Indian School Dar es Salaam

Ni ubaguzi Wa rangi labda msajiri ni Wa aina ya kihindi. Kwani nikianzisha shule nikaomba nisajiriwe WASUKUMA SCHOOL AU WACHAGA SCHOOL AU WAPEMBA SCHOOL AU WASAFA SCHOOL nitasajiriwa? Najua sitopata jibu rasmi!
 
Unasumbuliwa na ugonjwa uitwao EDS- "Exposure Deficiency Syndrome".
Tembea uone, zipo French Schools, Germany Schools maranyingi zimetengenezwa kwaajili ya ma TX ili watotowao wasichanganye mitaala na tamaduni
 
Duppy hao wahindi gari hiyo hapo ni wahindi Wa hapahapa watanzania siyo experts wala nani
 
Nilifikiri waafrika ni weusi naturally na hawa wageni waliohamia watabeba utaifa wa nchi husika. Mfano wamisiri, Libya, Morocco, Algeria, nk turawaita waarabu wa Misri, Libya, Morocco nk. Mfano wa kitaifa ni kwamba Yussuf Manji ni mtanzania ila sio muafrika. Sawa na Mohamedi Dewji na Bakhresa
 
Unapaswa uwe umeishi miaka mingapi au vizazi vingapi ili uweze kuitwa mu-AFRIKA au m-MAREKANI?
 
Sio kweli.Ukizaliwa mahali sheria ya kuzaliwa inakutambua kuwa wewe ni raia wa hapo hadi uje ukana uraia mwenyewe.Wahindi na waarabu ni waafrika sababu walizaliwa Africa na hawajaukana uraia wa Africa.Makaburu walipiga kelele sana kuhusu hili wamegoma kata kata popote waendapo wao hujitambulisha kama waafrika,Bara la africa lina waafrika weusi,waarabu kama hao wa misri,tunisia,moroco.libya nk na hawa wa Tanzania waarabu,pia Africa ina wahindi kama wa mauritius .madagascar na hawa wahindi wetu wa tanzania pia Africa ina wareno wako mozambique,angola na hata wengine wako mtwara,Africa ina wachina mfano zanzibar wapo,africa ina wagiriki na ina wazungu wengi mfano Africa kusini.

kUHUSU HIZO INDIAN schools hizo hazina tofauti na Christian schools,Muslim schools ambako mtaala wake pamoja na masomo mengine huwa na masomo ya dini ya kiislamu au kikiristo ukitaka kwenda shule hizo uwe tayari kuyasoma na kuishi kikikrsto au kiislamu wapokea mtu yeyote. Ndivyo ilivyo kwa french schools nk Hizo indian schools ni shule za kimataifa ambazo pamoja na masomo mengine ujiandae kusoma dini ya kihindu,kusoma kihindi na maandishi yao ya kihindi na kuishi kwa mila za kihindu .
 
Ishu hapo si wabaguzi, hapo ni ishu ya uminority kwasasa wao kujicanganya sana na sisi ndo mwazo wao wa kuisha kabisa
 
Ulichowaza ni kweli, lakini pia zipo shule zenye majina yenye uelekeo wa ubaguzi wa kiafrika kama hii iliyopo hapa Tabata Chang'ombe, na mbaya zaidi mafundisho yake ni ya uislamu wenye itikadi ....
 
Bado nina walakini. Ataeitwa muarabu ila mtanzania. Kuna kipindi tulipata miss Tanzania mhindi ikaleta maneno kdg kuwa araonekana muhindi na hatawakilisha bchi vyema, awekwe muafrika. Kadhia hii iloshamkuta Salim Mohamed Salim katika michakati ya siasa kama sikosei. Muafrika hana nywele zilizoangukia mgongoni kama wazungu. Ataitwa mzungu mtanzania ila sio mzungu muafrika. Au mchina mtanzania na sio mchina muafrika. Haiwezekani mchina kuwa muafrika ila inafaa kuwa mchina mtanzania, mkenya, mnigeria nk. Sijui unaelewa nnschojaribu kueleza
 
Ubaguzi unaanza mwenyewe kwa kujibagua. Hilo jina linarahisisha Huduma na upatikanaji wao. Shule zipo za mataifa mengi tu, kama hiyo inamfaa mhindi anaekaa nchini miaka michache na kurudi kwao. Itasaidia watoto wasipate shida kubadili mtaala pia.

Kama ilivyo tuna Cambridge system, acha nao wawe na ya kwao.
 
Sio kweli Mwafrika hatambuliwi kwa rangi hilo kwanza ulijue.Rangi za watu zilibuniwa na waongo wakubwa wenye akili nyingi waliobobea kwa uongo wa kimataifa.Nikupe mfano rangi nyeupe watu wamejifunza toka wako chekechea kuwa rangi nyeupe ikoje.Rangi nyeupe ni ile nyeupe kama karatasi nyeupe.Hao wahuni waongo wa kimataifa wadanganya dunia wakaja na theory kuwa duniani kuna watu weupe!!!!! Hao watu weupe ni wazungu,Hivi mtu hata uwe na akili ndogo kiasi gani unaamini mzungu ni mweupe? Anafanana na rangi ya karatasi nyeupe au shuka nyeupe? Lakini wameilaghai dunia hai wazungu wenyewe wanaamini kuwa wao weupe ilivyo mijinga.Pia wakaaminisha watu uwa kuna watu weusi.Mkaa ni mweusi angalia ngozi yako mwenyewe uone kama una rangi hiyo ucheki mkono wako hapo ulipo una rangi gani hauna rangi nyeusi.Jitizame mwenyewe.Hivyo waafrika sio watu weusi .Binadamu ni binadamu full stop hakuna mweusi wala mweupe ( no black or white)

Ukienda kihistoria mfano Afrika ya kusini kasome vitabu vya historia.Makaburu walifika afrika kusini kabla ya waswahili kuingia pale.Africa kusini ukisoma vitabu vya historia hata vilivyoandikwa na waswahili ,mswahili alimvamia kaburu kwenye eneo lake alilofika miaka mingi.Mswahili alimkuta kaburu pale.Waafrica wengi nchi tulizopo tulihamia hazikuwa zetu soma historia ya kabila lako utagundua asili yake sio tanzania,Wataalamu wa historia wanasema kabila linaloweza kusema Tanzania ni nchi yao na walivamiwa ni wahadzabe na wasandawe na wairaqw ambao hadi leo wanaishi maisha yale ya porini,Hao ndio wakazi asili wa Tanzania wengine wote wahamiaji wengi walitokea ethiopia,Uganda,kenya,kongo,zambia,malawi, Burundi,rwanda, sudan,Afrika kusini kama wangoni nk Hivyo kama ambavyo waarabu,wahindi nk ni wahamiaji tanzania vivyo hivyo makabila yote.Tanzania ni nchi ya wahamiaji kama ilivyo marekani ndio maana ina mabila mengi mno kuliko nchi yoyote duniani.Tanzania ina makabila zaidi ya mia na ishirini hakuna nchi duniani iko hivyo.Ndio maana hata mtu akitaka kuleta mapinduzi kupindua serikali hawezi sababu kila kabila liko kivyake mila zake na desturi zake na mambo yake na core values zake tunaunganishwa na lugha ya kiswahili tu the rest kila mtu kivyake kwenu kama mna mihemuko ya kisiasa kwetu hatuna,kwenu kama unategemea serikali kwetu mwiko hata kula kwa jirani heri ufe njaa kuliko kutegemea yeyote nk
 
Umeufunga mjadala huu, maelezo sahihi kabisa.
 
Unaeleweka lakini sivyo Ukweli ulivyo, Afrika ni bara, waafrika ni wakazi tu wa hilo bara, uafrika si weusi wa ngozi bali ukazi wa hili bara. Hivyo, wamoroko, Libya nk wote ni waafrika.
 
Jamani hivi wapi pana ubaguzu hapo na islamic school ni ubaguzi na Catholic School ni ubaguzi pamoja na shule mbalimbali zenye mlengo fulani.mbona mnatafuta mtu wa kumlaumu dhidi ya shida na matatizo mnayoyapitia
 
Kuna shule inaitwa Senge, hope ipo Singida. Kwani wanaosoma pale ni wa...?

Kwa nini serikali iliisajili? Achana na mawazo finyu, hata sisi tukianzisha Tanzanian school sio issue unless u-report violations zao!
 
Umaskini ukiuruhusu uingie mpaka kwenye akili una shida sana.
Nyamgulu usije wewe Ukawa. Muhindi, wahindi wanajibagua wenyewe na kuna hata baadhi ya wasomi wenye asili ya kihindi wanaliongelea hili jambo
 
Mzungu sio Mbaguzi.

Mwafrika ana ubaguzi zaidi kuliko mzungu.
Uzuri unashinda jamii forum tu

Sie tunaoshinda mitandao mikubwa kama reddit ,na wide coverage tunaona upuuzi na ufedhuli wao Kwa blacks tena Kwa Wa-Africa

Mpaka inafika hatua mtu unaona haya ,aibu kuendelea kusoma comments na hata nguvu ya kutype na kuchangia kutetea inaisha Kwa maneno Yao makali na hapo wapo nyuma ya keyboard vuta picha live
 
Ni ubaguzi Wa rangi labda msajiri ni Wa aina ya kihindi. Kwani nikianzisha shule nikaomba nisajiriwe WASUKUMA SCHOOL AU WACHAGA SCHOOL AU WAPEMBA SCHOOL AU WASAFA SCHOOL nitasajiriwa? Najua sitopata jibu rasmi!
Una walimu wenye vyeti mfano diploma au digriii za education in chaga,sukuma,pemba au safwa language ambao wamesomea vyuo accredited vinavyofundisha lughavl hizo? na wana teaching license? Kama unao nenda kaombe usajili hata kesho utapewa
 
Hebu tupe scenario kadhaa zinazothibitisha ubaguzi wa wazungu kwa waafrika kwa sikuhizi za sasa na si zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…