Nianze kwa kusema kwamba mimi sina team, ila nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa muziki wa Tanzania kila nipatapo muda.
Ninavutiwa sana na Muziki wa Diamond na namna anavyochukulia muziki kama kazi, jamaa anajitambua na anaelewa kuwa muziki ndio mlo wake.
Ukilinganisha sasa hivi na miaka ile ya 2009/2010 wakati anaanza muziki unaona kabisa jamaa amepiga hatua kubwa sana. Sasa hivi ukimsikiliza anavyoongea, content ya anachokiongea, na muonekano ni mbingu na ardhi na alivyokuwa 2009/2010.
Hili ni somo hata kwetu tujitahidi kupenda kile kinachotupa mkate wa kila siku, tujitahidi kuwa bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda.
Huu wimbo alioshirikishwa unaweza sema hastahili pongezi zozote kwa sababu kashirikishwa, lakini ukiungalia kwa undani ana mchango mkubwa sana. Kuna vionjo flani unaviona kabisa vya Mondi, kuna dancing styles unaziona ni za Mondi. Kuna sehemu Mondi anadance unaona kabisa anakuwa admired/revered na dancers, mfano kuna sehemu dancer mmoja wa kike anacheka. Unaona kabisa pamoja na kwamba wimbo ulikuwa ni hit song tayari lakini mwana anabring x-factor kwenye remix.
Moral of the story ni kwamba tukishatambua tunachokipenda, tufanye kazi kuwa bora zaidi kila siku.