International Street Children Day...12th April

Rwamuhuru

Member
Dec 22, 2010
50
0
shirika la Consortium for Street Children lenye makao yake makuu UK pamoja na mashirika mengine ya kupigania haki za watoto mitaani, limeitaka Umoja wa Mataifa kuitenga tarehe 12/04 ya kila mwaka kama siku ya mtoto wa mitaani duniani..

Kwa mara ya kwanza siku hiyo itaadhimishwa kesho trh 12/04 ili KUWA SAUTI kwa watoto wetu hawa ambao tumewatupa mbali na kuacha kusota na maisha tukiwapa majina mengi mabaya kama machokoraa na kusahauliwa na jamii yao ikiwamo serikali inayoishia kuwapiga kwa kutumia polisi bila kutafuta suluhisho la kudumu

Kwa upande wa Tanzania nina taarifa ya kuadhimishwa kwake Mkoani Arusha na MOSHI Kilimanjaro ikiandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali linalofanya kazi na watoto wa mitaani la Mkombozi....

Kwa watakaopenda kuwa sauti ya watoto hawa na kuungana na wadau wengine unakaribishwa kushiriki ama Moshi au Arusha (kwa wlaioko maeneo haya) na kwa upande wa Arusha yatafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia saa 4 asubuhi na kutakuwa na activities mbalimbali......Kwa walioko Arusha mnakaribishwa

Wale wa Moshi unaweza kuwasiliana na watu wa Mkombozi kwa taarifa zaidi

Waler wa Karatu kutokana na kuchelewa kwa taarifa tunapanga kuandaa siku hii hivi karibuni na watakaopenda wanaweza ni-PM na baadae kuwapa taarifa za kutosha

Kwa walioko mikoa mingine wanaofahamu kama inafanyika wanaweza kutoa taarifa hapa

BE THEIR VOICE, SPEAK FOR THEM....Kumbuka mtaa haukuzaa mtoto, HAWA NI WATOTO WETU....

Tembelea tovuti hizi kwa maelezo zaidi
Welcome to Consortium for Street Children
We want April 12th as International Day for Street Children | Facebook
Mkombozi (Kilimanjaro and Arusha Regions, Tanzania, East Africa)
http://www.mwemachildren.org
 
Back
Top Bottom