Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Bado nasubiri majibu yako tafadhali
Demokrasi ni kuingia mitaani na kuanza fujo? Demokrasia ni kukaidi amri ya jeshi la polisi?
Kama mngekuwa mnaijuwa demokrasia msingeyafanya yote hayo. Kwa kipi kikubwa kilichowafanya muingie mitaani na kusababisha umwagikaji wa damu? kama si roho mbaya na fitna na uzabizabina?
You sound like that fisadi bootlicker in state house. Salva someone!Shida yako haswa ni nini? kama kura mmeshindwa, tena vibaya sana. Wabunge hata nusu ya CCM hamjafikia, si msubiri muda wenu ukifika, na siasa zenu hizi za fujo, sasa wa Tanzania ndio kabisaaaaaaa wameshawashtukia. Hata wale wachache waliokuwa wakiwaung mkono, sasa mnawakosa.
Mh. Makamba ( Katibu Mkuu wa CCM) naomba unijibu hata kupitia kwa January Makamba ambaye huwa humu JF kwa jina jingine.
Ulisema CHADEMA hawakutii amri halali.
1. Je ukiwa na barua ya kukuruhusu kuandamana, kisha pakatokeo taarifa kwa mdomo kuwa umezuiwa kuandamana bila maandishi. Utatii amri ipi?
2. Kama polisi walikuwa na taarifa za kiitelijensia kuwa kuna shida itatokea na ndio maana wakawa wengi mno hata kutoka mikoa mingine kuzuia maandamano. Kwa nini wingi huo usitumike kuzuia yaliyokusudiwa katika taarifa hizo za kiitelijensia?
3. Unadhani kama kweli kuna taarifa za kweli zilizoonyesha kusudio lolote baya, je kwa nguvu iliyotumika na maisha yaliyoondolewa na waliojeruhiwa ( waliokuwamo na wasiokuwamo) imesaidia kugeuza ubaya wa yeyote aliyekusudia mabaya au mmewaongezea mashabaki hao waliokusudia mabaya?( kama kweli wapo waliokusudia mabaya)
4. Ni kwa nini vurugu haikutokea kabla ya polisi kuanza kuzuia maandamano?
5. Hata kama umezuiliwa kuandamana lakini ukapewa kibali cha mkutano wa hadhara. Je watu waende kwenye huo mkutano kwa Helkopta ili wasikamatwe kwa kuandamana? Je unaweza kuwawekea watu muda maalum wa kwenda kwenye mkutano mtu moja mmoja ili wasiende kwa pamoja au kwa makundi?
6. Kama kinacholindwa ni UMEYA na siyo wananchi wanaohudumiwa na meya huyo, ukishawaua utawasimamiaje?
7. Je CCM inaiheshimu mamlaka iliyo kuu (katiba) ambayo ndiyo mamlaka kuu kuliko zote?
TAFADHALI NIJIBU.
Viongozi wa Chadema walilazimisha maandamano yafanyike licha ya kuombwa na Mkuu wa Polisi Tanzania kuwa yasifanyike kwa sababu tu:
Walikuwa na nia ya kuwatisha wawekezaji wakubwa duniani ambao wapo Tanzania, huko huko Arusha kwa sasa.
Wawekezaji hao, wakiongozwa na Dhirubhai Ambani walikuwa Tanzania kwa nia ya mapumziko na biashara na kutazama mandhari ya Tanzania na uwezekano mkubwa wa kuwekeza Tanzania.
Kwa roho mbaya tu na kwa nia isiyoyatakia mema Tanzania, viongozi wa Chadema wakahakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa lazima na hata yangeruhusiwa na polisi basi fujo lazima zingetokea ili kuwatisha hao wawekezaji waone kuwa Tanzania si pa kuwekeza.
Yote hiyo, ni kwa sababu tu, ya chuki zao binafsi walizozijenga baada ya kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi uliopita.
Hakuna mantiki yoyote kwa wana siasa walio mahiri kulazimisha maandamano yafanyike wakati kuna wageni, tena wawekezaji muhimu ambao hakuna nchi katika hii dunia yetu ya sasa isiotaka wawepo au watembelee kwao.
Viongozi wa Chgadema kwa ajili tu ya chuki zao binafsi, wakaona hii ndio fursa ya kuipakaza matope (kama si m*v*) Tanzania. Walijuwa kuwa wawekezaji wakubwa kama hawa wanapokuja tena kwa idadi kubwa kama iliowasili hapa, lazima kuna waandishi wa habari wa kimataifa hususan wa mambo ya kibiashara na pia kuna watu wa intelijensia za kibiashara ambao misafara kama hiyo huwa hawakosekani.
Kwa namna ya maisha tunayoishi wa Tanzania au kwa mpenda amani yoyote, hata kama mna ugomvi wenu wa ndani, ajapo mgeni, tena ambae anaweza kuleta manufaa nyumbani kwenu, huwa mnasitisha ugomvi kwa siku mbili tatu mpaka mgeni aondoke. Haya hutokea hata majumbani mwetu, tukipapurana na bahati nzuri au mbaya mgeni akibisha hodi basi mara nyingi kwa wenye akili husitisha kupapurana kwao, wakamhudumia mgenina ikibidi kupapurana, wataendelea mgeni akisha ondoka.
Leo Chadema wameonyesha sura gani ya nchi yetu, kwa kulazimisha maandamano yaliyositishwa na Mkuu wa Polisi, mbele ya hawa wageni?
Nna uhakika, sura walioionyesha si nzuri, lakini, ni matumaini yangu kuwa wenyeji, waliowaalika hawa wageni, wataweza kuwafahamisha ukweli ulivyo na wataridhia si tu kuja tena kutembelea Tanzania, bali na kuwekeza kwa wingi, kwani kwa sasa bado tunahitaji mitaji ya nje.
Nawaomba wa Tanzania walaani kitendo cha viongozi wa Chadema baada ya kuuelewa huu ukweli wa kwanini hawa viongozi walilazimisha maandamano yafanyike.
Mungu awalaze popote apendapo Marehemu waliofarik.
Hizo ndio sababu ambazo hazipingiki, kulikuwa kuna umuhimu gani wa kufanya maandamano wakati kuna wageni? tena ni wawekezaji muhimu? kama si kuwatisha?
Mwanangwa,mtajuta. na bado.
maeneo potential yote yapo chini ya waasi wa fikra.
mtakoma! mtakoma! mtakoma! mtakoma!
wageni wanahusika nini na maandamano.Viongozi wa Chadema walilazimisha maandamano yafanyike licha ya kuombwa na Mkuu wa Polisi Tanzania kuwa yasifanyike kwa sababu tu: