikitisha jana hawakusema watapiga simu bali watabandika majina na kweli walibandika na kuwaita watu waje mikocheni...cha ajabu zaid hadi saa tatu na nusu ni mmoja tu kati ya watu watatu waliopigiwa simu according to panelist ambaye ndo huyo kajamaa ambaye alikuwepo..ndo kusema hao wengine wawili walikuwa hawaitaki hiyo kazi hadi wasije?
 
Unajua ni wakati wa kuchukua uamuzi mgumu....hii kulalamika lalamika haisaidii sisi kama vijana ambao tunategemewa katika nchi hii tuache kulalamika bali tuangalie system nzima ya nchi hii ilivyooza kuna hili suala la UBINAFSI nani anajua kwanini wametoa shortlist mbili? Ni muda wa kufanya uamuzi mgumu...

mkuu. muda wa kufanya maamuzi ni sasa hivi au October 2015? unashauri yafanyike mageuzi kama Misri?:frusty:
 
halafu mie nilionaga pia first day walitoa majina na kesho yake wakatoa tena

nikajua wamerudia tu watu ambao hawakupata nafasi ya kuona jana waone leo kumbe

wana Mission zao..mwenye nacho anazid kuongezewa

Mtoto wa Rita Mlaki kala shavu
 
Ushindi wa mezani upo kila sehemu kwa watoto wa wenye nchi..

But hii ya kumchinjia baharini mtoto wa mkulima alietoka sengerema kuja interview Dar na umemwita gazetini ni kujitafut laana..[/QUOTE
Mkuu inatia uchungu sana,yaani mtu wamemuita then amefika na gazeti kbsa na jina lipo,katoka Sengerema kasafili usiku mzima,kufika morogoro basi likazuiwa maana usiku ulilkuwa umefika,ikabidi jamaa adandie roli ili afike Dar alfajiri...kufika mbezi saa kumi na moja.alfajiri,foleni imefunga...nikamwambia akodi pikipiki aje hadi External ili nimpeleke mana alikuwa hapajui Msimbazi Center...hata kuoga wala kubadili nguo hakuna mana alifika saa moja kasoro!!!!Anafika pale eti wanamwambia kama jina lipo gazetini na mtandaoni halipo basi hawezi kupiga interview...jamaa akatoa gazeti jina lipo,msichana mmoja akaja na simu akamwambia jina lako lipo gazetini lkn kwenye website halipo...so hauruhusiwi kuingia ndani rudi tu kwenu.
Kwa kweli ni jamaa yangu,imeniuma sana,ni.bora hata angefanya ijulikane kashindwa kuliko kumkejeli na kumweka kando amekata sana tamaa!!!Inaumiza sana,ila ngoja ipo tu siku
 
mi niliona hilo tangazo lililorudiwa nikajua tu lazima watu waumie......
 
mi niliona hilo tangazo lililorudiwa nikajua tu lazima watu waumie......

Watu wameumia kweeeli mkuu!!!ha ha ha ha ha ila.huu nih uonezi kabisa
 
Nilimpeleka jamaa yangu Msimbazi Centre kufanya usaili wa TPDC...ameingia alfajili kutoka Sengerema Mwanza,baada ya kumfikisha niluenda zangu job kwa makubaliano ya kumfuata akitoka ktk usaili.
Kumbe hawa jamaa walitoa shortlist mbili baada ya yakwanza kusema waliikosea na kupunguza majina kuanzia mia na kitu,ajabu jina la mshikaji lilikuwa kati ya moja na ishirini...Gazeti la majina ya pili hakuwa nalo,so alijua kaitwa,baada ya safari ya usiku mzima anafika anaambiwa jina lake halikutolewa ktk majina ya mara ya pili,hivyo hana nafasi ya kufanya usaili,akatoa gazeti akawapa na kuwaonyesha jina,wakamkatalia wakasema wao wanajua shortlist ya pili na si ya kwanza.
Kwa kweli kuna vitu ktk maisha ni mtihani,umbali mrefu wa Sengerema to Dar,kulala Moro na kuamka alfajiri kuja Dar lkn no usaili..Kwa kweli hizi ajira ni majanga.


Nadhani akienda pale CMA(Mahakama ya Kazi) haraka anaweza kuwa na madai ya Msingi.Atafute wataalamu wa Sheria wakumsaidia haraka iwezekanavyo.
 
Yaani mimi ndo wamenikera wameniboa na kila kitu, walisema watabandika kwenye website ya coet.udsm jana saa 11 jioni tangu jioni hiyo mpaka leo asubuhi ya saa nne kasoro ndo majibu waruhusu web kufunguka. Hoja yangu ni, kama kweli walikuwa wanahitaji kusaili watu walishindwa nini kuweka results toka jana. Cha ajabu eti waliopita jana waende leo kufanya oral hivi mtu angeota kama kapita? Halafu kwa hiyo saa 4 na foleni za dar mtu anafikaje kwenye interview. Kiukweli TPDC HAMNA HAKI, MNA UONEVU ULIOKITHIRI, HUO SI UUNGWANA.
 
Yaani mimi ndo wamenikera wameniboa na kila kitu, walisema watabandika kwenye website ya coet.udsm jana saa 11 jioni tangu jioni hiyo mpaka leo asubuhi ya saa nne kasoro ndo majibu waruhusu web kufunguka. Hoja yangu ni, kama kweli walikuwa wanahitaji kusaili watu walishindwa nini kuweka results toka jana. Cha ajabu eti waliopita jana waende leo kufanya oral hivi mtu angeota kama kapita? Halafu kwa hiyo saa 4 na foleni za dar mtu anafikaje kwenye interview. Kiukweli TPDC HAMNA HAKI, MNA UONEVU ULIOKITHIRI, HUO SI UUNGWANA.
kumbe usanii uliendelea...hii kali.. halafu jamaa hawana hata aibu yani
 
Nashauri vijana wote tusio na ajira tuunganishe nguv na kuhakikisha kila mtu ana kadi ya kupiga kura 2015 jaman tubadilisheni mambo ili hata haya malalamiko yetu yapungue!
 
Back
Top Bottom