Si kweli. Kama yangu internal ni 32GB, na SD Card ni 8GB zina nafasi za kutosha lakini hata app ya 20MB haiingii
Wakuu hapa mtalalamika sana kama bila kujua yafuatayo
Unapo ambiwa simu ina Gb8 internal hiyo gb8 gawa kwa 2 , ina maana 4gb kwaajili ya media files na 4bg kwaajili ya app hapo hapo tayari sehem ya hiyo 4gb ya app imeshatumika kwa hizo app zilizo kuja na simu.
Chakufanya
1. Punguza app zisizo na matumizi, au zenye kujirudia rudia lakini zina matumizi ya aina moja.
2. Kumbuka ku clear cache kila unapo pata muda.
3. Hamisha media files kenda kwenye sd card kama unayo.
Hasa whatsapp files wengi hawajui kama kila picha au video unazo tuma hujihifadhi kwa siri kwenye folder la whatsapp.
4.Tumia app za kumove app kwenda wenye sd card.
5. Root simu yako ili uweze ku remove app zilizo kuja na simu ambazo huna matumizi nazo.
6. Restore simu yako ianze upya.
Nyingine wadau wataongezea.