Ingekutokea ungefanyaje?

Ingekutokea ungefanyaje?

Kiba

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2012
Posts
459
Reaction score
62
Habari wana jf. Hakika nina kisa kilichonitokea hadi sasa sijui lakufanya..

Nimeanza mapenzi na msichana tangu mwaka 2008 nikamsubiri hadi kamaliza shule .
Alipomaliza kidato cha nne bahati mbaya hakufaulu. Tukashauriana jinsi ya kufanya ili walau aendele kielimu .
Nikamtafutia chuo akaenda kumaliza chuo mwaka huu tukawa tumepanga kuishi pamoja mkoani Mwanza ninapofanyia kazi. Maskini binti huyu na kazi ya muda hadi matokeo ya chuo yatoke nikamtafutia na kipindi chote cha miaka miwili nilikua namjali sana hadi wazazi wangu wanamfahamu.

Imefika tarehe ambayo kaaga kwao anakuja Mwanza kaaga nyumbani vizuri na kwenda Mjini Arusha kwajili ya safari vizuri .mara gafla akiwa Arusha akawa apatikani kwa siku moja siku ya pili kaka mmoja kanipigia simu majira ya usiku na kuniambia je unamfahamu fulani?
Nikamjibu ndio ? Ni nani kwako ? Nikajibu vizuri ni mchumba wangu .
Kaniuliza una mda gani naye? Nikajibu miaka mitano? Akasema kweli kaka anastahili kuwa mchumba wako hila nami alikua na mahusiano nami kwa kipindi cha mwaka mmoja na hadi naongea nawe nimeachana naye kwa hasira baada ya kuniambia amekuja kuniaga anaenda kwa mchumba wake mjini mwanza ambaye ni wewe? Na nimelala naye siku hii ni ya pili ndio ananiambia.
Akaendelea ulipiga sm akazima leo ukapiga akakuambia yuko mjini na alikua kifuani kwangu.

Akaendelea ili kuakikisha mimi baada ya kukosana naye kutokana na safari nilimnyang'anya simu na ninayo hapa tena ina dakika ngoja nikupigie nayo? Akanipigia nayo kweli.
Wakati huo msichana ananipigia na sm ya dada yake aishie Arusha na kuniambia simu iko chaji?

Kitendo hicho kiliniuma sana hadi sasa nimemwambia aendelee kusubiri Arusha hadi nitakapopata Ushauri.

Naomba ushauri wako nifanyeje?
 
Sasa si ushukuru Mungu hata wameachana na huyo mtu wake ili na wewe upate muda wa kuwa nae.

Wewe unadhani wasingeachana ungeambulia kitu hapo?
 
Kiba, huyu binti wewe ulikuwa naye kwa miaka mitano, huyo mwenzako aliyekupigia simu alikuwa naye kwa mwaka mmoja! Ina maana akiwa na wewe, aliamua kutafuta mwingine? Inawezekana kuna tatizo la uaminifu hapa kama kweli huyo kaka aliyekupigia simu anasema ukweli.

Ila nakushauri mtafute huyo msichana, ukae naye na kuongea naye usikie kauli kutoka kwenye kinywa chake mwenyewe. M-bane kwa njia zozote zile unazozijua naamini itafikia pointi atakwabia ukweli. Isije kuwa huyo kijana kaamua kumharibia kwa makusudi baada ya kumkataa au kwa sababu yoyote ile.

Si busara sana kufanya maamuzi kwa kusikiliza maelezo ya upande mmoja. Ila kama utagundua kuwa mchumba wako huyo ni mwingi wa habari, ni vyema ujikalie pembeni kuepusha msongamano (refer 20%). Usije ukajikuta unainvest sehemu ambayo kismingi haina faida wala future na wewe.
 

we kama unampenda binti
mwache aje,kaa nae,ongea nae
huyo aliekupigia huna uhakika kama kweli au la
inaweza kua hila tu,kisa labda kakataliwa,ni vema umsikie na binti!!
 
kaka achana nae atakuja kukusumbua. Usiangalie gharama na ucje rudia tena kumsomesha mwanamke kwa lengo la kumuoa labda kama unamsaidia 2. Cku zote wanawake hawana shukran na hawajui kulpa fadhla.
 
Napata ushauri wenu vizuri wangwana.
 

we kama unampenda binti
mwache aje,kaa nae,ongea nae
huyo aliekupigia huna uhakika kama kweli au la
inaweza kua hila tu,kisa labda kakataliwa,ni vema umsikie na binti!!

Hawa vijana wa vibanda vya simu wahuni sana hawa! Yani kachukua simu ya mchumba wako akajidai kukupigia eti awachonganishe... Ali Kiba usikubali!!!
 
Last edited by a moderator:
Hawa vijana wa vibanda vya simu wahuni sana hawa! Yani kachukua simu ya mchumba wako akajidai kukupigia eti awachonganishe... Ali Kiba usikubali!!!
hahahaha, mnatabia mbaya nyie! mnataka kumpoza tu mwenzenu wakati manyoa yako nje kabisa! lol #UkionaManyoa ...
 
Hawa vijana wa vibanda vya simu wahuni sana hawa! Yani kachukua simu ya mchumba wako akajidai kukupigia eti awachonganishe... Ali Kiba usikubali!!!
mambo ya kwenye mitandao sio ya kuamini sana
kuna uongo mwingi,halafu Mentor kwani kakuambia
anaitwa ali kiba au kiba?
 
Last edited by a moderator:
hawa mabinti nao mmmmmh
inaonyesha moja kwa wakati mmoja inakuwa ngumu sana kwao.
 
Mwali, unajua kipendacho roho wewe!??????


Mwache bana...mimi nawajua watu wa vibanda vya simu...!!!!!!

#zaKuambiwa
Mi nilirithi kinyaa toka kwa mama na kiburi toka kwa baba.
Vitu kama hivi sivumilii, na sipotezi ma-time on investigation
 
Kuna haja ya kujua ukweli ya yote hayo na si kupitia kwenye simu,kwanza huyo mwanaume aliyekupigia simu huna uhakika kama ni kweli yote aliyokuambia ndiyo yaliyotokea,kwa kuwa uliweza kukaa nae miaka mitano basi haiwezi kukushinda siku moja yeye kuja huko na ukakaa nae na kujua mbivu na mbichi.
 
duh hiyo kali.......,
It hurts when someone plays with your feelings....,
ngoja aje talk to her even though the reality is seen

jaman girls na sie viruka njia
ukipata mtu anaekubeba haubebeki
mi watu kama hawa wananikeraga kweli
watu wanalilia nafasi kama hizo wengine wanazichezea
 
Jua likiwaka sana, akili ina_jam
Ntarudi jioni
 
Kwanza mkuu kwanini ulikuwa na uhusiano mtoto wa sekondari tena o level?
Alikuwa mdogo sana na inaonekana alikuwa hajakomaa kufanya maamuzi!


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kuna haja ya kujua ukweli ya yote hayo na si kupitia kwenye simu,kwanza huyo mwanaume aliyekupigia simu huna uhakika kama ni kweli yote aliyokuambia ndiyo yaliyotokea,kwa kuwa uliweza kukaa nae miaka mitano basi haiwezi kukushinda siku moja yeye kuja huko na ukakaa nae na kujua mbivu na mbichi.

inauma kama kweli mtu anakua na simu husika na alipomrejeshea nikamuuliza unamjua aliyekua na simu anang'ata ulimi na jamaa mwenyewe ni paparasi wa kituo cha radio 5 Arusha .je kama si kweli reporter huyo anaweza kuwa kwenye kibanda cha simu?
 
duh hiyo kali.......,
It hurts when someone plays with your feelings....,
ngoja aje talk to her even though the reality is seen

jaman girls na sie viruka njia
ukipata mtu anaekubeba haubebeki
mi watu kama hawa wananikeraga kweli
watu wanalilia nafasi kama hizo wengine wanazichezea
ebu waambie bana
 
Back
Top Bottom