Individual Retirement Arrangements (IRA) in Tanzania

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Pengine umefika wakati mamlaka husika zikaruhusu utaratibu wa kuwa na Individual Retirement Arrangements (IRA) hapa Tanzania.

IRA hizi ziwe tax-deductible, na ikiwezekana tax-exempt.

Faida zake ni nyingi. Kwa mfano:

1. Kujenga utamaduni wa uwajibikaji binafsi, hata kwenye mafao ya kustaafu, ambapo serikali haitasumbuka na wastaafu.
2. Kuimarisha ukwasi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja kama vile
UTT, na hivyo kuwapo kwa fedha nyingi zinazoweza kuikopesha serikali kupitia hatifungani na dhamana za serikali, ambazo hazina masharti magumu kama ya baadhi ya mikopo / misaada toka nje.
3. Kupata mitaji kwa miradi mikubwa ya binafsi na ya kitaifa ya maendeleo kupitia hatifungani za binafsi.

Nawasilisha.
Mlenge
 
Back
Top Bottom