Inawezekana Lipumba na Slaa kuunganisha nguvu 2015?

Naamini inawezekana endapo viongozi wetu watapunguza ubinafsi na chu wa madaraka, i believe we can
 
inawezekana kama dhamira ni kuingo'a CCM.....

bahati mbaya dhamira ni kuing'oa CCM na ni lazima sisi ndiyo tushinde(soma sisi wa chama fulani cha upinzani)... ni kwa mantiki hiyo hawawezi kuungana...

nadhani CHADEMA wanaweza kukubali fikra ya kuungana...wako kiasi fulani flexible kwa ushahidi wa mwaka 2000 ambapo Bob Makani alimpigia kampeni Lipumba na mikutano yao ya kampeni ilikuwa ni joint lakini sidhani kama CUF wanaweza hilo...bado wamefumba macho wakidhani wao ni most influncing party kwa sasa...iliwahi kuwa hivyo in 2000 na 2005 lakini si sasa...huu ni wakati wa CHADEMA ambao bila shaka wameng'ara sana tangu Slaa alipue bomu pale mwembe yanga TMK, kwa hiyo CHADEMA wanaona sasa ni zamu yao kuungwa mkono na CUF lakini CUF hawako tayari kusoma alama za nyakati ingawa maandishi yako wazi ubaoni...

ni kwa mantiki hiyo sioni CHADEMA wakikubali kuitoa haki yao ya uzaliwa wa kwanza kwa CUF nao CUF wakiwa bado usingizini hawana habari na mabadiliko yanayoendelea kutokea ni wazi kuwa kila mtu kivyake...

am sorry kwa washabiki hasa wa CUF...nafikiri wanahitaji kusoma maandishi ubaoni...kelele za kuwa CHADEMA ni CCM B hazitowafikisha popote, wanaweza kuwa na nguvu huko visiwani lakini kwa bara na overall kinchi wamefikia saturation point..no longer growing...they are rather declining..

mwenye macho haambiwi tazama.......
 
Back
Top Bottom