Ingeweza kuwa mbaya zaidi

Ingeweza kuwa mbaya zaidi

livingafrican

Member
Joined
Jun 11, 2009
Posts
58
Reaction score
19
Kuna mjita mmoja ambaye alizoea kusema "hii ni sawa,hali ingeweza kuwa mbaya zaidi". Kila watu wakimweleza matatizo yao jibu lake ni hilo hilo. Siku moja jirani yake alirudi kazini mapema na kumkuta mke wake akifanya mapenzi na mangi. Kwa hasira akawapiga risasi akawaua na yeye akajiua. Majirani walipofika kwenye msiba kila mtu akawa anasikitika na kulaani.Mjita kama kawaida alipofika akaanza kusema "hii ni sawa,hali ingeweza kuwa mbaya zaidi". Kila mtu akamshangaa na kumjia juu ,unamaanisha nini?.ngewezaje kuwa mbaya zaidi ya haya?. mjita akaangalia chini na kusema " kama angerudi mapema jana mi ndo ningekuwa maiti badala ya mangi"
 
Back
Top Bottom