GE2025 INEC, NIDA wamkana Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kama kuna mtu kamuelewa polepole anisaidie kueleweshwa vipi kura zinapatikana kwa kuunganisha hiyo mifumo wakati kura zinapigwa kwa makaratasi.
Kura za Urais ubunge na udiwani huunganishwa kwa nchi nzima. Lakini mifumo ndiyo husaidia kujua mambo ya idadi ya wapiga kura na Demografia Yao.

Mbona Lowassa alipogombea watu wake waliokuwa wanamsaidia kuratibu uhesabuji wa kura walikamatwa na kuambiwa kuwa waliingilia mfumo wa Tume?
 
Hawa wanaona Watanzania bado ni majuha kama zamani. Siku hizi watu wanaelewa kila kitu. Pia wajue tu hatukuhitaji Polepole aongee ndio tujue michezo hii. Tulishashtuka kitambo.. Mama yao aendelee tu kutulazimishia uongozi, ila ajue hakuna marefu yasiyo na ncha.. tupo hapa.
 
Kumbe INEC na NIDA wakuu hawakulala,

Walifuatilia press ya Pole Pole usiku ule?

Sasa kwanini huwa wanazima mitandao ikiwa ni wafuatiliaji wazuri wa press zake?

Nchi ngumu hii!
 
Kwenye majumuisho ya kura kura feki na vituo feki ndipo zinapo ingizwa kutumia huo mfumo wao
 
Subirini siku mkiitwa mbele ya sheria na kufanyiwa cross examination based on facts ndio mtajua hamjui, na mjue kusema tulikuwa tunafuata maelekezo haitawasaidia na sio defense under the law
 
Hupati uteuzi acha kujisumbua wewe hakuna mwenye Akili Timamu atakaa akuelewe licha ya kujifaragua kuandika mandishi mengi yasiyo na point hata moja, ni wajinga pekee watakaa kukusikiliza
 
Ni muda wa polepole kuja kudadavua vizuri maana bado wameweka pamba masikioni
ccm wanahaha kujibu jibu chawa wanakomaa kusaka Uteuzi kupitia humo humo lakini wenye Akili Timamu wapo na polepole hawatetereki
 
Sasa kwanini tumeccm inataka mawakala wasipewe matokeo na cm wasiende nazo vituoni? Huo sio uchaguzi
Tanzania hakuna uchaguzi kuna Maigizo tu kwani ccm walishapiga kura mapema wanasubiria kutangazwa tu
 
Huyo Mwambegele kachaguliwa na nani kukaa hapo? Kifupi hana jipya.

Juzi nilihudhuria mkutano na Tume huru na Waandishi wa Habari aliambiwa ukweli kuwa Tume haikubaliwi na haitakiwi na Wananchi...huyu Jaji aliwaka utadhani mwehu.
TUME HURU YA UCHAGUZI ❎❎❎

TUME CHAFU YA UCHAGUZI ✅✅✅
 
Wewe ndiyo una IQ ndogo zaidi kwa kuamini kukariri Maovu ujinga wote wa ccm na kukataa ccm isikosolewe, hakuna kitu kibaya kama kujiona upo sawa kwa kila kitu na hupaswi ukosolewe milele
 
Ukweli umejulikans hata watapetape vipi hakuna wa kuwaamini labda wale mazezeta wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…