International passport

Hivi karibuni nimebadilisha passport yangu iliyokuwa imejaa kurasa za Viza, na kabla ya kwenda huko nilipitia humu jamvini na kuisoma hii thread na leo naadika utaratibu mzima niliopitia.

Tarehe 31 May 2011, nilianzia uhamiaji makao makuu Kurasini kuomba mwongozo, niliyemkuta dirishani akanielekeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pale Uwanja wa Taifa, pale nilipewa Form, wakaniambia nizikamilishe kisha nipeleke Makao makuu; sikulipa kitu.
Nilijaza fomu ana siku hiyo hiyo nikamwona mwanasheria kuthibitisha fomu ya dhamana na vyeti vya kuzaliwa, changu na cha moja wa wazazi wangu; hapo nilipa TSh. 15,000 kama legal fee na 500 za stamp duty.

Kesho yake tarehe 01 June, nilienda tena Uhamiaji makao makuu nikiwa na form zangu pamoja na viambatanisho; barua ya maombi, nakala ya passport ya zamani, nakala ya veti vya kuzaliwa; changu na mzazi wangu na kuwasilisha kwa karani kwenye dirisha linalohusiana na aina ya safari yangu. Alizipitia nyaraka hizo kisha akaniandikia pay-in slip ya NMB kulipa TSH. 50,000.

Pale pale uhamiaji kuna dirisha la NMB unalipa kisha unapeleka pay-in slip kwa Mhasibu wa uhamiaji ndio wanakuandikia risiti ya serikali, ukitoka hapo unarudisha fomu zako kwa karani aliyekuhudumia; akaniandikai tarehe ya kupokea pasport baada ya siku 5, kisha akanielekeza kusubiri mtu wa kuchukua finger-print. Nilisubiri kama dakika 10, pamoja na wengine kisha akaja mtu mmoja anaita majina, mnapelekwa sehemu ya electronic fingerprint kisha unaondoka. Tarehe 6 June, nilikwenda Uhamiaji kule mjini (jengo la Wiza ya Mambo ya Ndani) na kukuta passport yangu ikiwa tayari.

Katika process zote hizi, hakuna aliyeniomba chochote au kujaribu kunikwamisha.

Hata hivyo, kila sehemu ya kazi magendo hazikosi, kwani wakati nashughulikia pasi yangu, niliwaona vishoka wakiwa na formu nyingi; wao hawapangi foleni za kawaida bali humpigia simu mtu wao naye huja pale mapokezi na kuwashughulikia kutumia dirisha mojawapo ambalo karani wake labda atakuwa ametoka, kisha wanalipa kawaida lakini ikifika finger-pringting ndipo waombaji halisi huitwa kuto nje ya jengo na kuingia ndani kwa pamoja. Nimefuatilia hii mara mbili nilipokwenda tena kumsindikiza dada yangu aliyekuwa anatafuta pasi; nikaona kuna mtu moja anaye dili na VISHOKA, ni dada mmoja mwembamba mweusi na mara zote anakuwa bize kwenye simu huku akizungunguka huku na kule.
Mwenye experience tofauti anaweza kutuwekea haPA.
 
ku renew ni rahisi saana,....

tabu inakuwa unapohitaji kwa mara ya kwanza....
 
ku renew ni rahisi saana,....tabu inakuwa unapohitaji kwa mara ya kwanza....
Dada yangu alikuwa anaomba pasi kwa mara ya kwanza, alipeleka fomu tarehe 2 June akaipata tarehe 10 June, hatukutoa chochote zaidi ya 50,000 na ada ya mwanasheria 15,000.
 
Passport siku hìzi wala sio kazi kupata wewe fata taratibu. Waeleze tu unataka kuwahi masomo unapata ndani ya siku tatu au nne
 
Back
Top Bottom