Serikali ina mkono mrefu na hawana sababu ya kutolea ufafanuzi wa kina wanapozuia kitu kisifanyike. Wana namna na njia nyingi za kupata habari, za kuaminika na kusadikika na zisozo hivyo. Maamuzi mengine yanateghemea muda na kuepusha fadhaa inayoweza kupatikana, na nilimsikia Mwema akisema yawachwe kwa sasa. Jee, huoni kuwa hawa viongozi wanao kaidi amri ya Serikali ndio wakorofi?
Na ukorofi huo wanaoufanya ni kwa faida ya nani? Raia wengi Tanzania hatuungi mkono ufedhuli kwa Serikali. Raia wengi Tanzania hutuungi mkono Maandamano haramu. Raia wengi Tanzania hatuungi mkono chama kisicho kuwa na maamuzi ya amani. Raia wengi wa Tanzania hatuungi mkono siasa za ubabe.
Bw Zomba, post yako umeituma ama kwa sababu hujui unamaanisha nini au unajua lakini kwa malengo ya kupotosha umma, kwa sababu kabla ya kusema kuwa CDM walikuwa na lengo la kuipaka matope nchi, ulipaswa ujiulize yafuatayo;
1) Wageni unaowaongelea walikuja lini Tz, kabla au baada ya kupigwa marufuku mkutano wa kwanza wa CDM hapo December?
2) Wageni unaowaongelea walikuja Tz, au waliomba kuja tz kabla au baada ya polisi kutoa kibali (kilichokuja kufutwa saa chache kabla) cha maandamano?
3) Je, maandamano ni haramu? Sio kwa mujibu wa sheria?, Je, sheria inazuia uwepo wa maandamano kama wapo wageni?
4) Pamoja na wanazoita taarifa za kiinteligensia kuwa maandamano yangeambatana na vurugu, je baada ya CDM 'kulazimisha' maandamano hayo, vurugu zilitokeaje? Ina maana inteligensia ilitabiri vurugu kwa kujua kuwa lazima polisi wangewakabili na kuwapiga waandamanaji?
5) Je, upo mfano wowote katika nchi hii ambapo maandamano halali yamewahi kusababisha vurugu ambazo hazikuchochewa na polisi?
Kumbe basi kwa taarifa yako, inaonyesha kuwa polisi walijua kuwa maandamano yatakuwa ya amani, lakini kwa kutaka kuwaonyesha 'wawekezaji' advertise, wakaamua kuyazuia maandamano hayo kwa nguvu kubwa (ingawa dhaifu), ili wawekezaji waamini kuwa watakuwa salama na serikali itakuwa hata tayari kuua watu ili kulinda maslahi ya wawekezaji.
Lakini wewe bw Zomba na serikali naomba mkumbuke kitu kimoja, hakuna serikali iliyowahi kubaki madarakani milele kwa kutumia ubabe na mabavu. Zaidi sana serikali inazidi kujiongezea chuki, kwa hiki ni kipindi ambacho ilitakiwa iwabembeleze wananchi kutokana na machungu ya ugumu wa maisha: Ukosefu wa umeme, bei ya umeme, nauli, dowans, wizi wa kura, ukosefu wa ajira, kushuka kwa thaamani ya shillingi, nk.
CCM inatakiwa ikumbike kuwa CDM hawakushindwa kwa kutopata kura nyingi zaidi mwaka jana bali kwa kushindwa kuzilinda kura walizopata. hivyo bas CCM wasidhani kuwa chance ya kuogelea kwenye same grace uchaguzi ujao ni kubwa, bali wanatakiwa wadelive, watekeleze ilani ya chama chao kwani kamwe, HAKI YA RAIA WA TZ HAITANYIMWA KWA RISASI.