Wajuzi wa mpira, nini sababu ya Simba kufungwa na Al Ahly?

Mdomo kaka,hawa makolo walishadadia mambo ya mamelodi kuliko kujiandaa kuukabili mchezo wao na al ahly,kingine hizi mechi za mtoano watu timu haziangalii takwimu Bali wanaangalia ushindi wa magoli.

Hizo takwimu za umiliki za Simba usifikirie kuziona Cairo maana mametumia nguvu nyingi Sana lakn wamepigwa kwahy automatically miili imechoka na watawenda Cairo kukamilisha ratiba tu.
 
Kolozzzz kolozzzz kolozzz
Wizardiiiiii wizardiiii wizardiiiii
Kimokooo kimokooo Cha motooo.

Leo tutawafundisha namna ya kumiliki mpira na kushinda, kwa pamoja. Mana hata yanga mechi za kwanza kwanza tulipatwa na homa hiyo. Kiufupi, simba wanafaya nyayo zetu
 
Mdomo kaka,hawa makolo walishadadia mambo ya mamelodi kuliko kujiandaa kuukabili mchezo wao na al ahly,kingine hizi mechi za mtoano watu timu haziangalii takwimu Bali wanaangalia ushindi wa magoli.

Hizo takwimu za umiliki za Simba usifikirie kuziona Cairo maana mametumia nguvu nyingi Sana lakn wamepigwa kwahy automatically miili imechoka na watawenda Cairo kukamilisha ratiba tu.
Mbona umeandika kishabiki sana na sio kitaalamu?
Nilitegemea ungetoa sababu za kiufundi zaidi ili kuelimishana lakini umeanza mdomo sijui wanaenda kukamilisha ratiba kumbuka meza huwa zinapinduliwa kama timu itacheza vizuri zaidi
 
.......mchezo wa mpira wa miguu ni kutafuta nafasi na kuzitumia kuzalisha goli, nafasi ni nini?, nafasi ni mazingira bora na rahisi ya kufunga goli, mfano:ukibaki wewe na kipa au na beki mmoja hiyo ni nafasi, Sasa haya yote simba walipata tena zaidi ya mara mbili au tatu.........
..........kwa nini tumepoteza, ni simple hatukutumia nafasi tulizotengeneza wakati huohuo wenzetu walitengeneza moja na wakaitumia kitu ambacho ndo lengo la mchezo, yaani tafuta nafasi itumie......
..........swali la msingi Kwa nini hatukutumia nafasi zile?, hapa ndo pana majibu mengi na mengine ni dhahania, nayo ni kama yafuatayo:
1.Pengine ndo ubora wetu ulipoisjia
2.Pengine ni kukosa utulivu kwa walipata nafasi
3.Pengine ni hujuma za wachezaji wenyewe
4.Pengine ni kukosa bahati(Alex Ferguson)
NB:kosa alilofanya inonga sio kubwa kuliko la waliotakiwa kutumia nafasi zaidi ya tatu wakashindwa, kama wataamua, uwezekano wa kupindua matokeo upo, goli moja ni la kawaida sana ktk football
 
Ubora wa wachezaji ndiyo umeishia pale, Simba inahitaji quality ya juu zaidi ya hii iliyonayo, huwezi tegemea tena kina Saido wakufikishe mbali na hakika Simba Haina wachezaji wa kuwafikisha nusu fainali hivyo management iamue kuingia sokoni kuleta quality players lakini kinachosikitisha wachezaji wanaokuja ni wa kupigwa tu Kila siku ni kama vile timu Iko auto pilot.
 
Binafsi niliona matatizo yafuatayo.
~Simba hawana clinical number 9
~Wachezaji wa simba ni wagumu kufanya maamuzi ya haraka kwenye maeneo ambayo inahitajika kufanya hivyo.
~Simba wachezaji wengi umri umewatupa mkono
~Bado Simba tuna tatizo la kupoteza mipira kizembe tena kwenye maeneo hatarishi.
~Simba tuna changamoto kwenye eneo zima la kiulinzi.
~Simba hawapo vizuri kwenye kutumia ipasavyo mipira iliyokufa pamoja na kona
~mastrika wa simba wanahitaji walau chance nyingi ili wafunge goli moja.
NINI KIFANYIKE CAIRO?
~Wawaheshimu Al ahly kwa kukaba zaidi then watumie kaunta kupata goli na washikilie bomba kwelikweli,kinyume na hapo habari yetu ndio imeisha hapa
 
Mdomo kaka,hawa makolo walishadadia mambo ya mamelodi kuliko kujiandaa kuukabili mchezo wao na al ahly,kingine hizi mechi za mtoano watu timu haziangalii takwimu Bali wanaangalia ushindi wa magoli.

Hizo takwimu za umiliki za Simba usifikirie kuziona Cairo maana mametumia nguvu nyingi Sana lakn wamepigwa kwahy automatically miili imechoka na watawenda Cairo kukamilisha ratiba tu.
Ngoja tuwaone UTOPOLO ambao hawakukomaa na mambo ya SIMBA wakafocus kwenye mechi yao
 
Back
Top Bottom