Inawezekana kweli Barbara Gonzalez ni tatizo Simba

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,621
16,700
NIMEONA na kusikia kelele nyingi mitandaoni kuhusu Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez. Inasemekana amekuwa shida pale Simba. Inasemekana.

Nimeona baadhi ya watu wakisema kuwa Barbara amekuwa akikwamisha baadhi ya vitu pale Simba. Tena wanaosema, wanaongea kwa kujiamini kweli.

Ni ngumu sana kuamini hivyo. Unajua kwanini? Subiri nitakueleza. Simba kama zilivyo taasisi nyingine kubwa ina changamoto zake nyingi. Ni kweli. Hakuna taasisi kubwa inayokosa changamoto.

Lakini hili la watu kujitokeza hadharani na kusema mtendaji mkuu ndiye chanzo cha matatizo makubwa pale Simba limenishtua zaidi. Mtendaji mkuu ndiye roho ya taasisi yoyote. Mipango yote huanzia na kumalizikia katika ofisi yake. Ila katika soka hii ni ofisi nyeti zaidi.

Unajua kwanini? Ni kwa sababu soka lina njia zake. Soka lina mipango na uendeshaji wa aina yake. Kuna fitina kubwa sana katika soka. Na kuna watu wa soka. Sasa ukisikia kuwa mtendaji mkuu amekuwa tatizo hadi watu wa mpira wanakaa pembeni, basi ni tatizo kubwa. Hiki ndicho kinaelezwa pale Simba. Inasemekana baadhi ya watu wamejiweka pembeni kwa sababu ya mtendaji wao.

Msimu uliopita tatizo hili lilizungumzwa chini chini. Baadaye baadhi ya wajumbe wa bodi kama Kassim Dewji walijitokeza hadharani na kumlalamikia wazi mtendaji mkuu kuwa anataka kufanya kila kitu peke yake.

Ni wachache kama Kassim wenye ujasiri wa kujitokeza hadharani na kusema haya. Ila yawezekana msimu uliopita maji yalimfika shingoni akaamua kusema ukweli hadharani.

Huyu ni mtu mkubwa ndani ya Simba. Amefanya makubwa Simba na soka la Tanzania analifahamu kwelikweli. Simba itakwendaje kama watu kama yeye hawashirikishwi? Inafikirisha sana. Ukisikia mtendaji mkuu Simba amekuwa tatizo unashtuka kwa sababu kubwa mbili

Kwanza, huyu ni mtu wa karibu sana wa mwekezaji Mohamed Dewji. Ndiye aliyebeba maono ya biashara yote ya mpira Simba. Inawezekana anatenda kwa kufikiria zaidi maslahi ya mwekezaji kuliko ya Wanasimba wenyewe. Hili ni tatizo kubwa kwasababu Simba ni ya watu. Wenye Simba yao wanataka zaidi furaha ya uwanjani kuliko hayo mambo mengine. Ndio maana wanaweza kupishana maono na wenzake.

Pili, katika picha ya nje, Simba imemtengeneza Barbara kuonekana kama mtu mahiri katika taasisi yao. Maendeleo makubwa yanayofanywa na Simba yanaonekana ni utendaji mahiri wa Barbara. Ni kwanini wameamua kufanya hivyo kama Barbara ni tatizo? Inafikirisha. Pengine wakati wanamtengeneza kuwa hivyo hawakuwaza madhara ya baadaye. Mtu akipewa sifa kubwa sana kuna sehemu lazima atawasumbua. Ila tukirejea katika

mafanikio ya Simba ndani ya uwanja tangu Barbara ameingia ni wazi kuwa kuna tatizo mahala. Katika msimu wake wa kwanza Simba ilibeba makombe yote ya ndani na kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yawezekana ilikuwa ni misingi imara aliyoacha mtangulizi wake, Senzo Mbatha. Inawezekana Senzo alijenga msingi wa mafanikio haya ndiyo sababu ikawa kazi rahisi kwa Barbara katika msimu wake wa kwanza.

Nini kimetokea msimu uliopita? Simba ilipoteza kila taji ililotwaa. Ndio msimu ambao watu walianza kumnyooshea vidole mtendaji mkuu.

Simba ikaondoshwa katika Ligi ya Mabingwa tena nyumbani. Angalau ikajipoza kwa kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Lakini kwa hapa ndani hakukuwa na maajabu sana.

M-simu huu mambo yameonekana kuwa magumu zaidi. Simba ikaanza kwa kupoteza Ngao ya Jamii. Kwenye ligi mpaka sasa ipo nafasi ya tatu na uwezekano wa kutwaa ubingwa ni mdogo.

Kwanini? Ni kwa sababu kuna shida ndani ya taasisi. Kuna shida katika maeneo nyeti. Nitazungumzia baadhi.

Kwanza, msimu uliopita Simba iliuza wachezaji wake wawili mahiri, Luis Miquisone na Clatous Chama. Ni kweli ilivuta mpunga mrefu, ila ndani ya uwanja ikabaki ovyo. Ikafeli zaidi katika usajili wa wachezaji. Haikununua wachezaji mahiri kama ilivyotarajiwa. Ni tatizo la nani? Hapa ofisi ya mtendaji mkuu inawajibika.

Pengine hawakuwa wepesi kusaka wachezaji na kukamilisha dili zao haraka. Mwisho wa siku wakanunua wachezaji wengi wenye uwezo wa kawaida.

Tatizo kubwa likaonekana zaidi katika usajili wa msimu huu. Wachezaji wengi mahiri iliowataka Simba hawakuweza kujiunga na timu hiyo.

Victorien Adebayor ndiye alikuwa wa kwanza kutajwa pale Simba. Hata hivyo dili lake likaenda kwa kasi ya kinyonga na akajiunga na RS Berkane ya Morocco.

Vipi kuhusu Stephane Aziz Ki? Simba ilitajwa kuwa ya kwanza kumhitaji. Kila kitu kilionekana kuwa vizuri mwanzoni, ila cha kushangaza akatua Yanga. Ilikuwa ni pigo kubwa. Ikaonekana kuwa Simba itaachana na Chris Mugalu na Meddie Kagere. Ikaonekana wazi kuwa anahitajika straika mahiri wa kuziba nafasi yao.

Akatajwa Cezar Manzoki. Habari zake zikaandikwa sana. Ikaelezwa kuwa Simba wamemalizana naye. Lakini nini kilitokea? Dili likafeli na Vipers wakamuuza China dakika za mwisho. Inasikitisha sana.

Eneo la pili ambalo limekuwa na shida ni katika makocha. Ghafla Simba ikaachana na Didier Gomes kwa madai kuwa ameshindwa kufikia malengo. Alikuwa amedumu kwa miezi tisa tu.

Ikamleta kocha Pablo Franco. Mwalimu asiyekuwa na uzoefu na soka la Afrika. Akaja kujifunza Simba na matokeo yake akashindwa kuwapa chochote kikubwa.

Nini kimetokea baada ya hapo? Akaja Zoran Maki ambaye hakutimiza hata miezi miwili kazini. Akatimka zake baada ya kushindwa kuelewana katika baadhi ya mambo. Simba ikalazimika kumchukua mzawa Juma Mgunda kama mbadala wa muda mfupi. Hadi sasa haieleweki kama Mgunda atasalia hadi mwisho wa msimu ama la.

Hivyo kwa ufupi katika utendaji Simba kuna vitu vinapwaya. Inawezekana mtendaji wa sasa anataka kufanya kila kitu peke yake, lakini hana uzoefu wa kutosha katika eneo hilo.

Hili lipo wazi. Barbara hana uzoefu katika soka. Kazi yake kubwa ya soka ameanzia Simba. Ana mengi ya kujifunza kwa wazoefu waliopo pale. Ila kama wazoefu wenyewe wanamuona kama ni tatizo, basi Simba ina safari ndefu.

Nakumbuka Yanga ilikuwa na international game Ccm Kirumba, basi Yale majizi yanayojiita makomandoo yakasafiri kwa gharama zao kwenda Mwanza kwa matarajio ya kurudi na pesa kibao za milangoni.

Basi siku moja kabla ya mechi Yusuf Manji akatangaza mechi itakuwa bure hakuna kiingilio.

Yale majizi ilibidi yarudi Dar kwa lift za malori na wengine kutumia nauli na ndugu zao na hapo ndio Manji alianza kupigwa vita.

Sasa majizi ya Simba muelewe Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya ni ya kwenda kuroga.

Pili Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti za kumhonga refa.

Tatu Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti mnakwenda kuwahonga wachezaji wa timu pinzani.

Huu ndio Ubaya wa Barbara kwa Simba, na ukisikia kuna mtu anajiita eti ni mtu wa mpira ujuwe ni jizi tu hilo hakuna lolote.

Tuelezeni wanachama wa Simba tangu mumchaguwe Mwenyekiti wenu Murtaza Mangungu Mission town, ambaye ndio muwakilishi wa wa wanachama amefanya nini?
 
Sahihi kabisa, kinachomuondoa Barbara pale kwa Makolo ni kwamba amezuia upigaji wa kijinga ndio maana wanaona bora aondoke. Lakini nafuu kwetu acha waparangane wakishtuka ligi imeisha.
 
Nakumbuka Yanga ilikuwa na international game Ccm Kirumba, basi Yale majizi yanayojiita makomandoo yakasafiri kwa gharama zao kwenda Mwanza kwa matarajio ya kurudi na pesa kibao za milangoni.

Basi siku moja kabla ya mechi Yusuf Manji akatangaza mechi itakuwa bure hakuna kiingilio.

Yale majizi ilibidi yarudi Dar kwa lift za malori na wengine kutumia nauli na ndugu zao na hapo ndio Manji alianza kupigwa vita.

Sasa majizi ya Simba muelewe Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya ni ya kwenda kuroga.

Pili Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti za kumhonga refa.

Tatu Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti mnakwenda kuwahonga wachezaji wa timu pinzani.

Huu ndio Ubaya wa Barbara kwa Simba, na ukisikia kuna mtu anajiita eti ni mtu wa mpira ujuwe ni jizi tu hilo hakuna lolote.

Tuelezeni wanachama wa Simba tangu mumchaguwe Mwenyekiti wenu Murtaza Mangungu Mission town, ambaye ndio muwakilishi wa wa wanachama amefanya nini?
Sahihi kabisa kuna watu wqlikuwa wana neemeka na hizi klabu kiujanja ujanja
-friends of simba ( kaburu)
 
Unajua kuna baadhi ya mambo kuyaanza kuyahusisha na mwenendo mbovu wa CEO sioni kama ni sahihi.

Ishu ya Zoran Maki kusepa mapema sidhani kama kuna mshabiki wa Simba yeyote ambaye anaweza kulaumu

Kocha ambaye alikuwa hamtaki Chama, Onyango, Phiri na kutuwekea kina Outtara. Kwangu mimi naona tulichelewa sana kumtimua na pengine hili ndio naweza kulihesabu kama tatizo kwa CEO kwa kushindwa kufanya maamuzi ya mapema

Ishu ya Manzoki ilikuwa na mambo mengi yaliyowekwa na management ya Vipers kama kikwazo.

Zipo habari zinazodai kuwa Vipers waliona upo uwezekano wa kukutana na Simba kwenye michuano ya kimataifa, so kuwapa Manzoki ni kumpa adui silaha ya kukushambulia mwenyewe.
 
Changamoto nyingine za Huyu mama ni pamoja na..

-i. KUSHINDWA kuitembelea Timu ya Wanawake Simba Queens

-ii. Kuzuia wachezaji kwenda Offisini kwake.

- iii. Kugeuza Gari yake kuwa Offisi.

-iv. Wachezaji kucheleweshewa posho.

V. LAWAMA kutoka body, MWENYEKITI, Manara nk nk nk........
 
Nakumbuka Yanga ilikuwa na international game Ccm Kirumba, basi Yale majizi yanayojiita makomandoo yakasafiri kwa gharama zao kwenda Mwanza kwa matarajio ya kurudi na pesa kibao za milangoni.

Basi siku moja kabla ya mechi Yusuf Manji akatangaza mechi itakuwa bure hakuna kiingilio.

Yale majizi ilibidi yarudi Dar kwa lift za malori na wengine kutumia nauli na ndugu zao na hapo ndio Manji alianza kupigwa vita.

Sasa majizi ya Simba muelewe Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya ni ya kwenda kuroga.

Pili Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti za kumhonga refa.

Tatu Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti mnakwenda kuwahonga wachezaji wa timu pinzani.

Huu ndio Ubaya wa Barbara kwa Simba, na ukisikia kuna mtu anajiita eti ni mtu wa mpira ujuwe ni jizi tu hilo hakuna lolote.

Tuelezeni wanachama wa Simba tangu mumchaguwe Mwenyekiti wenu Murtaza Mangungu Mission town, ambaye ndio muwakilishi wa wa wanachama amefanya nini?
Kuna kaukweli hapa
 
Mkude kuwa mdokoaji wa 'mali' za Mwamedi.
 
Huu ndiyo ukweli ambao huwa nawaambia hata YANGA. Ukisikia Mtu anajiita mtu wa mpira Simba au Yanga damu ujue ni hawa wapigaji. Kwanza naona Babra kakaa sana, kwa uswahili na majungu ya mpira wetu asingekaa hata Mwaka. Mimi shabiki wa Yanga wa kawaida, ila huwa nawaambia wanasimba mkiruhusu wahuni mnarudi hatua elfu nyuma. Babra kazuia ulaji

Hivi hawajiulizi wale Watu unawakuta jengo la Yanga au Simba wamekaa wanapiga soga muda wote wanapata wapi rizki zao? Halafu ndiyo wanajifanya wana uchungu sana na timu!!

Kwa mtu professional kama Babra hawezi kutoa handout kwa wajanjawajanja kama hawa. Ila kawanyoosha, miaka zaidi ya miwili!!
 
mpira wa bongo ni wa kihuni Barbara anataka kusimama kwenye mstari wa weredi na misingi ya uongozi kama aliyojifunza kwenye club zingine zenye mafanikio Al ahly na Kaizer Chiefs alipozitembelea kujifunza namna ya uendeshaji wa club.

kuna wahuni wako kwenye hizi club wanafanya maisha kwa pesa za upigaji.wabongo upigaji na uhuni sio kwenye soka tu hata taasisi zingine kama serikali na sekta binafsi wabongo wanawaza kuiba na upigaji tu,ukiwabana watakuchukia.
 
Kuna vitu ambavyo vipo wazi havijifichi.
Tuanze Kwa usajili kwenye hili eneo Babra alishindwa kabisa wakati wanauzwa wachezaji Chama na Luis konde boy Tena Kwa bei kubwa klabu ilitetereka pia Simba iliendelea kubaki na wachezaji mizigo bila sababu ya msingi timu kama Azam tumeshindwa kupambana mayo Kwa wachezaji wa ndani.
Eneo la pili ni benchi la ufundi Kishingo aliondoka baada ya kufanya mazungumzo na Mo pamoja na Babra na wakasema anaondoka Kwa changamoto za kifamilia lakini muda mchache akawa kaajiliwa na timu nyingine Morocco kama haitoshi tukasikia anaidai Simba.
Baada ya kutolewa na timu ya Botswana benchi la ufundi lilivunjwa ikiwa ni pamoja na makocha wa viungo na kipa mpaka Leo sidhani kama Kuna mtu anaweza kutueleza Nini yalikuwa makosa ya kocha wa viungo na makipa. Pablo alipoondolewa na kuletwa Zoran Maki ambaye pia aliondoka aliajiliwa kocha wa muda Mgunda pamoja na kocha wa makipa wa.muda Cha ajabu timu kubwa kama Simba haikuwa na kocha wa viungo Wala makipa Kwa muda mrefu happy tumlaumu nani.
Wore tulisikia jinsi Mo alivyopinga mkataba wa Azam wa miaka kumi wa bilioni 40 Kwa kusema haulingani na thamani ya Brand ya Simba ila tumeshuhudia Mo akiweka udhamini wa milioni 250 inabidi ieleweke alikuwepo kuifanya Simba iende mbele au kulinda maslahi ya mwekezaji.
Mwisho anapaswa kuishukuru Simba kwani imemtangaza vizuri mpaka ameweza kuteuliwa caf na kukutana na viongozi wakubwa fifa.
Kuna matukio ya aibu kama ya ushirikina dhidi ya mechi ya mbeya City ambalo lilikuwa linajirudia baada ya lile la Kaizerchief tunaamini yeye so sehemu ya tukio lakini kama mtendaji mkuu alichukua hatua gani ili lisijirudie na kuchafua brand ya Simba?
 
I concur with you comrade,majizi ndio yanayopiga kelele baada ya kubanwa na bibie
Nakumbuka Yanga ilikuwa na international game Ccm Kirumba, basi Yale majizi yanayojiita makomandoo yakasafiri kwa gharama zao kwenda Mwanza kwa matarajio ya kurudi na pesa kibao za milangoni.

Basi siku moja kabla ya mechi Yusuf Manji akatangaza mechi itakuwa bure hakuna kiingilio.

Yale majizi ilibidi yarudi Dar kwa lift za malori na wengine kutumia nauli na ndugu zao na hapo ndio Manji alianza kupigwa vita.

Sasa majizi ya Simba muelewe Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya ni ya kwenda kuroga.

Pili Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti za kumhonga refa.

Tatu Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti mnakwenda kuwahonga wachezaji wa timu pinzani.

Huu ndio Ubaya wa Barbara kwa Simba, na ukisikia kuna mtu anajiita eti ni mtu wa mpira ujuwe ni jizi tu hilo hakuna lolote.

Tuelezeni wanachama wa Simba tangu mumchaguwe Mwenyekiti wenu Murtaza Mangungu Mission town, ambaye ndio muwakilishi wa wa wanachama amefanya nini?
 
Nakumbuka Yanga ilikuwa na international game Ccm Kirumba, basi Yale majizi yanayojiita makomandoo yakasafiri kwa gharama zao kwenda Mwanza kwa matarajio ya kurudi na pesa kibao za milangoni.

Basi siku moja kabla ya mechi Yusuf Manji akatangaza mechi itakuwa bure hakuna kiingilio.

Yale majizi ilibidi yarudi Dar kwa lift za malori na wengine kutumia nauli na ndugu zao na hapo ndio Manji alianza kupigwa vita.

Sasa majizi ya Simba muelewe Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya ni ya kwenda kuroga.

Pili Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti za kumhonga refa.

Tatu Barbara hawezi kutowa pesa kwa kumdanganya eti mnakwenda kuwahonga wachezaji wa timu pinzani.

Huu ndio Ubaya wa Barbara kwa Simba, na ukisikia kuna mtu anajiita eti ni mtu wa mpira ujuwe ni jizi tu hilo hakuna lolote.

Tuelezeni wanachama wa Simba tangu mumchaguwe Mwenyekiti wenu Murtaza Mangungu Mission town, ambaye ndio muwakilishi wa wa wanachama amefanya nini?
100% upo sahihi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom