Infosys IPS (T) LTD wakanusha kuhusika na LUGUMI katika kashfa ya ubadhirifu

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Kampuni ya INFOSYS IPS (T) LTD imekanusha taarifa zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii kwamba kampuni hiyo inahusika na inashirikirikiana na Lugumi Enterprises katika kashfa ya ubadhirifu.

Katika habari zilizosambaaa inasemekana kwamba kampuni ya Infosys ilipokea mabilioni ya shilingi kutoka katika kampuni ya Lugumi, jambo ambalo wao wanadai si la kweli na ni la kupuuzwa na umma.

'Hatujawahi kufanya biashara na kampuni ya Lugumi Enterprises' Amesisitiza Bwana Sweki Donald, Naibu Meneja Mkuu Infosys IPS (T) LTD.

Video:
 
Haya sasa ukweli umewekwa wazi kumbe ni juhudi za kumpiga vita Waziri Kitwanga na kutaka kuichafua serikali ya Magufuli.

Wapiga dili tafuteni kiki nyingine ukweli ndio huu.
 
Mambo yazidi kunogaaa, lete utamuu babaaa
Mkuu mambo yamenoga kweli kweli kuna watu hawana hoja ya kisiasa na Waziri Kitwanga kabana chanel zao za upigaji. Sasa wameamua kumzushia vitu ata ukiangalia haviingii akilini ufisadi wa Lugumi ila anaeliliwa kuwajibishwa Kitwanga yani ni siasa chafu tupu za wapiga dili.

Ishu ya Stanbic na hati fungani wala hatukuwasikia kupiga kelele wanafiki wakubwa.
 
Kitaeleweka tu, mmefanya chini ya wamarekani ambao nao walikua wakifanya kazi chini ya Lugumi, bado kidogo tutapata ukweli
 
Haha utokaji wa hii taarifa na contribution za mwanzo umeniacha nikicheka.
Anyway mimi pia naona chuki tu binafsi na wivu wa baadhi ya watu. Kitwanga ni mtu safi kabisa.
 
Haha utokaji wa hii taarifa na contribution za mwanzo umeniacha nikicheka.
Anyway mimi pia naona chuki tu binafsi na wivu wa baadhi ya watu. Kitwanga ni mtu safi kabisa.
Mkuu wakati Magufuli na serikali yake wakipambana kuleta maendeleo ya nchi yetu kwa juhudi kubwa kuna watu wanapambana kuona hafanikishi hilo kwa manufaa ya vyama vyao na dili zao. Kelele nyingi ila ndio mafisadi wakubwa tungewaachia funguo ya hazina tungejuta sisi na vizazi vyote.
 
Mkuu wakati Magufuli na serikali yake wakipambana kuleta maendeleo ya nchi yetu kwa juhudi kubwa kuna watu wanapambana kuona hafanikishi hilo kwa manufaa ya vyama vyao na dili zao. Kelele nyingi ila ndio mafisadi wakubwa tungewaachia funguo ya hazina tungejuta sisi na vizazi vyote.
Kweli kbs. Ila kwa hili la kitwanga naona vita anapigwa na watu wenye wivu waliomo humohumo CCM. Sidhani kama ni wapinzani. Namfahamu kitwanga vzr. Haya mambo anasingiziwa tu. Ni wivu na chuki binafsi
 
Huu Uzi umeanzishwa na Kitwanga ili ahadae watanzania.chief!hana pakutokea kwenye hili sakata la Lugumi!
 
Kweli kbs. Ila kwa hili la kitwanga naona vita anapigwa na watu wenye wivu waliomo humohumo ccm. Sidhani kama ni wapinzani. Namfahamu kitwanga vzr. Haya mambo anasingiziwa tu. Ni wivu na chuki binafsi
Ndio maana nimesema vyama vyao na dili zao yani wote wote hii ishu imewaunganisha.
 
Hao ni vibaka kama vibaka wengine ukishaona wameibuka leo wadhajianda au wamesafisha ushahidi kitambo, ila subiri tuone.
 
Sasa kimeanza kueleweka, na Lugumi is on the run.
Tujitayarishe kwa suprises zaidi.
Wazee wa unga inaelekea wamebanwa!
 
Kitwanga ni kweli amewabana wazee wa dili chafu.
Hii kashfa ya Lugumi inanichekesha sana, eti Lugumi kakimbia, kakimbilia wapi? Eti haijulikani......
Swali langu, is Lugumi Invisible person?
Kakamatwa gaidi àliyekimbia (mwenye kofia ya pama) kwenye tukio la ulipuzi wa wamja wa ndege Ubelgiji, huyu Lugumi asiyejua hata kusoma atajifichaje asikamatike?
 
Huu Uzi umeanzishwa na kitwanga ili ahadae watanzania.chief!hana pakutokea kwenye hili sakata la lugumi!
Haijalishi nani ni muanzulishi wa uzi, ila kilichomo ni maelezo yaliyonyooka tu, next step kwa wanahabari ni kuitafuta Biometrica na kupata ufafanuzi wao juu ya hii issue, maana maistream ya habari tz haitaki kutafuta ukweli, wao ni kupakua habari jamiiforums na kuziweka kwenye magazeti yao tu.
 
BIO METRICA.jpg

INFOSYS.jpg
 
Back
Top Bottom