Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,279
Wanakijiji wenye hasira leo wameyachoma moto magari ya jeshi baada ya wanajeshi kuwauwa watu kadhaa waliodhaniwa kuwa wanamgambo katika jimbo la kaskazini mashariki mwa India.
Kiongozi wa jimbo hilo la Nagaland Neiphiu Rio amelaani kwa matamshi makali mkasa huo aliosema haukutarajiwa na kuamuru kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji hayo.
Afisa mmoja wa jeshi amesema wanajeshi walililenga kwa risasi lori moja na kusababisha vifo vya watu 6 baada ya kupokea taarifa za intelejinsia kwamba wanamgambo wa vuguvugu la waasi wapo katika eneo hilo.
Kufuatia vifo hivyo wanakikiji wenye hasira walivamia na kuyachoma moto magarii mawili ya jeshi na katika rapsha hiyo wanajeshi walifyetua pia risasi na kuwawauwa watu wengine 9. Jeshi la India limesema limefadhaishwa na kisa hicho na kuahidi uchunguzi wa kina wa mkasa huo