Ingekuwa ni wewe ungemshaurije?

Ingekuwa ni wewe ungemshaurije?

Good Neighbour

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2017
Posts
942
Reaction score
898
Majuzi mdogo wangu alinitembelea nyumbani baada ya stori za hapa na pale akanieleza sababu ya kunitembelea.Akanieleza kuhusu matatizo yanayomsibu katika mahusiano yake,maelezo yake yako hivi.

"Bro nimekaa na mchumba wangu kwa muda wa miaka miwili sasa licha ya tofauti zetu za kidini mimi kuwa mkristu na yeye kuwa muislam,Kwa umri 29 na yeye 24 miaka.Mchumba wangu huyu ana mtoto mmoja ambaye anaishi kwa wazazi wa mwanaume aliyeachana nae,Nilitokea kumpenda sana huyu mwanamke lakini naona kadri siku zinavyokwenda ni kama yeye anakuwa chanzo cha kufanya mapenzi yangu kwake yapungue tena kwa kiwango kikubwa sana!Mapenzi ndio yalinifanya:-

1.Nikomae kiume nihame toka kwenye kupanga chumba na kwenda kupanga nyumba nzima kama ambavyo alikuwa akitamani siku zote

2.Nimepigana vita ya jihad kuhakikisha anakuwa na simu nzuri kama ambavo siku zote ametamani(yenye thamani ya zaidi ya 1.4M) "aliimba msanii O-ten,akipendacho binti mwanaume lazima atanunua"

3.Japo wanasema hutakiwi kukumbushia ukisamehe lakini Nimemsamehe makosa mengi sana hapo nyuma yakiwemo kuchelewa kurudi om bila taarifa na kurudi akiwa amekunywa/lewa zaidi ya mara 15,kuchelewa kupika,kuondoka bila kuaga

4.Nivumilie majibu yake mabaya,kununa nuna bila sababu,kumhudumia kwa kadri Mungu alivyonibariki katika haso zangu

5.Kutulia na kufocus na yeye na kuwaweka wanawake wengine kando ili kutengeneza future na yeye lakini naona kama bado hanielewi

Sasa kila nikimtazama namuona kama mtu ambaye hana focus,huwezi amini kwa miaka yote hii miwili hakuna siku aliyowahi nambia tujadili jambo la msingi au maendeleo zaidi ya kuomba hela za matumizi.
nlimwahidi kumfungulia biashara lakini napata hofu na wasiwasi mkubwa kama ntapigwa hela sababu sioni focus yake katika maisha.

Kwa miaka yote hii miwili amekuwa ni mtu ambaye yupo tu home hana msukumo au kuonyesha dalili zozote za kutaka kufanya kazi ni mpaka mimi nianzishe mada na kumwambie nataka afanye kazi sababu maisha yanabadilika.

Mpaka leo ni mtu ambaye hawezi kukwambia kazi njema ukitoka wala kukwambia za kazi au pole na kazi ukirudi na akifanya hivyo ni mpaka ajiskie tu
Tumekuwa tukigombana mara kwa mara hasa mwaka huu na mara nyingi tukigombana basi yeye huamua kuondoka na kwenda kwao sababu si mbali sana na hapa tunapoishi(sh 1000 tu kwa boda boda) na atakaa kimya asinitafute mpaka mimi ntakapomuanza.

Kisa hiki ndio kilichonleta kwako,majuzi baada ya kuamua kumtoa out sababu muda mwingi anakuwa bored kuwa home tukawa tumepata kilevi(wote tunakunywa).Tukiwa bar kuna majibu alinipa ambayo sikupendezwa nayo,tulivofika om aliendelea kunijibu vibaya nikaamua kumpiga naye akaamua kuchukua mawe na KUPASUA VIOO VYA GARI YANGU kama namna flani ya kulipiza kisasi na matusi juu,ambapo ameniingiza katika gharama kubwa za kutengeneza gari na ukizingatia bado namhudumia yeye,nalipa kodi+majukumu mengine

Baada ya kisa hiki nimekuwa nikiwaza mambo mengi hasa nikijumlisha na hayo yote nliyokuhadithia.kwasasa tupo hatuongei sana kama mwanzo ila tunaishi pamoja mimi nikienda kwenye mishe zangu huku yeye akiwa yuko home,Je wewe unanishaurije kuendelea nae au kuachana nae?

Je ungekuwa wewe ungemshauri nini Dogo?
 
alishakosea toka mwanzo..waswahili wasema SAMAK MKUNJE ANGALI MBICHI.
toka mwanzo dogo angeweka misimamo mikali hayo mazoea yasingekuwepo!
wanaume wengi siku hizi wanadekeza sn wanawake hivyo kupelekea mwanamke wako kukuona wee km mwanamke mwenzie..
Uuna ukweli mkubwa sana hapo nakubaliana na wewe.Sasa unamshaurije?
 
Ungekuwa ni kaka/dada ungeshaurije tukiacha wazazi kwanza
Ningemwambia atafute mwanamke ambaye hana mzigo. Maana hii itampa taabu.Pia suala la dini aliangalie hasa kama yeye ni mkristo. Waislam mara nyingi wanaruhusu mtu wao kuoa au kuolewa ilmradi anayefanya hivyo abadili dini lakini siyo wao kubadilishwa dini. Hata kama tunajidanganya kuwa hatuna udini, upo na ni tatizo kwenye mahusiano ya kudumu. Mdogo wako ajue hatafuti rafiki bali mtu wa kufa naye.
 
Anatha souljar down, kiukweli hawa viumbe siku zinavozidi kwenda nao wanakuwa heartless sana cases za hawa watu kutokuwa na shkurana na mimi pia ni muanga wa ilo jambo, lakini cha kujifunza kaa na mwanamke anayekupenda sio unayempa wewe sana utaishi kwa amani na utaenjoy lakn kunyume chake utapata heart break kubwa kuliko rift Valley.

MAPENZI NI UGONJWA WA AKILI, VIJANA TUJENGE TAIFA.
 
Atemane nae tu.

She is a disturbed woman atampotezea focus ya maisha yake.

Alitakiwa awe humble na anyooke hasa kwa vile amekutana na mwanaume aliemkubali pamoja na kwamba ana mtoto tayari.

Drop her! She ain't worth your time, efforts or energy.
 
kuna ukweli mkubwa sana hapo nakubaliana na wewe.Sasa unamshaurije?
nothing is impossible under the sun.
there is no way always there is a way.
kwa wao binafsi hawawezi kumaliza hizo tofauti zao sababu akisema alazmishe huyo samaki atavunjika!!
na ishu mbaya zaidi km hajamtambulisha popote hapo pia kutakuwa na sintofaham!!
ajaribu kwa watu wazima ambao wanaweza kuwakalisha chini wakapewa somo zuri la mahusiano labda atabadilika.
 
Ningemwambia atafute mwanamke ambaye hana mzigo. Maana hii itampa taabu.Pia suala la dini aliangalie hasa kama yeye ni mkristo. Waislam mara nyingi wanaruhusu mtu wao kuoa au kuolewa ilmradi anayefanya hivyo abadili dini lakini siyo wao kubadilishwa dini. Hata kama tunajidanganya kuwa hatuna udini, upo na ni tatizo kwenye mahusiano ya kudumu. Mdogo wako ajue hatafuti rafiki bali mtu wa kufa naye.
Asante kwa ushauri makini
keeping black to black and throwing white to white suala la dini lipo sana Tu
 
Atemane nae tu.

She is a disturbed woman atampotezea focus ya maisha yake.

Alitakiwa awe humble na anyooke hasa kwa vile amekutana na mwanaume aliemkubali pamoja na kwamba ana mtoto tayari.

Drop her! She ain't worth your time, efforts or energy.
There is a very high degree of Truth in Thy words.
Nakuunga mkono kwa kiasi kikubwa sana
 
Back
Top Bottom