Inglishi ya zamani

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,076
Natanguliza salamu zangu mbele kama tai,ni hivi wakati tuko shule ya msingi mwalimu wa kiingereza aliwahi kutufundisha kwamba neno lolote ktk lugha ya kiingereza linaloanzia na herufi A E I O U,lazima uanze na neno AN mifanoz:
A.an animal,an elephant,an onion, na mengineyo
Ila mimi nilimuuliza mwalimu
Je?Aunt nitamuita an AUNT.mwalimu akaona haiwezekani kusema an Aunt akasema ni Kiingereza kipya wakati yy anasoma hakikuwepo,kuna ukweli wowote katika hili?
La pili pia aliwahi kusema kwamba neno lolote linaloishiwa na herufi ER lina maana ya huyo mtu anayefanya kitu hiko mifanoz:
Walk=walkER
Teach=TeachER
Fight=fightER
Kick=KickER na mengine mengi
Mimi pia nikamuuliza mwalimu maneno haya nayo yamekaaje maana yanaishiwa na ER
1:SupER
2.WatER
3:powER
Pia akaniambia hiko ni Kiingereza cha zamani,Je?kuna ukweli wowote ktk hilo,naomba msaada kwa wale wanaojua lugha ya inglishi






Happy Birthday for Ya Exam!!!
 
nami nlifundishwa matamshi haya TO,DO yanasauti sawa yaani TU,DU ..nkamuuliza mwalimu je GO=GU....hakunijibu!
 
Back
Top Bottom