Intelijensia: Maana, Dhana na Muelekeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Intelijensia: Maana, Dhana na Muelekeo

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Chifunanga, Jul 11, 2011.

 1. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Utangulizi
  Tokea 9/11 vyombo vya usalama wa taifa vimekua vikijihusisha zaidi na masuala ya ulinzi wa mipaka na kutafuta na kuzuia ugaidi. Vyombo
  vya usalama vya nchi nyingi vimefanya marekebisho makubwa baada ya ushauri uliotokana na ripoti na utafiti uliofichua mapungufu yaliyo
  enda kusababisha mabomu ya August 7 1998 Tanzania na 9/11, kutokana na kukosa intelijensia ya kutosha.


  Kumekuwa na mabadiliko hapa kwetu pia, ingawa sio makubwa sana na sio ya wazi kutokana na uhalisi wa kazi. Hata hivyo mambo ya usalama wa taifa yamekuwa yakijitokeza bungeni na inalekea yataendelea kutokea katika siku zijazo.


  Intelijensia sio jambo rahisi kulielewa. Ni jambo ambalo lina mambo mengi sana na limezungukwa na mitazamo potofu. Baadhi ya mambo yanaendeleawa chanzo cha mijadala kati wanausalama na wasomi, na mara nyingi ndani ya kila kundi. Ila pia, kama eneo la kujifunza, intelijensia linainua hisiaza kutaka kuifahamu zaidi. Ingawa hisia hizo hupelekea kusisitiza uchama na mambo yakiusalama ya kipindi hicho bila kuweka misingi kwenye mambo ya muhimu zaidiyanayohusu usalama wa taifa.


  Kama walivyo watanzania wengi, pia wabunge wengi hawajihusishi na mambo ya intelijensia, au kuusikia uzito unaokuja na majukumu ya intelijensia. Baadhi hufatilia. Kwa wale wanaongilia fani hii kwa mara ya kwanza na kwa wale ambao wamekuwepo kwa muda, thread hii inajaribu kuwapa mwangaza wasomaji kwenye maeneo matatu ya intelijensia: asili ya intelijensia, maelezo kuhusu vipengele vyake, na picha kidogo kwenye jinsi serikali inavyofanya kazi za kiintelijensia. Mambo haya yataelezewa kwa juu juu tu, na mambo kadha wa kadha yanaweza kutajwa tu pale itakapokua muhimu kwenye kutaka uelezea kitu fulani.
  Sehemu ya Kwanza: Intelijensia
  Neno intelijensia/usalama wa taifa mara nyingi huwa linahusishwa na kuingiza uwoga au kufanya na kuficha uovu. Ukweli ni kwamba intelijensia ni kama kazi zingine kama uhasibu, au marketing. Kikundi au kampuni yoyote ambayo ina ajenda au mtazamo fulani kitatumia intelijensia kuelekeza matokeo, kuzuia vipingamizi na kuushinda upinzani.
  Sehemu ya kwanza ya thread hii, tutaangalia intelijensia mtu halafu tutaangalia intelijensia idara. Nia ni kuonyesha kuwa kazi za kiusalama kwenye idara na kikundi fulani ni jnsi nyingine tu ya kujaribu kufanya intelijensia mtu kwenye skeli ya ukubwa zaidi. Halafu tutaelezea matokeo ya intelijensia na mzunguko wa intelijensia. Na mwishowe mtazamo, tathmini na haja ya intelijensia itafuata.


  Intelijensia mtu
  Kwanza neno intelijensia linatokana na neno intelligence ambalo linaelezwa kama ni uwezo wa kujifunza, kufikiri na kuelewa mambo, aliokuwa nao mtu, na ni mara chache huelezwa kama taarifa au jinsi ya kupata taarifa mara nyingi kwa kazi za kijeshi au kiserikali. Mitazamo hii inaelezea mambo mawili muhimu. Kwanza, intelijensia inahusiana na maamuzi yatakayochukuliwa, na pili kwamba maamuzi hayo yatatokana na utabiri utakaofanya kutoka kwenye taarifa zilizopatikana.


  ****ngoja nikale kwanza.....nitarudi muda si mrefu*****....HAYA NIMERUDI

  Intelijensia idara
  Kwamba intelijensia mtu kwa upana wake ndio unaunda intelijensia idara sio jambo la ajabu. Intelijensia ni jambo la kawaida kwa mtu, na idara zinaundwa na watu. Hii maana yake sehemu ya Intelijensia ndani ya serikali ni muendelezo tu wa kujaribu kutengeneza intelijensia mtu kwa upana zaidi.

  [imebidi nifanye marekebisho kwenye paragraph hii kwa kushindwa kuweka mambo fulani fulani, mwenye macho na asome]. Idara nyingi za usalama barani afrika, hasa kwa nchi zilizotawaliwa na wazungu, ingawa idara hizo zilianzishwa au kubadilishwa chini ya uongozi uliokuwepo wakati nchi hizo zinapata uhuru, bado mpangilio wake kwa kiasi fulani unafuata mfumo wa Idara mbadala za uingereza. Hivi karibuni wamarekani pia wameweza kuingiza mambo yao kwenye ku'influence' utendaji kazi wa idara hizo. Kwa mfumo wa kiingereza, intelijensia na ukusanyaji wa taarifa ni kitu kimoja. Wataalamu wa intelijensia wa uingereza wanasema kuwa intelijensia inatafsiri na ni sehemu ya kawaida kabisa katika kufanya maamuzi fulani. Wamarekani wao, wanaona intelijensia ni zaidi ya taarifa, kwamba intelijensia ni sawa na taarifa pamoja na tafsiri ya taarifa hizo. Wamarekani wanasema kuwa intelijensia sio tu kupata taarifa na kuzitafsiri kwa nia ya kutolea maamuzi, bali pia ni njia nyingine ya kuelekeza matendo fulani fulani. Wamarekani wanadhani kuwa kazi ya intelijensia sio kutafuta ukweli, bali ni kusaidia kutafanya maamuzi ambayo yataleta mafanikio ya kuukandamiza au kuufuta upinzani.

  Sehemu za intelijensia
  Watu, Idara, Maamuzi, na Matokeo ndio sehemu ambazo intelijensia inafanya nazo kazi. Intelijensia inaanza na kupata taarifa au data, baada ya hapo taarifa hizo zinahakikiwa nakutafsiriwa, baada ya kutafsiriwa zinakuwa elimu. Elimu hiyo inatakiwa kueleweka na kutolewa maamuzi, elimu hiyo pia inabidi iweze kuotea jambo litakalotokea baadae.

  Kama taarifa nyingi zitaletwa kuhusiana na jambo fulani, zikiwekwa pamoja zinaanza kuonyesha jambo ambalo linatokea au linataka kutokea. Na wingi wa taarifa unavyozidi kuongezeka kunapelekea kuwa na elimu kuhusu jambo hilo. Elimu ya kutosha ikishapatikana, jambo hilo litaanza kueleweka na kupelekea kulitolea maamuzi. Uwezo wa kulielewa jambo linalotokea huwa linahusu muda huu, na linaweza kubadilika kwenye muda mwingine mbeleni.


  *********naenda kuangalia ze komedi......nitarudi badae au kesho mungu akipenda ***********
   
 2. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mkuu
  Nadhani ni wakati mwafaka wa kujua maswala haya kwani mara kadha watu wamechanganya shughuli za intelligence officers na zile za CID hali ni vitu tofauti kabisa.

  Kama utaweza kutupa somo hilo litasaidia kuelimisha watu wengi hatujui swala hili kwani limekaa kificho sana.
   
 3. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Kwenye lugha kuna kitu kinaitwa 'euphemism' yaani neno linalotoa picha mbaya kupewa neno jingine kuleta picha nzuri lakini jambo ni lile lile. Mfano: wakati wa ukoloni kule Mtwara kulikuwa na kazi ya kuangamiza panya, job title ya waafrika ilikuwa 'rat catcher' na ile ya wazungu 'rodent officer'. Sasa neno zuri la hiyo kazi ya ufukunyuzi ni 'intellegence' na neno baya ni 'spy' au 'espionage'.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu kwanini unakwenda mbali namna hiyo. Unapozungumzia ujasusi wa US huwezi kuufananisha hata kidogo na wa Tanzania. Mahitaji ya ujasusu hapa Tanzania yanatakiwa kuekelea kwenye uchumi zaidi na ulinzi wa mipaka, lakini ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa hayo yote hayafanyiki. Kazi kubwa inayofanyika ni kukilinda chama na kuwalinda viongozi waliopo. Unaweza kuona kuwa kazi kubwa ni sabotage, assassinations na kazi ambazo hazina beniefits kubwa kwa Tanzania na watanzania, sana sana zina manufaa kwa baadhi ya wanasiasa na matajiri.

  Usijali kazi ya jasusi ni ushushushu, operations officer, muuaji, analyst au manager kazi zote kama zikitekelezwa vizuri zina umuhimu wake. Mnyororo ni vifund0 vyote huwezi kusema kimoja ni muhimu zaidi kuliko kingine.
   
 5. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,199
  Likes Received: 520
  Trophy Points: 280
  Intelijensia...Hardthinking,analysing,way forward/solution+creative imaginations
   
 6. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  This is hard to digest because it depends on the people in the govenment .How they act what they want to do and the like.
   
 7. m

  mwanakalunde New Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It inolves clandestine activities, collection of data and analysis. Sometimes killing in the name of National security!!
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,988
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Hii inaruhusiwa?
   
 9. Nyasirori

  Nyasirori Senior Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Mkuu bado unakula? Maana ni muda mrefu sasa tangu uahidi kurejea.
   
 10. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mh atakuwa out of memory!
   
 11. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkuu, sio kweli kuwa kazi ya TISS ni kulinda chama na kuwalinda viongozi. Kazi wanazofanya ni nyingi kweli, karibia zote ulizoliorodhesha. Ni kwa bahati mbaya sana hawawezi kutangaza kwenye TV au magazeti au redio. Watanzia wengi wanasikia kuhusu hawa watu kutoka kwenye stori za vijiweni na sio authentic sources.
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,054
  Trophy Points: 280
  Tumeshindwa Kibiti
   
 13. Azaria Daudi

  Azaria Daudi Member

  #13
  Jul 2, 2017
  Joined: May 3, 2016
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Samahani Kama kuna topic unaitaka na haionekani kwenye orodha ya jukwaa fulan unaipataje? Mm natafuta hii topic ya siri nzito kuhusu umbo la dunia kwenye jukwaa hili
   
 14. neo1

  neo1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2017
  Joined: Sep 1, 2013
  Messages: 473
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 80
  Mzee the comedy toka 2011....hujamaliza?
   
 15. leiguanan

  leiguanan JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2017
  Joined: Jun 24, 2017
  Messages: 547
  Likes Received: 1,781
  Trophy Points: 180
  Hahahaha
   
 16. Rays Dinho

  Rays Dinho Member

  #16
  Aug 2, 2017
  Joined: Feb 2, 2015
  Messages: 93
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  ngoja tusubiri arudi tufaidike
   
 17. KENZY

  KENZY JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2017
  Joined: Dec 27, 2015
  Messages: 6,253
  Likes Received: 5,248
  Trophy Points: 280
  itakuwa yupo TISS huyu huenda wamembeba!
   
 18. Poise

  Poise JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 6,710
  Likes Received: 6,148
  Trophy Points: 280
  Imebidi ni like post yake Labda atarudi. Aiseee.
   
 19. agent sniper

  agent sniper Senior Member

  #19
  Aug 4, 2017
  Joined: Jul 3, 2017
  Messages: 182
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 60
  Huu ndio ukweli ila watakupinga ila ni moja tu aliyendani ya uwanja ndio anajua namna ya kuucheza mpira mpaka ushindi...kuli mshabiki juu ya jukwaaa .... kama chumba haukilali ni ngumu kukitambua ilie njee

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 20. Poise

  Poise JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 6,710
  Likes Received: 6,148
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Labda, Wamempeleka wapi!?
  Duuuuuuh!
   
Loading...