International passport | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

International passport

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Straight corner, May 23, 2011.

 1. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hi wana JF!
  Katika harakati za kusaka elimu, nimepata admision ya chuo cha nje na katika harakati za kusaka ufadhili inatakiwa niwe na Passport ya kusafiria nje ya nchi tena ndani ya wiki hii yaani kabla ya 27 May 2011. Baadhi ya watu wameniambia siwezi kufanikiwa ndani ya wiki hii otherwise nitoe mlungura/pesa ya kueleweka! Nimeambiwa gharama ya kawaida ni Tsh 50'000/=.
  Please, nifanyeje au ndio nizitafute hizo pesa tu!
  (Niko Dar es Salaam)
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Anza mchakato, nenda Immigration jaza ile fomu yao weka na picha. Hakikisha umeenda na viambatanishi (mf. Ile barua ya admission, etc.), wanaweza wakaharakisha though itakugharimu kama wiki hivi. Mengine utaelezwa huko
   
 3. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Thanx mkuu, ntajaribu.
  Lakini ni sijaelewa kama kwa procedure za kawaida ni lazima wiki 1 iishe au ni delay ndio inasababisha mda kuongezeka!
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wiki moja ni kawaida kwa muombaji wa mara ya kwanza. Unahitaji siku nzima, au zaidi kutegemeana na foleni, ili kujaza paperwork, finger printing, na uthibitisho mwingine. Then kuna processing yao kabla hawaja-qualify ombi lako, ndio ifuate print work. If its 27th na bado unasita kuanza process, nina wasiwasi na mpango wako. Vipi kuhusu viza?
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nadhani ukiwa na sababu ya msingi na makaratasi yanayoonyesha umuhimu wa wewe kuipata mapema iwezekanavyo wanaweza wakakufanikishia!Muhimu wewe uende pale ukiwa umejiandaa kikamilifu ili kusiwe na usumbufu....bila kusahau vijisenti kidogo maana ndivyo nchi yetu inavyoendeshwa!
   
 6. M

  Mukalabamu Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Pole mkuu.Passport unaweza kuipata hata 24hrs baada ya ombi lako kukubaliwa na kufanya finger printing nk.Ila inabidi uandike barua kwa nini unaitaka kwa dharura na uambatanishe uthibitisho wa dharura yako eg,copy ya barua ya sponsor inayotaka udhibitisho wa passport yako kabla ya muda uliopewa
   
 7. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sorry for late reply, viza pia sina ila nimeambiwa kikubwa ni passport na visa baadaye kwani hata scholarship ndio hii sijaiweka mkononi. Thanx kwa kujali tena!
   
 8. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  Asante sister, pengine unisaidie kujua ni docs zipi niende nazo kupunguza 'njoo baadaye, mara kesho and the like'.
   
 9. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  Mkuu nashukuru sana kwa mchango wako, ntawapa feedback kitakachotokea huko kwenye ofisi za watu!
   
 10. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Kwa mahesabu ya harakaharaka na wewe unashida ndani ya wiki upate hiyo pass kwa gharama ya sh 50,000 nakupa pole kwa hapa bongo! mimi pia nilikua na dharura kama yako ilinigharimu 120,000 na nilipata hiyo pass baada ya wiki mbili na nusu na mimi niko mkoani wala sikutaka kujua bei halali ya hiyo pass baada ya kuipata kwakua waliniahidi nitaipata baada ya wiki moja! jaribu hii ndio bongo mwendo mdundo!
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  *Picha za passport size tano nadhani...background iwe ya rangi ya bahari!
  *Cheti cha kuzaliwa
  *Kwa wewe usisahau barua kutoka huko unapotaka kwenda kusoma inayoonyesha kwamba unahitaji passport asap!
  *Na ada ya fomu na ya soda kidogo!

  Kama nimesahau kitu anaefahamu atarekebisha!
   
 12. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ya soda yanatoka wapi? Mie pale immigration wakati wote nikienda na shida zangu huwa nakamilisha tu documents na siombwi hata senti tano.
   
 13. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani kama ni dharura kweli toka humu JF nenda kafuatilie, navyohisi ni mchecheto wa kupata taarifa kuwa umepata scholarship, hiyo passport unaweza kupata mapema kabisa tena kwa bei ya 50000, nenda na documents kama wadau walivyosema hapo juu mengine utayajua huko huko.
   
 14. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Du, ama kweli kawia ufike ila ni hatari sana mkuu!
   
 15. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante Lizzy, sasa najua japo pa kuanzia! Nimepanga kwenda huko kesho! Stay blessed!
   
 16. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Mkuu ndiyo hali hata mimi niliyokuwa naitarajia, lakini utaona michango ya wengi inaonesha ni kinyume! Nasubiri kesho nijionee mwenyewe!
  Thanx!
   
 17. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35


  Sawa mkuu, kulingana na ratiba nimepanga niende huko kesho!
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  natoka uhamiaje pale posta kufuatili passport ya wife tulikuwa wote, tulianzia pale ofisi ya mkuu wa wilaya temeke tulichukua form tukajaza tar hiyo ilikuwa 12 may tukairudisha tar 13 may ikiwa na cheti cha kuzaliwa cha wife, cha baba yake na mama yake, wife ni mjasiriamali so tukabeba na barua toka serikali za mitaa. ktk ile form wife alijaza yeye ni mjasiriamali tulipofika uhamiaji kurasini yule ofisa alipoona imeandikwa mjasiliamali akamuuliza ni biashara gani unafanya akamwambia saloon eti anataka aone leseni ya biashara wife akamwambia ipo alipoona ipo akajidai eti nimesahau na barua ya mwaliko toka huko unakoenda, jamaa anatengeneza mazingira ya rushwa wife akashangaa. tukatoka nje pale nadhani kuna ka genge flani kanashirikisha wafanyakazi wa uhamiaji na stationery moja pale nje maana tulipotoka tu nje akaja jamaa akatuuliza mmefikia wapi? tukamweleza yaliyotusibu akatuchukua mpaka ndani ya stationery yake akaanza kutupa procedure tuliweka stamp duty moja tu kumbe ilibidi ziwe tatu halafu akatuambia kuna mtu yupo pale kwa hamsini tu tunapata passport, hiyo ni ya mlungula halafu unalipia sasa passport yenyewe alfu arobaini so kitu tisini hicho. tukampa jamaa hamsini yake akaiweka kwenye bahasha akaitwa mshkaji mmoja pale nje akapewa mzigo akamtwangia mama mmoja kule ndani tukaambiwa tumsubiri yupo pale nje kwenye vibanda, sie tukaingia kwa ofisi kumsubiri. dk tano akaingia mama mmoja mfupi hivi yule jamaa tuliyekuwa naye akamfuata wakateta kidogo jamaa akarudi kwetu akamwambia wife mfwate yule mama mwambie nimetumwa na flani, wife akafanya km alivyoambiwa, maza akamwambia wife nicheki dirisha ntakalokaa uje hapo hapo basi mambo yakafanyika kwa haraka tu tukamaliza kulipia wakaahidi within a week itakuwa tayari yaani tarehe 20 may, ijumaa wife akaenda pale posta passport bado tukampigia yule jamaa wa kurasini akasema tuje jtatu yaani leo, leo nao hatujaona jina la wife pale, tukamtwangia yule jamaa wa kurasini akazungumza na mama wa uhamiaji akaambiwa aje afuatilizie pale town, jamaa kaja kazama ndani km dk tano aloorudi akasema tumwachie risiti yeye by tomorrow itakuwa tayari nimerudi home sasa nasubiri kesho.
   
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  so kamanda tayarisha photocopy ya cheti cha kuzaliwa chako cha baba na mama, hiyo barua ya admission barua ya maombi ya passport barua ya serikali za mitaa photocopy ya kitambulisho chako form wanadai zinalipiwa shs alfu kumi pale wilayani temeke uwanja wa taifa lkn sisi tulichukua hatukulipa chochote picha tano zenye background ya blue ukiend photopoint ukiwaambia wanazijua shs alfu tano picha moja itiwe muhuri na mwanasheria au mhuri wa mahakama na kuna sehemu kwenye form ya kiapo mwanasheria ana sign, uwe na mashahidi wawili na wadhamini wawili wata sign kwenye form na address zao hapo form imekamilika.ELFU HAMSINI HIYO TAYARISHA KABSAA na alfu arobaini ya halali kwa passport yenyewe. maana wansema wakikupa ni TEN YRS ndo urudi ku renew wao wale makaratasi tuuuuu? km vipi ni pm nikupe namba ya jamaa akusaidie fasta tuu
   
 20. duda

  duda Senior Member

  #20
  May 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni PM nikuunganishe na mtu wa uhamiaji,atakusaidia ontime
   
Loading...