Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,235
- 4,382
Historia imeandikwa, Revocatus Chiponda (Baba Levo aka Chawa Pro Max), amezipiga bao husda na hila za Maalhaji wa Ujiji!
Kwanini namkubali Baba Levo? au ni kwanini anakubalika na wanakigoma? (Ukimuangalia kwa miwani ya uchawa huwezi kuona hizi sifa)
1. Pragmatic (ni mwalisia wa mandeleo)
Alipokuwa kijiji kimoja cha huko Ujiji kwa wajumbe, alipiga punch moja kali sana, nikajisemea, "Huyu ndo mbunge anayeendana na Vision 2050". Aliulizwa swali kwamba: Atakifanyia nini hicho kijiji ambacho pwani yake imepakana na ziwa Tanganyika?
Baba Levo alijibu kwamba: Yeye ana connection kubwa na watu wenye rasilimali kama GSM na Lukuga (Diamond Platnumz), kwahiyo atawashawishi wapeleke uwekezaji kwenye pwani ya ziwa Tanganyika inayopakana na kijiji hicho, na hoteli hiyo itavutia watalii na wageni, hivyo kutengeneza ajira n.k (hii ni hoja nzito na inachora mstari wa utofauti na wabunge wasiokuwa na mguso na utatuzi wenye uhalisia na matatizo ya wananchi; wabunge wengi huishia kusema serikali itafanya hiki na kile na kusahau kutumia nguvu yao ya mawakala wa mabadiliko kwa kushirikisha sekta binafsi na kutatua kero za wananchi). Kwakuwa tayari ana mindset ya kibepari mamboleo, huyu atafanya jambo, na ana historia ya kufanya hivo.
2. Anajiamini na mpambanaji
Tusemezane pembeni tu: hivi ni wangapi kati yetu wangaliweza kuzishinda husda na hila za Maalhaji wa Ujiji? Hapa amenifundisha kitu, nikipata wasaa nitakuja kumng'ata sikio aniambie anasali dhehebu gani, na ikiwa anasali Biblia na Novena ipi!
3. Ni mwanamapinduzi na sio mnafiki
Hii ngonjera ya ACT kuwa project ya CCM, Baba Levo alishatusanua kabla hata ya hii chombeza ya Polepole, kwa wafuatiliaji. Baba Levo alitupa ahadi ya kumuumbua Kijicho Upembe, ya ni kwanini sio mpinzani. Na aliyasema wazi haya maneno na hadharani.
Kwahiyo baada ya leo, tutegemee muda wowote, kambi ya Baba Levo ikianza kuinua zile silaha zake nzito nzito, uelekeo wa ACT Wazalendo, tayari kuanza kupeleka moto na kuwacharaza mboko vilivyo kama Benjamini Netanyahu. Kwakuwa Kijicho Upembe aliyataka basi atayapata!
Kwa hizo sifa hapo juu, sioni kabisa kama Kijicho Upembe ana uthubutu wa kupambana na Baba Levo; na haitonishangaza ikiwa Kijicho Upembe atakimbia pambano. Kwasababu hata ikiwa Kijicho Upembe ataamua kushiriki mpambano wa uchafuzi, kura za maoni tayari zinaonesha kwamba Baba Levo anauwezekano wa kushinda kwa 75% na hili nilishalitabiri mapema sana mwezi wa saba mwanzoni << GE2025 - Uchafuzi wa Ubunge Kigoma Mjini: Kijicho Upembe vs Chawa Pro Max; Chawa anashambulia kama Netanyahu, anaongoza kura za maoni >>
Moto utawaka ubembeni!
MC