Interpol imetaka maafisa 6 wa FIFA kukamatwa

Interpol imetaka maafisa 6 wa FIFA kukamatwa

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
150603110229_interpol_640x360_bbc_nocredit.jpg


Shirika la maafisa wa polisi wa kimataifa Interpol limetoa ilani ya kukamatwa kwa watu sita wanaohusishwa na FIFA kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi.

Agizo hilo linawalenga maafisa wanne wa mashirika makuu pamoja na maafisa wawili wakuu wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA akiwemo aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner.

Sita hao tayari walikuwa wametajwa katika mashtaka yaliofunguliwa dhidi yao na mamlaka ya mahakama za Marekani wiki iliopita.

Ilani hiyo inawalenga watu wanaotafutwa kwa lengo la kuwakamata ili wasafirishwe hadi mataifa waliohusika na ufisadi huo ili washtakiwe ,lakini mataifa hayawezi kulazimishwa kumzuilia mtu yeyote aliyetajwa.


Chanzo: BBC
 
shida ni Africa kuandaa kombe la dunia... urusi kupewa nafasi ya kuandaa world cup, na Qatar.....

juzi tu tumetoka Germany karibu kabisa na uingereza inayolilia kuandaa kombe la dunia... hizi ni fitna zote zinaanza kwakuwa fifa inajali hata mataifa madogo kwenye mpira.

ulaya inataka kuendeleza ufalme wake kwenye mpira... wanauharibu tu
 
Back
Top Bottom