Inawezekanaje kunguru akaingia kwenye Engine ya ndege mpaka analeta hitilafu bila wao kujua?

My take:

Inawezekanaje kunguru kuingia ndani ya engine bila wao kujua?

Ina maaana wameacha matundu makubwa ya ndege mkubwa kama kunguru?
Ndege kuingia kwenye engine za ndege ni tatizo kwenye sehemu nyingi duniani. Kuhusu kuacha matundu... nakushauri ujaribu ku-google jinsi injini za ndege za jet zinavyoundwa na zinavyofanya kazi. Jibu ni ndiyo. Enjini za jet kwa mbele zina uwazi ili kuvuta hewa. Ndege huwa wanavutwa kwa ndani!
 
Hata watu huwa wanavutwa, haya madege hatari mno, kule kongo ng'ombe ashawahi vutwa akaponea chupuchupu,
 
Sasa hizi injini wameshindwaga kuziwekea manyavunyavu angalau. Hawa jamaa wafikirie bwn, haezekan tatzo hilo lisiwe na solution!!!
Hilo wanalijua nadhani sababu ya calculation za msukumo wa hewa final ngana na kuweka wavu.
 
Ndege ya Shirika la ndege la Ujerumani, Condor, imelazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Moi, Mombasa, Kenya, baada ya kunguru wawili kuingia katika injini ya ndege hiyo.
Tukio hilo limetokea dakika chache baada ya ndege hiyo kuondoka visiwani Zanzibar, leo Mei 29, saa 3 asubuhi.

Kwa mujibu wa gazeti dada la Mwananchi, Bussiness Daily, kunguru wawili waliingia kwenye injini ya ndege hiyo.
Polisi wa Viwanja vya Ndege, Pwani, Noah Mviwanda amesema ndege hiyo ilitua salama katika uwanja wa ndege wa Moi, na hakuna abiria yeyote aliyejeruhiwa.

Wakati wanahabari wa Bussiness Daily walipotinga uwanjani hapo, abiria wa ndege hiyo walikuwa wakielekea hotelini.
Mmoja wa abiria ambaye hakutaka kutajwa jina, amesema, wataondoka kwa kutumia ndege nyingine, kesho.

Abiria mwingine, Morris, amesema: “Tunamshukuru Mungu tupo salama, tunakwenda hotelini, hadi kesho tutakaposafiri kwa ndege nyingine.”

My take:

Inawezekanaje kunguru kuingia ndani ya engine bila wao kujua?

Ina maaana wameacha matundu makubwa ya ndege mkubwa kama kunguru?
Ni tukio la kawaida kwani injini ya ndege inauwezo mkubwa wa kuvuta kitu chochote kilicho mbele yake, mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili huko marekani mtu mmoja aliyepita mbele ya injini ikiwa imewashwa alivutwa na kusagwa kwenye injini. Uwanja was ndege wa Mwanza ulikuwa na matokeo mengi ya aina hiyo enzi za minofu ya samaki iliyosababishwa na ndege wakubwa waliokuwa wanakula mabaki ya samaki hao.
 
Engine za ndege ziko wazi kama eneo lina ndege wengi kama anga la Kongo kuingia kwenye engine wala sio ajabu na ni hatari sana
 
Wanabodi tukumbushane kuwa engine huvuta hewa kuingia kwenye turbine yake kwa speed / velocity kubwa sana ili ndege iwenze kwenda. hivyo ndege wanyama wanaokuwa kwenye mkondo wa hewa inayovutwa au karibu na mkondo huvutwa hadi kwenye engine (Turbine) na kusagwa sagwa. Liquid / solid (damu / Nyama / manyoya) yao usababisha hitilafu kwenye muundo mzima wa engine.
Kwa kifupi ni hayo tu.
 
Un
Poor IQ wakati kila siku kuna wazanzibari wanalilia kwenda Yemen na Somalia kujiunga makundi ya kigaidi, tena wengine wanajifanya nzi na kupanda bure ndege ya 'Emirates' wakifika huko Urabuni wanabadilika.
unaudhi sana Uzi mzuri utauharibu kwa upumbavu wako
 
Ni tukio la kawaida kwani injini ya ndege inauwezo mkubwa wa kuvuta kitu chochote kilicho mbele yake, mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili huko marekani mtu mmoja aliyepita mbele ya injini ikiwa imewashwa alivutwa na kusagwa kwenye injini. Uwanja was ndege wa Mwanza ulikuwa na matokeo mengi ya aina hiyo enzi za minofu ya samaki iliyosababishwa na ndege wakubwa waliokuwa wanakula mabaki ya samaki hao.
Nalikumbuka hilo tukio na video yake ili treand sana yani yule jamaa hakujua kwamba amekufa maana alivutwa kwa spidi ya mwanga uji uji wa damu ndio ulitokea nyuma ya injini yani alikufa kifo kibaya sana na inaonyesha alijisahau kupita karibu na injini iliyokolea spidi vibaya mno akavutwa kama kiunyoya
 
Sio kunguru tu, ni ndege wengi wengine wanalingana na bata, ipo hivi engine za ndege si unazijua ? Sasa wakati ndege ikipaa hua inaenda mbele so ikikutana na hao ndege huko juu uso kwa uso ndege hao huenda kwenye engine ambayo imekaa kama feni na kusababisha engine isizunguke na hata kulipuka

Hii sio mara ya kwanza, pale mwanza imewahi kutokea kwa ndege ya jeshi zile fighter jet na pia kule marekani kuna ndege ilipata tatizo hilo hadi ikatua kwenye mto unaitwa HUDSON RIVER ,ipo movie yake kabisa
 
Sio kuingia ndani ya engine, hapana mie nakumbuka nilkuwa natoka nchi flani hapa Africa narudi bongo kupitia South Africa basi ile tunaruka tu kunguru au mwewe alivutwa kwa upepo mkali unaosababishwa na mzunguko wa engine na tukasikia kama kishindo flani afu ndege ikatua kwa dharura na baadae tukabadilishiwa ndege tukaendelea na hamsini zetu
 
Ndege ya Shirika la ndege la Ujerumani, Condor, imelazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Moi, Mombasa, Kenya, baada ya kunguru wawili kuingia katika injini ya ndege hiyo.
Tukio hilo limetokea dakika chache baada ya ndege hiyo kuondoka visiwani Zanzibar, leo Mei 29, saa 3 asubuhi.

Kwa mujibu wa gazeti dada la Mwananchi, Bussiness Daily, kunguru wawili waliingia kwenye injini ya ndege hiyo.
Polisi wa Viwanja vya Ndege, Pwani, Noah Mviwanda amesema ndege hiyo ilitua salama katika uwanja wa ndege wa Moi, na hakuna abiria yeyote aliyejeruhiwa.

Wakati wanahabari wa Bussiness Daily walipotinga uwanjani hapo, abiria wa ndege hiyo walikuwa wakielekea hotelini.
Mmoja wa abiria ambaye hakutaka kutajwa jina, amesema, wataondoka kwa kutumia ndege nyingine, kesho.

Abiria mwingine, Morris, amesema: “Tunamshukuru Mungu tupo salama, tunakwenda hotelini, hadi kesho tutakaposafiri kwa ndege nyingine.”

My take:

Inawezekanaje kunguru kuingia ndani ya engine bila wao kujua?

Ina maaana wameacha matundu makubwa ya ndege mkubwa kama kunguru?
Uchawi
 
Back
Top Bottom