India kukumbwa na kimbunga fani

India kukumbwa na kimbunga fani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mamia kwa maelfu ya watu wamehamishwa kwenye pwani ya mashariki mwa India wakati kimbunga kikali kikivuma kuelekea Ghuba ya Bengal kabla ya kupiga leo.

Idara ya Hali ya Hewa ya India imesema Kimbunga Fani ambacho ni kikali mno kinatarajiwa kupiga karibu na mji wa Odisha, wenye hekalu la Kihindi la Puri, kikiandamana na upepo mkali unaovuma hadi kilometa 200 kwa saa.

Majimbo ya Andhra Pradesh, Odisha na Bengal Magharibi yanatarajiwa kukumbwa na mvua kubwa na mafuriko. Karibu watu milioni moja wanatarajiwa kuhamishwa kutoka maeneo ya nyanda za chini hadi kwenye vituo vya muda, shule na majengo mengine yaliyo salama.


Muungwana
 
Nikushukuru neema ya Mungu haya majanga yasitukumbe, maana ni balaa sana na hivi hatuna ujuzi wa majanga vitatumaliza kama mdondo wa kuku.
 
Kutakuwa na tetesi ya vita maeneo mengi
Kutatokea matetemeko
Kutatokea vimbunga maeneo mengi
Nchi ya Tanzania kutaibuka mfalme katili asiyejali haki za binadamu

Na ule mwisho ukikaribia sana, taifa litainuka juu ya taifa lingine ili kupigana,,,,,, na ufalme utainuka juu ya ufalme.
 
Back
Top Bottom