International Schools zina nini cha zaidi?

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
5,347
11,996
ANAANDIKA BICHWA KOMWE:-

Hizi shule zinazoitwa "international schools" zinafundisha nini cha ziada sana ambacho hakimo penginepo?

Ni kweli, shule zina mazingira mazuri na yanayofurahisha, lakini je, kile wanachofundishwa wale watoto kina hadhi gani ya kulipiwa mamilioni?

Hapa ieleweke vema kwamba siungi mkono mashule ya kata ambayo kimsingi ni mashule butu yasiyo na sifa wala vigezo vya kuwa shule. Mashule ya kata ni maeneo maalumu ambayo watoto wanaenda kujazwa ujinga na kupoteza wakati.

Hizi international schools pia ni kama mashule ya kata yaliyochangamka tu isipokuwa pale unaenda kununua KIINGEREZA kwa milioni hamsini kwa mwaka.

Zaidi sana mtoto atapewa midoli ya kuchezea na mabembea ya kuning'inia. Of course bila kusahau CHETI CHA KIINGEREZA.

Linapokuja swala la maarifa ni kitu kingine kabisa. Hawa watoto ni makanjanja tu kama watoto wengine wanaosoma kwenye mashule ya kata.

Mpaka sasa sijaona ni kwanini mtoto akanunue Kiingereza kwa shilingi milioni hamsini wakati mtu anaweza kujifunza Kiingereza hata chini ya mti na akabukua vema tu kama makanjanja wengine akina Dayamondi waliojifunza Vingereza magetoni.

Tukiwawezesha hawa walimu wetu uchwara wa shule za Kata wataweza kufundisha kizungu vizuri tu.

Tuanze kudahili walimu ambao wana ufaulu mkubwa badala ya kudahili vilaza wenye MADIVISHENI FOO ati ndio wakawe walimu!

Hili lizingatiwe sana.
 
Kuna international school na kuna English medium hizo international school achana nazo hizo zina watu na hadhi zao.

alafu hizi English medium nadhani ndio unaziongelea wewe of which una point nzuri.
Kuna international school na kuna English medium hizo international school achana nazo hizo zina watu na hadhi zao.

alafu hizi English medium nadhani ndio unaziongelea wewe of which una point nzuri.
Hiyo international school ina kitu gani cha tofauti sana?
 
Maskini mmeshaaza nongwa,

Hapo umeshakula zako kipolo Cha wali na chai ya mdalasin na sigara pembeni
Kwanza, sio KIPOLO ni KIPORO.

Pili, Kiporo cha wali kina virutubisho vingi sana vya wanga ndani ya mwili ambavyo vina uwezo wa kuutia mwili nishati na nguvu.

Tatu, inaonekana wewe hukuweza kupata hata elimu ya shule ya kata, ndio maana huwezi kuandika wala kuelewa umuhimu wa virutubisho vya wanga katika mwili.
 
Bichwa komwe naoma unaindika vitu bila research hakuna walimu vilaza siku hizi shule za kata sema mazingira ya kufanyia kazi ndio yanawapelekea kuwa vilaza
Just imagine mimi mwalimu wa kata naletewa mtoto hajui kuandika jina lake,usiku hakula chakula,anaishi na bibi yake nayeye ndo anategemewa kuihudumia familia, mimi mwalimu wa kata nitatoboa kweli?


Just imagine wewe mwalimu wa international school unaletewa mtoto ambaye hajui kuwa kuna watu tanzania hii wanalala njaa,hajui dhiki yoyote,nani ataoboa?
 
Wengi wao wapo bright sanaa
Wanajiamini, wanajua kazi nje ya masomo kama kupiga vyombo vya mziki, wengine wanaweza kurusha ndege washaanza kufundisha upilot mfano Alpha schools.
Shule za kata wanafunzi wanachoweza ni kukariri notes tu lakini int schools wanaweza vyote.

Wanakua na uelewa na mahusiano na wenzao wa mataifa mbalimbali tofauti na kata
 
Tungekuwa na waalimu wa kufundisha kizungu for kama Kenya au Uganda, tusingeenda hizo, international, lugha ya kimombo ni Swahili ya dunia, kukijua ni muhimu Sana, Dunia ni, kama kijiji, wanaotoa ajira nzuri, ni Hao wanaoongea kizungu vzr!

Al Jazeera yote hqkuna mtangszaji mbongo! CNN yote hakuna mbongo, ukitaka kujua, umuhimu wa, kizungu muulize, Prof Tibaijuka, Dr Steregomena Tax, Dr Asha migiro, au, Muulize Dr Talimba, na Aden rage kwanini watoto wao waliwapereka Vyuo vya Melbourne austaria,au muulize yule kijana Benjamin Fernandes boss wa, NARA, acha kuuliza watu vilaza ambao umwamba wao, unaishia kupiga picha na hauvuki mipaka, Maulid kitenge, Gerald hando, chombo gani kingine ndani, ya Afrika kinaweza kumpa ajira!
 
Hiyo international school ina kitu gani cha tofauti sana?
Mitaala yao ni tofauti kabisa ya hii ya necta kule ni vitendo zaidi wanasoma masomo ya dunia ya kwanza..
Mfano international schools nyingi za hapa bongo zinafundisha biashara sana ndio maana wafanya biashara wengi wakubwaa wahindi, waarabu na wazungu watoto wao wapo huko mzungu hafanyi vitu kwa show off ukiona mzungu amepeleka mtoto wake shule flan na anaisifia ujue hiyo shule inajua.
 
mtoto aliesoma huku na usa are the same na wanaweza pambana pamoja kwenye interviews moja
This is really myopic. Extremely myopic!

Kumbe lengo la kusoma INTERNATIONAL SCHOOL ni kwenda uRaya kufanya interviews na wazungu?

Na kwanini wasome mtaala wa wazungu? ili iweje? wakawe vijakazi wa uRaya?
 
Back
Top Bottom