India: Wananchi wachoma Magari ya Jeshi baada ya wenzao kuuawa kimakosa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,266
07bfaf18a0b0383c8fa3a4279bf7f9c2


Wanakijiji wenye hasira leo wameyachoma moto magari ya jeshi baada ya wanajeshi kuwauwa watu kadhaa waliodhaniwa kuwa wanamgambo katika jimbo la kaskazini mashariki mwa India.

Kiongozi wa jimbo hilo la Nagaland Neiphiu Rio amelaani kwa matamshi makali mkasa huo aliosema haukutarajiwa na kuamuru kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji hayo.

Afisa mmoja wa jeshi amesema wanajeshi walililenga kwa risasi lori moja na kusababisha vifo vya watu 6 baada ya kupokea taarifa za intelejinsia kwamba wanamgambo wa vuguvugu la waasi wapo katika eneo hilo.

Kufuatia vifo hivyo wanakikiji wenye hasira walivamia na kuyachoma moto magarii mawili ya jeshi na katika rapsha hiyo wanajeshi walifyetua pia risasi na kuwawauwa watu wengine 9. Jeshi la India limesema limefadhaishwa na kisa hicho na kuahidi uchunguzi wa kina wa mkasa huo
 
Hao ndio wananchi sasa, ambapo dhuruma ikifanyika hawaangalii nani kaifanya!!lakini ile nchi nyingine, kila kitu ni kumuachia mungu tu, mfano kwa sasa mgambo wa jiji wanavyo tamba mjini, juu ya wamachinga, imefikia supu zinauziwa kwenye chupa za chai!!
 
Back
Top Bottom