Inawezekana Lipumba na Slaa kuunganisha nguvu 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inawezekana Lipumba na Slaa kuunganisha nguvu 2015?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Calipso, Sep 15, 2010.

 1. C

  Calipso JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Baada ya utafiti nilioufanya,kwa kweli tunahitaji wapinzani tubadilike kumg'oa huyu jini CCM,tunahitaji kuunganisha nguvu za ziada, nimeangalia hivi vyama vyetu vya upinzani kwa kweli vimegawana maeneo,kwa mfano Cuf wanakubalika saana baadhi ya mikoa,na Chadema nao wanakubalika saana baadhi ya mikoa mengine,na kuna sababu nyingi zinazofanya hivi vyama kugawana maeneo,kwa mfano,moja ya sababu ni propaganda ya ccm inayofanywa kusingizia Cuf ni ya pemba na Uislam,na Chadema ni uchaga na Ukristo,kwa kweli ccm wamefanikiwa kwa hili,na wananchi wengi wamelipokea hili bila kujua athari zake,Hili lina Athari kubwa kwetu na ni faida kwa ccm ambapo wamefanikiwa kwa kitumia kitengo cha usalama kueneza hali hii,wamezigawa kura za wapinzani,Jamani tuamkeni,kwa nini isiwezekane kuunganisha nguvu ili hili dudu lipotee kabisa duniani? Bila ya kuwa kitu kimoja ni ngumu Kuing'oa ccm,kwani wanatumia pesa nyingi saana,askari woote wao,jeshi lipo nyuma yao,wana Usalama wa hali ya juu,hata wanafikia kushirikiana na baadhi ya mataifa makubwa kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani. Je itawezekana kuing'oa ccm bila kuwa kuunganisha nguvu zetu?
   
 2. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ushindi ni wa uhakika kukiwa na umoja wa vyama hivi viwili, vinginevyo ni kuwapa CCM miaka mingine mitano.
   
 3. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Hili likiwezekana CCM hawana pa kutokea.Mkuu Calipso wazo lako ni la maana sana,si wewe tu uliyeona hali hiyo....Kuna wakati kulishaanza kufanyika mazungumzo ya msingi ya kuunganisha nguvu ya vyama vya Upinzania haswa CUF na Chadema,lakini kuna ugumu mno kufikia tamati ya maazimio hayo........Kwa sababu mazungumzo yanatawaliwa na ubinafsi na nani ni bora kuliko mwingine?....Hivi sasa CUF ina nguvu upande mzima wa Pwani na Zanzibar,na Nguvu ya CUF inaongezwa zaidi na mwanaharakati Jussa..."Huyu jamaa ni wa kuangaliwa sana,ana uwezo wa kujenga na kubomoa" ni msomi mjenga Hoja mzuri lakini pia ni mbinafsi na mbaguzi mkubwa,Uwepo wake CUF unakiongezea sana chama nguvu na uweo wa kupambanua Hoja.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kuunganisha vyama halitawezekana, Ruzuku ya vyama vya Siasa inakokotolewa kwa vigezo vya idadi wa wabunge na kura za uraisi. Sasa chama kipi kiunge kingine baada ya uchaguzi kikose ruzuku?
   
 5. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo LIPUMBA HAWEZI KUKUBALI KUMWACHIA DR SLAA AMBAE NDDO ANA NGUVU KUBWA YA KISIASA NA TATIZO LINGINE CUF WAMEKWWISHA FUNGA NDOA NA CCM ZANZIBAR KWA JINA LA SERIKARI YA MSETO NA KUGOMBEA KWA LIPUMBA NI STRATEGY YA CCM ILI KUPUNGUZA KURA ZA UPINZANI, SO SIO RAHISI KWA SASA KUUNGANA, CUF INAPOTEZA NGUVU BARA NA BAADA YA KUINGIA KWENYE SERIKALII YA MSETO ZANZIBAR ITAPOTEZA NGUVU ZANZIBAR VILE VILE NA CREDIBILITY YAKE KWANI KUSHINDA ZNZ HAWAWEZI HIYO NI JANJA TU YA KUWAPA ULAJI AKINA SHEIKH SHARIF HAMADI NA VIONGOZI WA JUU WA CUF WANANCHI WA KAWAIDA WAMEUMIA
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Ni wazo zuri sana hilo ila umechelewa.

  CUF na CCM walishaanza kushirikiana zamani sana.

  [​IMG]
   
 7. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Acha uongo na propaganda za ccm hapa
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Nimebahatika kuhudhuria mikutano ya kampeni ya Cuf na Chadema mwaka huu. Mazingira niliyoyaona hasa kwenye mkutano wa Cuf yanaziba kabisa ule mwanya kidogo uliokuwepo wa ushirikiano. Kwa mfano kwenye mkutano mmoja, Cuf walimshambulia sana Dr Slaa wakisema Lipumba pekee ndiye kiongozi asiye na kashfa kwani hajapora mke wa mtu na mengine mengi yaliyofanya watu waione Cuf kama attack dog wa Ccm. Bahati nzuri, mambo haya badala ya kumbomoa Slaa, yamefanya watu wengi kuona kama ndiye pekee anaweza kuwakomboa watanzania miongoni mwa hawa wagombea wote na kwa baadhi ya maeneo kama Musoma mjini iliyokuwa stronghold ya Cuf Mara wamejimaliza wenyewe.

  Kuna kitu kimoja ambacho nakiona. Kama Ccm hawatang'oka mwaka huu, na mambo yakieendelea kama ilivyo sasa bila mabadiliko makubwa, Chadema kufikia mwaka 2015 watakuwa wamejijengea uwezo wa kuibwaga Ccm bila kuhitaji muungano au msaada wa chama chochote.
   
 9. k

  kisoti Member

  #9
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa nini ubinafsi uwekwe mbele zaidi kuliko maendeleo na maslahi ya nchi kwa ujumla?Tutawezaje kujikwamua katika janga hili la umaskini kama tutaweka mbele maslahi binafsi kuliko ya umma? Nani tumwamini zaidi katika kuikomboa Tanzania kutoka katika dimbwi la umaskini?Ubinafsi ndio sumu kubwa ya maendeleo ya nchi yetu.

   
 10. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ubovu mmoja wa wanacuf ni kwamba kwao hapendwi mtu wala hazipendwi sera.....wao huwa wanapigia kura chama,
  hilo ni moja ya tatizo kubwa sana kwa Cuf
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kama hata mmoja wao hata shinda mwaka huu then hamna haja ya wao kuunganisha nguvu 2015 kwani political capitol yao by then itakua ndogo mno. Mtu kama Lipumba kagombea tokea 1995, sasa 2015 afanye nini tena? As for Slaa ikitokea akashindwa nadhani bado ana nafasi ya kujijenga kwa 2015 lakini Lipumba ata kuwa liability tu.
   
 12. E=mcsquared

  E=mcsquared JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Calipso;

  To get a concrete answer on your problem, just follow the arithmetics below:
  1. CUF Bara=80% undercover CCM
  2. CUF visiwani= 100% Anti-CCM
  CHADEMA Jamhuri ya Muungano wa Tanzania = 100% Anti-CCM
  Rest of the opposition parties= 98% undercover CCM
  Nadhani baada ya hapo jibu unalo tayari!
   
 13. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wote wakiwa na umri gani vile? With Youth Vote na jinsi vijana wanavyoipanga sasa hivi sijui kama kuna any of above 40 kutoka upinzani akaweza kuleta mvuto wa kushinda nguvu za mgombea wa CCM ambaye kuna uwezekano akawa chini ya umri wa miaka 50.

  Lakini pia kama hawa wameshindwa kushirikiana sasa wakati wakiua kuna kazi ya kupanda kilima cha "incumbent candidate" hivi ni lipi litaweza kuzuia ubinafsi wao na vyama vyao katika mazingira ya kutamanisha kama 2015.

  omarilyas
   
 14. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ukweli ni kwamba CCM waliweza kufanikiwa kuwapachika makada yao katika vyama vyote vya siasa, isipokuwa CHADEMA tu. Kazi kubwa ya makada hawa katika vyama hivyo ni pamoja na kuvujisha siri na mipango ya vyama husika kwa CCM, kuhakikisha kuwa mipango yote ya vyama hivyo kuungana yanavurugwa ili wasifanikiwe, nk. CHADEMA nao waliweza kushtukia hilo, na kujaribu kuthibiti. Makada hawa mimi nawafananisha na virusi ndani ya vyama vya upinzani....! Lingine ni kwamba CCM imeshikilia DOLA, hivyo mgombea wake anazunguka kuomba kura kwa kutumia nafasi yake ya URAISI, hivyo rasimali za umma zinatumika kwa kampeni yake...! Kwa hiyo vyama vya upinzani kuungana ni vigumu sana kutokana na virusi vilivyopo katika vyama hivyo kwa lengo la kuzungukazunguka kuharibu na kuua vyama hivyo.
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Lipumba akiunganisha nguvu na Slaa atahama NCHI na kunyimwa posho zake za DENGU na KUNGUMANGA anazopewa na CCM
   
 16. C

  Calipso JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Duh! kwa hali hii,naweza kuamini kuwa ccm wana mapandikizi mpaka chadema.. maana nimeamini chadema ndio hawataki mshikamano na ndio wanaharibu na kuwagawa wapinzani,mfano kule mbeya. yaani humu tulitakiwa tusaidiane mawazo,ili vyama vyetu viweze kuwa kitu kimoja kuing'oa ccm,badala yake mnaongea pumba tu humu na kuwasaidia ccm.. NIMECHOKA MWENYEWE
   
 17. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hahaha... mtasema udini lakini ndio ukweli... CUF Waislamu ni wengi!... hata wakiungana na chadema therez No way waislamu wamchague mtu mwenye PHD katika sheria za kanisa... wapiga debe wote wa misikini wa CUF watahamia CCM .. mambo yaleyale tu!! TATIZO NI SLAA!!! MBOYE MBONA LIKUWA POA TU!..

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI! USHINDI WA KISHINDO 97% ZILIZOBAKI WATAGAWANA
   
 18. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Calipso,

  Jibu kwa swali lako kuu ni "Ndiyo inawezekana". Mimi naongeza kwamba inawezekana hata Oktoba 2010 endapo yafuatayo yatazingatiwa:-

  1. Watanzania watambue kwamba ni propaganda za CCM zisizo na msingi kwamba CUF ni ya Wapemba tu. Tukihesabu WaTz wa Bara waliuohudhuria mikutano ya Prof. Lipumba huko Ruvuma,Mtwara na Lindi, tutaridhika CUF ni chama cha kitaifa. Hata huko Kagera wapo.

  2. WaTz. tutambue ni uzushi mtupu unaorudiwa rudiwa na CCM kwamba eti CHADEMA ni chama cha Wachagga. Dr. Willibrod Slaa jemadari wa CHADEMA ktk mchakato huu, sio Mchagga bali ni M'Mbulu wa huko Karatu; Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Arfi ni Mfipa wa Mpanda kama Waziri Mkuu wetu Mizengo Pinda; Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, mpambanaji aliyetukuka, ni mzaliwa wa Kigoma Kaskazini (labda ni Mha). Bob Makani, Mwenyekiti Mstaafu aliyerithisha Mwenyekiti Freeman Mbowe, ni Msukuma wa Shinyanga. Huo uChagga uko wapi?

  3.WanaJF wataona nimeorodhesha wakuu wa CHADEMA, watano. Watatu yaani Bob Makani, Said Arfi na Zitto Kabwe ni Waislamu. Dr. Slaa na Freeman Mbowe ni Wakristo. Narudia ni uzushi mtupu wa CCM kusema CHADEMA ni chama cha Wachagga au cha Wakristo!!

  4. Kwa vile CUF na CHADEMA katika kampeni zinazoendelea wanaazimia kubadilisha Katiba ya Tanzania: endapo hata sasa wataachiana majimbo kimya kimya, itawezekana kupata Wabunge wengi zaidi.

  5. Wimbi la Dr Slaa kama Mgombea u-Rais linaloikumba Tanzania sasa litaweza kumwingiza Ikulu na ataweza kuunda Serikali ya Mseto akishirikisha Lipumba na wanaCUF wengine. Hasa ikizingatiwa kwamba kila kukicha udhaifu wa CCM na mkwere wao unadhihirika, WaTz wawe jasiri na kutaka mabadiliko ya kweli ifikapo 31 Oktoba.
   
 19. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mheshimiwa Calipso,
  KWA SASA UWEZEKANO WA LIPUMBA NA SLAA KUUNGANA NI MGUMU SANA. SABABU KUBWA NI KWAMBA LIPUMBA NA CUF SASA HIVI WANASHEREKEA KUUNDWA KWA SERIAKALI YA MUNGANO VISIWANI. KWAO HUO NI USHINDI MKUBWA. NIMEWASIKIA HATA BAADHI YA WAGOMBEA WAO WA UBUNGE WANATUMIA DHANA HIYO KUJINADI. CUF WANJIONA WANANGUVU KULIKO CHADEMA NA SASA WAKO KARIBU ZAIDI NA CCM KULIKO UPINZANI. LAKINI WANGEWEZA KUUNGANA TU HATA BILA KAMPENI WANGESHINDA.
   
 20. B

  BWAXY Member

  #20
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  pamoja na yote haya lakini kuna wenye macho lakini hawaoni, kuna wenye masikio lakini hawasikii.sijui tuwasaidieje hawa na kwa uhakika kabisa ndio wanaoturudisha nyuma. Hatutachoka kuwahubiria na iko siku watafungua macho na masikio waweze kutumia kura yao kwa manufaa bora ya taifa letu.
   
Loading...