Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,803
Sijui ni hofu,woga,ukada au nini? Vyombo vya habari vya TZ havitulishi habari vile inavyotakiwa nadhani ndio maana watanzania tunaishi kwa habari za umbea na ushabiki usiokuwa na maana, kwa sababu tunapewa habari za juu juu mno na vyombo vyetu vya habari. Hakuna uchambuzi makini wa mambo hasa yanayotokea ndani ya nchi yetu.
Juzi tu hapa tumesikia viongozi wa juu wakitoa matamko mazito ya kutoa vipigo vizito kwa wananchi( Mbeya). Vyombo vya habari kimyaaa. Kwao hiyo sio story.
Kama ingekuwa Kenya leo wanasheria nguli wangeongoza mijadala mizito kujadili kilichoamuliwa jana na mahakama dhidi ya kesi ya Tundu Lissu kupinga maamuzi ya Spika kumvua ubunge.
Habari za Konki Likwidi ndo zinapewa mjadala mzito mpaka bungeni cha ajabu hili eti linaonekana ni la kipuuzi tu. Hii ni hatari kwa afya ya akili ya wananchi wetu. Huenda ndio maisha tulioyachagua.