India yatupiga jeki kusaidia Kilimo Kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

India yatupiga jeki kusaidia Kilimo Kwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babu M, Jan 15, 2011.

 1. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Prof. Jumanne Maghembe akiwa na Balozi wa India nchini Mh. Kocheril Velayudhan Bhagirath


  Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amefanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Bwana Kocheril Velayudhan Bhagirath na kumueleza kuwa nchi yake imeamua kuisaidia Tanzania fedha, kiasi cha dola 92,000 za Kimarekani ambazo zitaelekezwa kwenye miradi ya Kilimo katika kutekeleza azma ya KILIMO KWANZA.


  Balozi huyo wa India nchini aliwasilisha nakala ya barua iliyotoka kwa Waziri Mkuu wa India kwa Waziri Maghembe na kumueleza kuwa barua hiyo pia amemfikishia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda kumfahamisha kuhusu msaada huo wa fedha.


  Aidha, Balozi Bhagirath alimweleza Waziri Maghembe kuwa India imeifanya Tanzania kuwa nchi ya pili kwa kuipatia udhamini wa wanafunzi wa Elimu ya Juu kwenda kusoma nchini humo na kwa mwaka wa masomo wa 2010/2011 jumla yake imefikia wanafunzi 196 nyuma ya Afghanistan.


  Balozi Bhagirath aliongeza kuwa nchi yake ipo mbioni kuanzisha kituo kikubwa cha kuzalisha mbegu za mazao ya nafaka ambayo ni mpunga na mahindi chini ya Mpango wa Export Processing Zones (EPZ) na kwamba eneo limeshapatikana huko Bagamoyo mkoani Pwani.


  Waziri Maghembe alimshukuru Balozi Bhagirath kwa niaba ya India na kumuakikishia kuwa Tanzania ipo mstari wa mbele katika kushirikiana na India katika maeneo yote yanayolenga kukuza na kuendeleza kilimo.


  Chanzo: Michuzi


  Mtazamo: Tunatia huruma...Kila kitu ni lazima tupokee...Mambo mengine yako ndani ya uwezo wetu.
   
 2. l

  limited JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hiviiiiiiiiii kilimo kwanza ndio nini? tunapoke 92000 usd tunompa mtu mara mia(94000000 usd) yake akale na mkewe. mahesabu mengine bwana
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Dola 92,000 tu? umekosea tarakimu?
   
Loading...