Insane Anahitaji Huruma, Kusaidiwa. Sio Kulaumiwa, Kulaaniwa na Kususwa! He Needs Help, Tumsaidieje?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,669
119,281
Wanabodi,

Angalizo: Great Minds hawadiscuss watu, wana discuss ideas na kutafuta solutions to the problems.
Hili sio bandiko la kumsema mtu, bali ni bandiko la somo linaloitwa psychoanalysis ambalo linahusiana na kwa nini binadamu fulani, anafanya jambo fulani, au kutenda tendo fulani la ajabu, watu wanashangaa, bila kujua kuwa mtu huyo ana tatizo, na anahitaji msaada, hivyo hili ni bandiko la kutoa solution to the problem ya kitu kinachoitwa, pseudo insanity.

Pseudo Insanity ni Nini?.
Kabla ya kuzungumzia pseudo insanity ni nini, kwanza tuzungumzia insanity ni nini?. Kwa kifupi insanity ni wazimu, mtu anayeitwa insane ni mwenda wazimu, lakini hii pseudo insanity sio wazimu kama wazimu kabisa, bali ni hali ya mtu kurukwa na akili kwa muda, na kupandwa na wazimu wa muda, na kufanya kitendo cha ajabu, kisha akili zake zinamrudia na kujilaumu, kwa nini ametenda kitendo kile. Usually huwa anajuta. Wengi wa watu wanaukubwa na hii pseudo insanity wengi huishia kuwa ma psychopath ambao ni watu wa hatari sana!.

Insanity ni Ugonjwa Kama Ugonjwa Mwingine Wowote, Isane Anahitaji Tiba.
Insanity ni ugonjwa, ni tatizo la kisaikolojia linalohitaji ufumbuzi wa kisaikolojia. Mtu insane ni mgonjwa, ni mtu asiyejielewa, asiyejitambua, hivyo anahitaji msaada wa matibabu kwa kusaidiwa kujielewa na kujitambua, anahitaji kutibiwa ili apone, kwa sababu insane yeye hajijui kuwa ni insane, na sio kulaumiwa, kulaaniwa na kususwa!. Insane is someone who seriously needs help and not ridicule!, hivyo badala ya kumlaumu na kumlaani, tujiulize, tumsaidieje?. Insane is a problem, Watanzania tujifunze kutafuta solutions to the problems sio kulaumu, kulaani, kushutumu na kulalamika tuu. Jee sisi kama Watanzania, tufanyeje kuwasaidia insane wetu?.

Tukio lolote la ajabu likitokea, simple minds wao wana discuss people, watalizungumzia kwa kuuliza nani kafanya nini, ordinary minds wao wana discuss event, tukio, limetokea wapi, limetokeaje tokeaje, limetokea vipi etc, lakini great minds, wao wata discuss ideas, ilikuwaje hadi tukio kama hili litokee, nini chanzo kilichopelekea tukio hilo kutokea?, what was the motive behind na the underlying facts and causative agents, zilizosababisha tukio hilo?.

Kila mtu mzima mwenye akili zake timamu, akifanya jambo la ajabu, watu wenye akili hawaanzi kulaani na kulaumu, bali huanza kwa kujiuliza, inawezekana vipi mtu mzima na akili zake timamu akafanya tukio kama lile, au kituko kama kile?, hivyo unafanya kitu kinaitwa a quick psychoanalysis assesment, ili kubaini chanzo.

Kulipotokea uvamizi wa studio za Clouds, mimi nilifanya a quick psychoanalysis assessment na mara moja tuu nikagundua kuna kila dalili za insanity. Mtu insane akifanya tukio la ajabu au kituko, sio jambo la kushangilia au kulipigia kelele, kushutumu kulaani na kulaumu, na kumsusia au kumtenga, bali ni jambo la kuhurumiwa, kusaidiwa na kutafutiwa tiba kwa sababu wakati akitenda kitendo kile, masikini wa watu hakujua atendalo!. Hata watu wote wanao commit suicide, by the time anaamua kujiua, anakuwa under insanity, akitokea mtu kumstua au kumgutusha, akili zinamrudia, hivyo msifanye masikhara kabisa na watu insane, huanza hivi hivi wasiposaidiwa, huishia kufanya mambo makubwa ya ajabu na mengine ya hatari!.

Kuna watu wengi katika hali ya kawaida kabisa, wanaonekana kama ni wazima na wako timamu kabisa, wala huwezi kuwadhania kuwa ni insane, lakini pindi insanity ikiwaingia, vituko wanavyofanya under insanity, ndivyo vinawatambulisha kuwa sio wazima bali ni vichaa!. Hii inaitwa kughafilika. Kuna wabakaji wengi haswa wale wabakaji wa next of kin, au vitoto vidogo, hawa wote ni vichaa kwa ukichaa wa kughafilika.

Kuwa kichaa sio lazima mpaka mtu aokote makopo au kula majajalani, lakini kuna ukichaa unaitwa "pseudo insanity" ambapo mtu ni mzima kabisa, anarukwa na akili kwa muda mfupi, anaghafilika, anafanya tukio, au kituko, kisha akili zinamrudia, anakuwa haamini kuwa ni yeye aliyefanya tukio hilo au kituko hicho!. Lakini wengi wa insane hawa, akili zikiisha warudia, kwanza watanyon'gonyea, kisha watatahayari, na mwisho hujuta na kuomba msamaha!.

The best thing to do kwa mwenye akili timamu, ni kujutia na kuomba msamaha!. Ukiona insane ametenda jambo la ajabu na hajutii, ujue huyo sii mzima, ni mtu anayehitaji msaada, its a temporary rightmove kwa media kumuepuka ili kumstahi asizidi kujiaibisha, yaani shun him out temporarily, lakini sio kumsusia habari zake, huku ni kuwasusia wananchi anaowatumikia. Hili la viongozi vichaa, nimelisema hapa
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...

Japo mimi sio mtaalamu wa hii psychoanalysis lakini nimepitia juu juu kwa kusoma maandishi ya Sigmund Freud na kusomea Jung Psychology, hivyo kuna vitu vya ajabu binadamu anavifanya ambavyo vinasabishwa na msongo wa mawazo ya mateso ya utotoni na kusababisha kitu kiitwacho "deep rooted neurosis" ya kumbukumbu ya maumivu na mateso ya utotoni, au kupigika kimaisha yaliyohifadhiwa kwenye subconscious mind, sasa ukijumlisha na "karma" affects za mapito ya maisha ya mtu aliyopitia, pressure za kazi, maisha, ndoa, utajiri wa ghafla, kupendwa sana na mfalme, bad media publicity, siri za kuiba jina na kufoji vyeti vya watu ambazo mwanzo zilikuwa ni well kept secrets, sasa ziko to an open,etc, etc, hivyo mtu hujikuta anapata depression, anafanya mambo ya ajabu ajabu, watu wanashangaa na kumlaumu, wengine kumlaani, bila kujua chanzo, kisababishi na the motive behind, laiti wangelijua, wangegundua ni mtu anayehitaji zaidi kuhurumiwa na kusaidiwa kuliko kulaumiwa, kulaaniwa, kushutumiwa na kususiwa!.

Kitendo alichokifanya mtu isane kuvamia Clouds Media lengo ni kumflict pain kwa mtu insane mwingine kutokana na maumivu aliomsababishia. Hii ni sadism, hufanywa na ma sadists. Kile kitendo cha kulia madhabahuni ni some form of pain release, ila kwa pain za deep rooted neurosis haziishi kwa kulia tuu au kumwaga chozi madhabahuni kwa kumlilia Mungu, bali mtu anakuwa kama mdudu nge, nge akichachamaa huinua mkia juu na ku sting, chochote anachokutana nacho, ndipo pain zinakuwa released kwa kuinflict pain kwa wengine, hivyo mtu mmoja alimtumia huyo mzazi na mtoto aliyetelekezwa ambaye nae ni insane, kuinflict pain kwa mtu insane mwingine, ili na yeye aumie kama yeye alivyoumia, hivyo yeye kupata gratification kwa maumivu yake ya ndani. Hili nimelizungumza kwenye
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta ...

Katika sakata hili, muathiika mkubwa kabisa ni yule mtoto an innocent victim anayelelewa na insane mother aliyetelekezwa ambaye ni an innocent victim!. Sijui kama mama yule alijua anatumika na alilipwa kiasi gani?!, ila kwa nguvu alioitumia kuvamia Clouds, wale vijana wa shilawadu, watakuwa nao walidakishwa mtonyo wa nguvu kwa ahadi ya kuitangaza habari hiyo ili kumkomoa fulani, na usikute hata kwa huyo mdada pia ni insane ndio aliwalengesha, ndio maana alikwenda pale kwa hasira with full force na makirikiri ili kufidia mtonyo wake, watu wavute mtonyo, waseme watatoa, halafu hawajatoa, hata ningekuwa mimi, ningekasirika!.

Kwa vile muathirika mkuu ni kale kachanga, kwanza kama ni kweli mchungaji ndie mhusika, then he has to be responsible kutoa matunzo kupitia ustawi wa jamii, na ikibidi kisheria kwa kuhusisha vipimo vya DNA.

Kwa sisi tuliopitia hiyo psychoanalysis, kwa kumsikiliza tuu huyo mwanamke, utagundua, she is insane!, mtu asiye na mahali pa kuishi, anayelala kanisani, can do anything with anyone, hivyo you never know ni watu wangapi wengine aliwahudumia!. The bottom line ni mtoto asaidiwe!. Mtu anaemtumia mtu mwingine insane ili kuinflict pain kwa adui yake, pia ni insane, anahitaji kusaidiwa, ila pia mtu anaemsupport huyo isane na kunyamazia vitendo vya insanity, nae need his head, seriously be examined!.

Tupo tuliolaani, tuliolaumu, tulioshutumu, tulio beza, lakini tunaweza kuwa tulifanya yote haya kwa kutojua kuwa tuna deal na a mental case ya insanity, baada ya kujua hili, Watanzania tuingiwe na huruma ya shauku ya kuhurumiana na kusaidiana, na mimi pia nitasaidia.

Insanity ziko za aina nyingi na levels tofauti, kati ya inanity zote, pseudo insanity ndio the hardest to detect kwa sababu ni kichaa cha muda tuu, kinapanda mtu anafanya tukio kisha kinayeyuka anakuwa normal kabisa and you can't tell. Ma sex maniacs na ma psychopaths wako kwenye kundi hili. Usually insane hajijui ila walio sane ndio wanaobaini mwenzao ni insane, sasa ikitokea mtu ni insane na kuna watu wanaviona hivyo vitendo vya insanity as just normal na kumpongeza, then they might be insane as well ila hawajijui.

Ziko pseudo insanity zinazosababishwa na alcohol intoxication hivyo kutenda vitu vya ajabu ukilewa, ukiwa sober, inajuta.

Kuna insanity ya groups psychology ambapo kundi la watu wanampiga mwizi wa kuku hadi kumuua kwa kumwagia mafuta na kumchoma akiwa hai, halafu watu hao hao wanashangilia mafisadi kama ya EPA kusamehewa!.

Pia kuna pseudo insanity ya daredevils kafanya jambo la hatari, likifanikiwa unaonekana shujaa likibumba unaonekana kichaa kama watu wanaohudhuria mikutano na maandamano yasiyo na vibali.

Kama katiba imetoa haki hizo na zile, na kuna taratibu, sheria na kanuni za kudeal na kila situation halafu mtu akaibuka na kwenda kinyume cha katiba au kutaja taja tuu majina ya watu na kuwatuhumu bila ushahidi, japo ni ushujaa lakini ni insanity.

Situations za matukio ya everyday events kwenye familia zetu nayo ni insanity. Mtu yoyote anayepiga mke wake, wanaume anayetelekeza família, mwanamke anayetelekeza kichanga chake, ulevi wa kupindukia, wizi na udokozi, tabia za u play boy. Wadada wanaojiuza, umbeya, ufukunyuku, kupiga chabo, etc etc vyote hivi ni insanity.

Hata mimi binafsi nikitumia usafiri wa boda boda kwa sababu unafika haraka kuliko gari, nilipoutumia kwenda rough and very fast, sikujua nilikuwa under insanity hadi yaliponikuta ya kunikuta, hivyo hata hili bandiko linaweza kuwa ni la insanity, only the sane ones ndio watatambua na insane wenzangu na mimi hatuwezi kutambua. Insane huwezi kumrekebisha insane mwenzake, hivyo naomba ukiliona hili bandiko ni too offensive, unaweza kuwa wewe ndio uko sane, liripoti kwa mode lifungwe.

Namalizia kwa kusisitiza, mtu insane anahitaji kuonewa huruma, kusaidiwa, kufarijiwa na sio kulaumiwa, kulaaniwa kulaumiwa, kususiwa na kutengwa!, this man needs help seriously, Jee tumsaidieje?. Naombeni tushirikiane kutoa mawazo positive jinsi ya kuwasaidia insane hawa, tufanyeje?!.

N.B tunaomba mawazo na ushauri tuu, please hakuna kutaja majina!, hatuzungumzi watu hapa tunazungumza ideas.

Jumatano Njema
Paskali
Update 1. Iwapo tatizo la insanity litamtokea mkuu wa nchi, katiba yetu imeweka utaratibu ufuatao kushughulikia tatizo hili endapo litatokea.
1. Baraza la Mawaziri.

Katiba No. 37


(2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya akili, laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania, na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais kutokana ya akili, hamudu kazi zake; na iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.
Update 2: Huu ni ushauri wa kidakitari wa jinsi ya kusaidia
Katika elimu ya matibabu ya matatizo ya akili kuna kitu kinaitwa INSIGHT,kabla hujaamua kumpatia mgonjwa matibabu lazima ufanye Mental State Examination na hii ndio itakuambia kama mgonjwa ana good insight au poor insight.Good ni pale mgonjwa anapotambua kwamba ni mgonjwa kweli na anahitaji matibabu na Poor ni pale inapokuwa kinyume chake yaani mgonjwa hajioni kama mgonjwa na isitoshe hahitaji matibabu na labda sometimes anakuona wewe daktari ndiye mgonjwa.

Huyu mwenye Good insight unaweza fanya just psychotherapy au Cognitive behavioural therapy au hata occupational therapy na akapona vizuri but huyu mwenye poor insight mpaka sindano zinaweza zisifanye kazi kwake.

Insight haikusaidii tu kuchagua aina ya matibabu lakini pia inakusaidia kujua prognosis(hatima ya mgonjwa) kwani akiwa na good insight wengi hupona na akiwa na Poor insight expect the worst or atleast the most evil.

In relation to your topic,Kabla ya matibabu lazima mgonjwa akubali kwamba ni mgonjwa na kweli anahitaji msaada otherwise ni kazi bure.Hatofaidika chochote na matibabu yetu.

cc Paschal Mayalla
Mkuu Magafu, asante sana kwa bandiko hili ambalo ndio msaada mkubwa wa kwanza very objective katika kumsaidia huyu kijana mwenzetu.
Wengine tuendelee kuchangia objectively kwa lengo la kusaidia.

Paskali
 
Sasa hawa wamefukuzwa kazi mbona hatuwapi nafasi ya kuonewa huruma?sheria zifuate mkondo wewe umezungusha mwandiko wako ila danganya wajinga wenzako,nchi hii inaongozwa na sheria kuleta upendeleo ety baadhi ya watu wakikosea wasaidiwe wengine jela ni double standard,pasco jielewe wewe mnafiki sana huna jipya
 
Sasa hawa wamefukuzwa kazi mbona hatuwapi nafasi ya kuonewa huruma?sheria zifuate mkondo wewe umezungusha mwandiko wako ila danganya wajinga wenzako,nchi hii inaongozwa na sheria kuleta upendeleo ety baadhi ya watu wakikosea wasaidiwe wengine jela ni double standard,pasco jielewe wewe mnafiki sana huna jipya
Nilikuwa napenda sana kujifunza mengi kwa pasko lakini njaa imeshampoteza kwenye misimamo yake.
 
Wanabodi,
Angalizo: Great Minds hawadiscuss watu, wana discuss ideas na kutafuta solutions to problems.
Hili sio bandiko la kumsema mtu, bali kutoa solution ya tatizo la insanity. Insanity ni tatizo la kisaikolojia linalohitaji ufumbuzi wa kisaikolojia. Mtu insane anahitaji kuhurumiwa, anahitaji msaada wa kusaidiwa kutibiwa kwa sababu yeye hajijui kuwa ni insane, na sio kulaumiwa na kulaaniwa na kususwa!. He is someone who seriously needs help, hivyo tujiulize, tumsaidieje?. He is a problem, Watanzania tujifunze kutafuta solutions to the problems sio kulaani, kushutumu na kulalamika tuu. Jee tufanyeje kumsaidia mtu huyu katika matatizo yake?.

Tukio lolote la ajabu likitokea, simple minds wao wana discuss people, watalizungumzia kwa kuuliza nani kafanya nini, ordinary minds wao wana discuss event, tukio, limetokea wapi, limetokeaje, limetokea vipi etc, lakini great minds, wao wata discuss ideas, ilikuwa hadi tukio kama hili litokee, what was the motive behind na the underlying facts and causative agents, zilizosababisha, inawezekana vipi mtu mzima na akili zake timamu akafanya tukio kama lile, hivyo unafanya kitu kinaitwa a quick psychoanalysis, na mara moja tuu nikagundua kuna insanity. Mtu insane akifanya tukio, sio jambo la kushangilia au kulipigia kelele, kushutumu kulaani na kulaumu, na kumsusia au kumtenga, bali ni jambo la kuhurumiwa, kusaidiwa na kutafutiwa tiba!. Watu wote wanao commit suicide, huanza hivi hivi, msifanye masikhara!.

Kuna watu wengi katika hali ya kawaida kabisa, wanaoneka ni wazima na ni timamu kabisa, wala huwezi kuwadhania kuwa ni vichaa, lakini vituko wanavyofanya, ndivyo vinawatambulisha kuwa sio wazima bali ni vichaa!. Kuwa kichaa sio lazima mpaka mtu aokote makopo au kula majajalani, lakini kuna ukichaa unaitwa "pseudo insanity" ambapo mtu ni mzima kabisa, anarukwa na akili, anafanya kituko, kisha akili zinamrudia, anakuwa haamini kuwa ni yeye aliyefanya hivyo, kwanza atanyon'gonyea, kisha atatahayai, na the best thing to do kwa mwenye akili timamu, ni kujutia na kuomba msamaha!. Ukiona insane ametenda jambo la ajabu na hajutii, ujue huyo sii mzima, ni mtu anayehitaji msaada, its a temporary right move kwa media kumuepuka ili kumstahi asizidi kujiaibisha, yaani shun him, lakini sio kumsusia habari zake, huku ni kuwasusia wananchi anaowatumikia. Hili la viongozi vichaa, nimelisema hapa
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...

Japo mimi sio mtaalamu wa kitu kinachoitwa psychoanalysis lakini nimepitia juu juu, hivyo kuna vitu vya ajabu binadamu anavifanya ambavyo vinasabishwa na msongo wa mawazo ya mateso ya utotoni na kusababisha kitu kiitwacho "deep rooted neurosis" ya maumivu yaliyohifadhiwa kwenye sub conscious mind, sasa ukijumlisha na "karma" effects za mapito ya maisha ya mtu aliyopitia, pressure kazi, maisha, ndoa bila mtoto, utajiri wa ghafla, kupenda na mfalme, bad media publicity, siri za kuiba jina na kufoji vyeti zimefumka, etc, etc, hivyo mtu hujikuta anafanya mambo ya ajabu ajabu, watu wanashangaa na kumlaumu, wengine kumlaani, bila kujua chanzo, kisababishi na the motive behind, laiti wangelijua, wangegundua ni mtu anayehitaji zaidi kuhurumiwa na kusaidiwa kuliko kulaumiwa, kulaaniwa, kushutumiwa na kususiwa!.

Kitendo alichokifanya mtu isane kuvamia Clouds Media lengo ni kumflict pain kwa mtu isane mwingine kutokana na maumivu aliomsababishia ni sadism, hufanywa na ma sadists. Kile kitendo cha kulia madhabahuni ni some form of pain release, ila kwa pain za deep rooted neurosis haziishi kwa kulia tuu au kumwaga chozi, bali mtu anakuwa kama mdudu nge, nge akichachamaa huinua mkia juu na ku sting, chochote anachokutana nacho, ndipo pain zinakuwa released kwa kuinflict pain kwa wengine, hivyo mtu mmoja alimtumia huyo mzazi na mtoto aliyetelekezwa ambaye nae ni insane, kuinflict pain kwa mtu isane mwingine, ili na yeye aumie kama yeye alivyoumia, hivyo yeye kupata gratification kwa maumivu yake ya ndani. Hili nimelizungumza kwenye
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta ...

Katika sakata hili, muathiika mkubwa kabisa ni yule mtoto innocent anayelelewa na isane mother aliyetelekezwa ambaye ni an innocent victim!. Sijui kama mama yule alijua anatumika na alilipwa kiasi gani?!, ila kwa nguvu alioitumia kuvamia Clouds, wale vijana wa shilawadu, watakuwa labda walidakishwa mtonyo wa nguvu kwa ahadi ya kuitangaza, na usikute hata kwa huyo mdada pia ni isane ndio aliwalengesha, ndio maana alikwenda pale kwa hasira with full force kufidia mtonyo wake, watu wavute mtonyo, waseme watatoa, halafu hawajatoa, hata ningekuwa mimi, ningekasirika!.

Kwa vile muathirika mkuu ni kale kachanga, kwanza kama ni kweli mchungaji ndie mhusika, then he has to be responsible kutoa matunzo kupitia kiustawi wa jamii, na ikibidi kisheria kwa kuhusisha vipimo vya DNA.

Kwa sisi tuliopitia hiyo psychoanalysis, kwa kumsikiliza tuu huyo mwanamke, utagundua, she is insane!, mtu asiye na mahali pa kuishi, anayelala kanisani, can do anything with anyone, hivyo you never know ni watu wangapi wengine aliwahudumia!. The bottom line ni mtoto asaidiwe!. Mtu anaemtumia mtu mwingine insane ili kuinflict pain kwa adui yake, pia ni insane, anahitaji kusaidiwa, ila pia mtu anaemsupport huyo isane na kunyamazia vitendo vya insanity, nae need his head, seriously be examined!.

Tupo tuliolaani, tuliolaumu, tulioshutumu, tulio beza, lakini tunaweza kuwa tulifanya yote haya kwa kutojua kuwa tuna deal na a mental case ya insanity, baada ya kujua hili, Watanzania tuingiwe na huruma ya shauku ya kuhurumiana na kusaidiana, na mimi pia nitasaidia.

Namalizia kwa tulikusisitiza, Mtu Insane Anahitaji Kuonewa Huruma, Kusaidiwa, Kufarijiwa na Sio Kulaumiwa, Kulaaniwa kulaumiwa, Kususiwa na Kutengwa!, This Man Needs Help Seriously, Jee Tumsaidieje?. Naombeni tushirikiane kutoa mawazo positive jinsi ya kuwasaidia insane hawa, tufanyeje?!.

N.B tunaomba mawazo na ushauri tuu, please hakuna kutaja majina!, hatuzungumzi watu hapa tunazungumza ideas.

Jumatano Njema
Paskali
Tired of you please, stop posting!
 
Bhebhe nkoi, chuu. Hata kama sijaoa na kupata mtoto bado ila ile kadi ya clinik nikipewa kufoji nadhani nitaifoji vizuri sana zaidi yao.Chanjo ngapi per day?kalam na mwandiko ule ule toka amezaliwa.
 
Ndugu yangu pasco cha muhimu ni kumpeleka hospital Ili kumpima akili zake . Ikiwa doctor atasema hana Tatizo itabidi tumuanzishe form one Ili kutatua chanzo cha Tatizo ambacho ni kufeli kidato cha nne Na kuamua kutumia vyeti vya mtu.

Akishamaliza form four sasa tutaanza kuchukua hatua za kisheria kwa kosa lake la awali la kutumia vyeti vya mtu.
 
Aweke vyeti na kukubali kakosea ili sheria ichukue mkondo wake ili apatiwe tiba na nafsi yake iwe huru, lakin ukisema aonewe huruma wakati ana makosa haiingii akilini na kama mmegundua ni kichaa na mmeamua kumlinda muacheni aivuruge nchi
 
Back
Top Bottom