Inawezekana kweli?

Inawezekana kweli?

Misunderstood

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2020
Posts
385
Reaction score
887
Habari vipenzi

Nina swali linanitatiza mno, nikaona ni vyema nililete huku hakika nitapata majibu!

Inapata miezi kama saba sasa tangu niachane na mpenzi wangu niliyemzoeaga sana niliyekuwa naye kwa kipindi cha miaka sita! Mwaka wa sita na wa mwisho ulikuwa mbaya sana kwetu ilopelekea mwezi wa mwezi wa 02/2020 uhusiano wetu kugonga mwamba. Nikapitia maumivu makali mnooo sikudhani hata kama nitafika hii leo. Na sasa nimebakiwa na hofu je ipo siku nitamsahau kabisa? Haitaniaffect kwenye mahusiano mengine hasa ya ndoa?

Sasa naomba sana kwa wale waliowahi kupitia extreme pain and heart breaks kutokana na mahusiano kuvunjika tafadhali waniambie experience yao! Je, walifika muda hayo maumivu kuisha kabisa? Hata walioko kwenye ndoa haijawahi kuwaathiri? Ilichukua muda gani hiyo hali kuisha kabisa? Iliisha baada ya kufanya nini?

NB: Ilishindikana kureconcile kabisa, ilikuweka mambo sawa.

Natanguliza shukrani zangu! Asante.
 
Sasa naomba sana kwa wale waliowahi kupitia extreme pain and heart breaks kutokana na mahusiano kuvunjika tafadhali waniambie experience yao! Je walifika muda hayo maumivu kuisha kabisa? Hata walioko kwenye ndoa haijawahi kuwaathiri? Ilichukua muda gani hiyo hali kuisha kabisa? Iliisha baada ya kufanya nini?
NB: ilishindikana kureconcile kabisa, ilikuweka mambo sawa.

Natanguliza shukrani zangu! Asante.

Nimewahi kupitia unayopitia na ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuijua JF kwasababu katika kugoogle namna ya kusahau mtu nikaletwa huku JF

Nilikuwa natamani kulia lakini machozi hayaji
Appetite ikapotea
Nikapiga hata simu nyumbani kuomba kughairisha mwaka manake nilijiona hata darasani hakieleweki

Nikaweka uzi humu wa kuomba msaada wa namna ya kumsahau ambapo kimsingi nilipata mawazo kadhaa ambayo yalinisaidia kiasi chake

Kimsingi kilichonisaidia kupotezea ni baada ya kuweka mbele mambo ya msingi zaidi katika maisha yangu,nikaanza kutumia muda wangu mwingi kusoma sana kwasababu ndio kilinipeleka kule

Nikaanza kufikiria mtu nayempenda zaidi katika hii dunia ambaye ni baba yangu,nikaanza kuwasiliana nae sanaaaaaa

Nikaanza kwenda kanisani siku za jumapili na jumamosi kufanya usafi

Jitahidi kuwa busy na mambo yako,hayo unayopitia sasa hayatakuwa hivyo milele....pole,pambana
 
Naomba link ya huo uzi Mkuu
 
Time heals, muda unavyokwenda itakua kawaida tuu, chamsingi usije jaribu kuwasiliana nae, Kuna watu w muhimu ambao wanakupenda xana as Johana said hapo juu, 4 the meantime wakat unapona jeraha, ishi kwaajili yao
 
Nimewahi kupitia unayopitia na ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuijua JF kwasababu katika kugoogle namna ya kusahau mtu nikaletwa huku JF

Nilikuwa natamani kulia lakini machozi hayaji
Appetite ikapotea
Nikapiga hata simu nyumbani kuomba kughairisha mwaka manake nilijiona hata darasani hakieleweki

Nikaweka uzi humu wa kuomba msaada wa namna ya kumsahau ambapo kimsingi nilipata mawazo kadhaa ambayo yalinisaidia kiasi chake

Kimsingi kilichonisaidia kupotezea ni baada ya kuweka mbele mambo ya msingi zaidi katika maisha yangu,nikaanza kutumia muda wangu mwingi kusoma sana kwasababu ndio kilinipeleka kule

Nikaanza kufikiria mtu nayempenda zaidi katika hii dunia ambaye ni baba yangu,nikaanza kuwasiliana nae sanaaaaaa

Nikaanza kwenda kanisani siku za jumapili na jumamosi kufanya usafi

Jitahidi kuwa busy na mambo yako,hayo unayopitia sasa hayatakuwa hivyo milele....pole,pambana

Pole joanah ila kumsahau/kumtoa moyoni mtu ambae uliuaminisha moyo kuwa anao umuhimu sana sio kazi rahisi. Kusema kwa mdomo huwa ni rahisi sana ila kazi huja kwenye utendaji nadhani tuliowahi kupitia hii hali tunaelewa, nakumbuka ilinichukua mda sana kuwa sawa lakini imenisaidia pia kwa mahusiano yangu baada ya hapo nimekuwa mwepesi wa kukubaliana na hali pindi ikitokea kuachwa/kuachana na mtu.
 
Pole joanah ila kumsahau/kumtoa moyoni mtu ambae uliuminisha moyo kuwa anao umuhimu sana sio kazi rahisi. Kusema kwa mdomo huwa ni rahisi sana ila kazi huja kwenye utendaji nadhani tuliowahi kupitia hii hali tunaelewa, nakumbuka ilinichukua mda sana kuwa sawa lakini imenisaidia pia kwa mahusiano yangu baada ya hapo nimekuwa mwepesi wa kukubaliana na hali pindi ikitokea kuachwa/kuachana na mtu.
Asante recycle Bin

Ni kazi ngumu kweli lakini ikifika muda mambo yameharibika hakuna namna zaidi ya kupambana umsahau

Maisha lazima yaendelee
 
Kweli kabisa maana kuna mda lazima ukubali ukweli mchungu japo inauma hasa ukiwaza hata ufanyaje(zuri au baya) hautoweza kubadili uhalisia wa maamuzi ya mtu hasa kwenye suala zima la mahusiano.
 
Back
Top Bottom