tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewaonya makarani watakaotoa taarifa za uchaguzi na kuwataka kusimamia viapo vya utunzaji wa siri katika kipindi chote cha uchaguzi.
Onyo hilo limetolewa na Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Njombe Mjini, Samson Meda wakati wa mafunzo kwa makarani waongozaji wa vituo vya kupigia kura katika jimbo hilo.
Soma pia: Asina Omar: Watendaji wa uchaguzi mkaishi viapo vyenu
"Utendaji wenu na uwajibikaji wenu katika kipindi chote cha utumishi wenu kwa Tume mtawajibika kwa tume huru ya taifa ya uchaguzi na sio mamlaka nyingine yoyote, isipokuwa kama jambo hilo litahitajika kwa mujibu wa sheria nyingine ya nchi" amesema Samson Meda
Aidha, Meda amesema katika viapo vya kujiondoa uanachama wa Chama cha Siasa kwa makarani ambao ni wanasiasa, hakuwaondoi moja kwa moja katika vyama vyao isipokuwa ni kwa kipindi kifupi cha utekelezaji wa majukumu ya tume kwa kuwa, kuwa Mwanachama wa Chama chochote cha siasa sio dhambi bali ni haki ya kikatiba.
Makarani 366 wa jimbo la Njombe mjini wameapishwa na kupewa Mafunzo kwa ajili ya kwenda kusimamizi shughuli za uchaguzi katika vituo na maeneo watakayopangiwa na tume.