Kuna sintofahamu nyingi na za muda mrefu kati ya Uganda ya M7 na Rwanda ya PaKa tofauti na wengi tunavyoiangazia jumla jumla,kufupisha tu ukianzia toka enzi za mapambano ya watutsi tokea uganda wakijaribu kufanya regime change ina kigali kuuangusha utawala wa kihutu wa Habyarimana,M7 used to feel more comfortable with the Late Gen.Fred Gisa Rwigemana ambae alifariki two days before wapiganaji wa Rwandese Patriotic Front hawajavuka mpaka wa uganda na rwanda kuingia rasmi katika ardhi ya rwanda kuondeleza mapambano ya kuitafuta Kigali.Kuhusu kifo chake kuna hadithi yake tata pia,yeye ndio alikua kiongozi wa RPF na ndio angekua kiongozi wa rwanda.M7 aliumizwa sana na kifo cha Gen Rwigema,hakua na jinsi mapambano ilibidi lazima yasonge mbele na lazima pawepo kiongozi,ndio akaibuka kagame ambae ilibidi m7 aanze kujifunza kumzoea na kumuamini na kumtia kwenye plan zake na Gen Rwigema.Then RPF ikasonga mbele ikaingia rwanda na badae yakatokea yaliyotokea ikiwemo kutunguliwa kwa ndege iliyombeba Raia mhutu wa rwanda Habyarimana na mwenzake wa Burundi wakijaribu kutua uwanja wa ndege wa rwanda wakitokea Dar,Tanzania,hakuna anaejua mpaka leo kiuhakika nani waliitungua ile ndege lkn kwa kiasi kikubwa wanahisiwa ni RPF,Japo walikanusha haraka mara tu baada ya tukio kutokea kwamba hawahusiki bali wahutu wenye msimamo mkali waliokua wanapinga mazungumzo ya amani yaliyokua yakifanyika tanzania kati ya habyarimana na RPF kimtindo.Baada ya tukio hilo kila mtu anajua kilichotokea ni mauaji ya kimbari ya watutsi.Mwisho wa siku RPF chini ya PaKa wakachukua nchi.
Sintofahamu za uganda na Rwanda haikuchukua muda zikaanza chini chini,kina Kagame wakihisi their ugandan brothers treated them like kids or as if they supposed to be surbodinate to them,yani kiufupi walihisi M7 anataka kuitawala rwanda na uganda pia na kuwafanya wao vibaraka wake tu.Na kulikua na conversation za wazi kwenye officers mess yao pale kiyovu kati ya kagame akiwa vice president na waziri wa ulinzi kati yake na marehemu patric karegeya wakicomplain kuhusu uganda inavyowatreat.Anyways hivyo ndivyo kutokuaminiana kulivyo anza mpaka kufikia issue za kina kalegeya na nyamwasa kukimbilia uhamishoni badae na yaliyotokea.Ni kwamba kila upande ukaanza kuhisi kuan njama za upande wa pili kutaka kufanya regime change,hofu serious zaidi mwanzo ilianza kwa uganda baada ya uchaguzi 2001,kulijitokeza habari za kikundi cha PRA kikiongozwa na wanajeshi wawili wa uganda col. Antony chakabari na samson mande(google these names kujielimisha zaidi).Iko kikundi trained in rwanda kwa lengo la kumuondo m7 madarakani,badae kukawa na mazungumzo ya pande zote mbili uganda na rwanda na viongozi wa iko kikundi nchini sweden kwa msaada wa jumuia ya ulaya,wakayatuliza.Pia vita ya rwanda na uganda ndani ya congo wakati ule iliacha jeraha kubwa kwa uhusiano wa nchi hizo mbili,inasemekana waganda wengi sana walikufa kwenye ile vita,m7 doesnt wanna let it go mpaka leo.
Pia ni kweli rwanda inaccess na mifumo ya kiintelijensia ya uganda,they monitor everything going on in uganda,iko kitu m7 kinamkosesha raha,ndio mana nae anajibu mapigo kwa kuwaunga mkono RNC -RWANDA NATONAL CONGRESS ya Gen.Kayumba nyamwasa anaeishi uhamishoni south africa ambae kagame amemkosakosa mara kadha kummaliza huko huko south africa akafanikiwa kummaliza patric karegeya kwa kumnyonga kwa mashuka hotelini.
Katika kuidhiti rwanda kujipenyeza kwenye mifumo ya kiusalama ya uganda mwaka jana may 2018 m7 alimfuta kazi IGP wa uganda mganda mwenye asili ya kitutsi General EDWARD KALEKEZI KAYIHURA maarufu kwa jina la KALE KAYIHURA.
View attachment 1044910
Gen.KALE KAYIHURA na mkewe ANGELLA