fdizzle
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 1,891
- 2,367
Haujapita muda mrefu tangu Tanzania itembelewe (kimya kimya) na mwanasoka maarufu duniani David Beckham.
Wakati huyo mchezaji alipotembelea Tanzania ingawa wengine wanasema ni Kenya yalitolewa maoni mbali mbali na wadau kuwa serikali ingefanya japo kujipendekeza ili angalau huyo jamaa aandike kuwa yupo Tanzania kwani itasaidia kuongeza watalii kwa kuwa huyo mchezaji ana mashabiki wengi duniani na pia anafahamika na wengi (hata wale wasio fuatilia mpira ukitaja hilo jina asilimia kubwa wanajua unamzungumzia mchezaji).
Baadhi waliponda kama kawaida yao maana hatufanani kimtazamo kuwa hakukuwa na haja ya kujipendekeza kwake.
Sasa kuna habari kuwa mchezaji mwingine maarufu duniani Wayne Rooney anatarajia kuitembelea Tanzania hivi karibuni.
Hizi ni fursa za kuongeza watalii kwa kuwatumia hawa wachezaji na hivyo kuongeza pato la taifa lakini kwa masikitiko makubwa wa husika hawalioni hili.
Nawaza tu, ingekuwa enzi za mzee wa msoga, hizi fursa zisingeachwa zipite hivi hivi.
Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app