Indian toilets

Wazee wa Pori kwa Pori sisi ni Jembe au sabuni either mtoni au Porini
 
Vyoo vya kukaa kwenye public toilet nidisaster...


Mkuu umenikumbusha mwaka 1986 tukiwa tunakaa Upanga, kuna jirani yetu aliwaleta wazazi wake toka kijijini mbaya zaidi nadhani hakuwapa orientation ya namna ya kutumia hicho choo, kilichotokea ni kwamba walibana siku ya kwanza na haja ndogo walitumia bafu, siku ya tatu au ya nne kama sikosei, waliamua kuondoka, na hapo hawakusema nini kimewaondoa mpaka walipofika kwao ndipo wakasema hawawezi kuishi sehemu yenye huduma ya haja ndogo pekee (bafu) kumbe choo ya kukaa walikuwa hawajawahi kuiona wala kuitumia.
 
View attachment 846246


Nilikiona hiki dukani, nilikumbuka vile vyoo vya ceramic tulivyotumia boarding schools. Indian toilet wengi hupenda kukiweka kama family toilet au communal toilet. Ukikijenga zingatia aging issues.

Kwa experience yangu wazee wengi wa 65+ hawawezi kuchuchumaa wakienda haja. Technology ilivvyoendelea siku hizi hata cancer ikiwahiwa inapona na HIV si tatizo tena kama unabuia njugu kila siku.

Maana yake aging population huko tuendako itakuwa kubwa. Sasa uwalete wazee kutoka kijijini kwa matibabu mjini. Kuwawekea Indian toilet ni kuwatesa.
Nimekuelewa sana!
Niliwahi kubomoa moja ya choo na kuweka ya kukaa Kwa ajili ya wazee wangu au yeyote mwenye issues za kuchuchumaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kwamba, ukikisema vibaya hiki, kuna watu wanasema kwamba vyoo vya kukaa haviko natural katika kusababisha mtu ajisafishe mpaka mwisho, kwa mana kwamba, choo cha kuchuchumaa, kinasaidia mtu kujikunja vizuri na kumaliza haja vizuri zaidi kuliko cha kukaa.

Na hapo hapo umeibua suala la wazee wanaoweza kuwa na matatizo ya kuchuchumaa.

Sasa hapo kinatakiwa choo kinachofanya anatomy ikae kama umechuchumaa, wakati umekaa, kitakuwa nina address mambo ya angle ya kusaidia kujisafisha vizuri kama choo cha kuchuchumaa, halafu kinatoa support kwa wanaohitaji support kama wazee.

Choo cha aina hiyo sijawahi kukiona bado. Mtu atakayeweza kukitengeneza anaweza kutengeneza a hit toilet.

Especially kama ataweza kutengeneza na mikono ya kushikia mbele ili mtu uweze kunya halafu unajisikia kama unaendesha pikipiki moja babu kubwa!!!

Yani unamaliza haja zako halafu umeshika handles una engage fantasies zako, kama unataka kurusha ndege unarusha, kama unataka kuendesha pikipiki unaendesha, kama unataka kutumia handles kuweka kitabu usome unasoma.

Hicho hata mimi nitakitafuta.


Hii idea yako kama mchina akiipata hachelewi kutengeneza!!!
 
Vyoo vya kuchuchumaa vinafaa kwa watu chini ya 50 years.
Umri ukizidi hapo vyoo vya kukaa vinafaa zaidi kwa usalama wa mtumiaji. Kwa umri mkubwa, pressure inaweza kupanda na kusababisha maafa chooni kwa mtumiaji kama atachuchumaa.

Cha muhimu hapa sio kukwepa matumizi ya aina fulani ya choo. Badala yake ni suala zima la usafi kwa wote.
Mtumiaji au msaidizi wake ahakikishe anakiacha choo kikiwa kisafi kwa matumizi ya mtu mwingine.
 
Mkuu umenikumbusha mwaka 1986 tukiwa tunakaa Upanga, kuna jirani yetu aliwaleta wazazi wake toka kijijini mbaya zaidi nadhani hakuwapa orientation ya namna ya kutumia hicho choo, kilichotokea ni kwamba walibana siku ya kwanza na haja ndogo walitumia bafu, siku ya tatu au ya nne kama sikosei, waliamua kuondoka, na hapo hawakusema nini kimewaondoa mpaka walipofika kwao ndipo wakasema hawawezi kuishi sehemu yenye huduma ya haja ndogo pekee (bafu) kumbe choo ya kuchuchuma walikuwa hawajawahi kuiona wala kuitumia.
Kuna dada mmoja wa Kisomali huko huko Upanga sasa anaishi Holland. Alimpeleka mtoto wa miaka mitano nyumbani. Mtoto ameshindwa kabisa kutumia Indian toilet. Mama yake alinunua potty. Alilitumia mpaka likizo inakwisha.
Walipoondoka bibi alinunua Choo cha kukaa. Alisema nisipoweka hiki hawarudi tena hawa.

Kuhusu wazee, siku ya kwanza wakija unaenda nao taratibu. Na unawaambia wakuulize chochote kunachowatatiza.
 
Vyoo vya kuchuchumaa vinafaa kwa watu chini ya 50 years.
Umri ukizidi hapo vyoo vya kukaa vinafaa zaidi kwa usalama wa mtumiaji. Kwa umri mkubwa, pressure inaweza kupanda na kusababisha maafa chooni kwa mtumiaji kama atachuchumaa.

Cha muhimu hapa sio kukwepa matumizi ya aina fulani ya choo. Badala yake ni suala zima la usafi kwa wote.
Mtumiaji au msaidizi wake ahakikishe anakiacha choo kikiwa kisafi kwa matumizi ya mtu mwingine.
Kuna nyumba niliwahi kupanga back in the days. Land Lady alikuwa mama wa ki Nigeria na tuliishi nae. Yule mama alikuwa msafi sana. Sasa karatasi za maelezo ya kusafisha ukimaliza kutumia zilikuwa chooni na jikoni.

Rafiki zangu wakija kunitembelea wanakuta maelezo. Walikuwa wananicheka sana. Lakini kodi ilikuwa nafuu kwa hali yangu ya wakati huo.
 

Hii idea yako kama mchina akiipata hachelewi kutengeneza!!!
Ujue hizi ideas ambazo zinaweza kuonekana za kuchekeshachekesha zinawatoa watu halafu unabaki unashangaa mwenyewe.

Kuna kipindi cha nyuma nilikuwa nimekaa na jamaa mmoja anaitwa Alpha, watoto wa Obay watakuwa wanamjua, jamaa mtambo mtambo fresh hivi, mtu varuvaru chizi fresh.

Basi Alpha akiwa anakunywa haishi maneno.

Siku moja tunakunya, Alpha akasema hapa Dar es slam kuna bonge la deal, watu wanalilazia damu tu.

Nikamuuliza Alpha, kila siku unakuja na ma deal mapya, unataka kutupa deal gani sasa?

Akasema hapa Dar ukianzisha vyoo vya kulipa utapata hela nzuri, halafu utasaidia watu kumaliza haja zao.

Hapo kipindi cha nmyuma kabisa, Dar haina vyoo vya kulipia.

Basi watu tukacheka, tukasema huyu Alpha tu na maneno yake anafurahisha baraza.

Miaka michache baadaye, jiji likaichukua idea ile ile, vile vile alivyoisema Alpha, vyoo vya kulipia vikaanzishwa.

Kuna siku nimekuja likizo Dar, nimetoka Zanzibar, natembea Mnazi Mmoja, nikaingia kwenye moja ya vyoo hivi.

Nikakumbuka yale maneno ya chizi fresh Alpha yamekuja kuwa kweli, nikasema mara nyingine huwa tunacheka ideas nzuri kama utani, watu wanafanyia kweli.
 
Public toilet za bongo ukiweka vyoo vy kukalia aisee kuna mengi utakuta huko either mzigo umejaa mpaka unamwagikia au hicho cha kukalia hakipo!!
Vipi ila sehemu yenye utulivu kidogo kwenye mahotel makubwa makubwa nabhata kule iluku mbona vipo
 
Back
Top Bottom