Inawezekana kupenda tena baada ya kuumizwa?

Inawezekana kupenda tena baada ya kuumizwa?

Kim2 Asante ndugu yangu. Kusema ukweli naona giza mbele yangu. Kazi ninayo inayoniwezesha kula na kufanya mambo mengine.
Imakuwaje mtu ambae umemsubilia muda wa miaka minne au mitano anakuja kukutenda bial huruma?
 
kwa mujibu wa maelezo yako, ni kwamba mtu apende kwa machale!? kwamba part 1 akizingua awe amejiandaa ku-join part 2?
No, No...No please namaanisha penda saaana tena deeply in love ila ujiwekee mawazo ya one day unaweza achwa hivyo ujiandae kama in case... Sisemi uwe na wawili at the same time laa hasha.
 
Kaka pole sana kwa yaliyokukuta, piga moyo konde then move one mungu wetu ni mwema sana hapo amekuepusha na matatizo makubwa sana, kitu ambacho kinakusumbua ni muda mliokaa na huyo mtu lakin hio haijastify kuwa umuoe

Ni bora umeona ubaya wake ss hivi kuliko mngekuwa mmeshafunga ndoa, tulia usije kukurupuka kutafuta mtu wa kureplace coz ilo ni kosa kubwa sana uguza majeraha yako kwanza

Baada ya muda utajisikia aman na muombe sana mungu akuongoze kwenye kutafuta mpenzi wa kweli kwa akil zako mwenyewe hutaweza
Ninamaumivu kama yako ila namshukuru mungu amenipa ujasiri hadi hv ninayoandika hapa am happy again and ready to move on ila it takes time

Mwisho kabisa ni bora kuvunja uchumba na sio kuvunja ndoa,take it in a positive way and move on baada ya miaka mmne au mitano ndio utajua kwanini mungu alikuepusha na huyo mti
 
Huwezi kupenda tena kwa dhati kama umetendwa,utajua ni wale wale
 
Asante sana Madaraka Daniel kwa ushauri mzuri. Naomba uniambie kama umeweza kupenda mwanamke mwingine kwa kiwango kama zamani au hata kuzidisha.
 
Asante sana Madaraka Daniel kwa ushauri mzuri. Naomba uniambie kama umeweza kupenda mwanamke mwingine kwa kiwango kama zamani au hata kuzidisha.

Yani unaweza ukapenda zaidi ya mwanzoni. Achilia tu moyo wako
 
Mkuu umri wako usikukatishe tamaa ya kutafuta yule anayestahili kwako kuna msemo unasema "usioe kisa umri umeenda au umeona rika lako wameoa au wazazi wanakuuliza mwanangu viipi?"angalia furaha yako iko wapii alafu wewe ni mwanaume hata ufikishe 50 yrs bdo unaweza oa na kupata watoto
Don't give up

wakuu nawasalimu!
niwakumbushe kitu kimoja, mwili ni kasha njisia imewekwa na mwenyewe matendo hufuata,kuna matendo yaonekanayo na Yale yasioonekana. yasioonekana no kama Yale ya kupenda haya hufa kwa muda na kuzinduka! MTU humchukia wake aliemkuta anafinywa, akasau na kumrudia! iweje were usione utakaempenda tena? pengine ni mgonjwa was kupenda bats kwa ile kunya kunya! unaweza kuta bats anahara! tujazie hapo!
 
Mkuu, Mbona sikuelewi hata kidogo? Nnani alikuambia kuwa huyo ndiye mpenzi wako pekee?? Ulifahamuje kuwa huyo ndo umempenda kuliko wengine wote?
Achana na maneno mlioambiana mkiwa faragha. Yale ni maneno tu. Yule utakayempenda bado hujakutana naye mkuu. Hivi unajua maana ya mapenzi? Hilo neno lenyewe linaonesha ni zaidi ya penzi moja. Weye ulipenda, kumbe hukupendwa. Hivyo hakukuwa na Mapenzi. Siku utakapokutana na hilo penzi na weye utoe penzi, ndo utajua kumbe kuna kupendana kusiko na mwosho.
Fungua tu macho mkuu, iko siku utakutana na penzi lako la kweli lisilo isha wala kuchuja. Viruka njia hawajui penzi
 
Dear pole sana . 5 years ? Uchumba or boyfriend and girlfriend ? To me naona ilikuwa ni miaka mingi sana especially kwa experience niliyopitia ya mahusiano , I'm just not ready to repeat the same mistake again , by staying uchumba for the long years, I did it once, I have learned from it and will never do that ever again, aaaghhhhrrr ... Unless God says so to wait then will do it.. Anyway unaweza kusahau by doing hobbies unazozipenda.. Binafsi I used most of my time to volunteer , Church and be more close to my family .. ( These help to forget huyo ex ).. Sasa sijui wewe dear hobbies zako ni nini.. Ila naomba nikushauri next mahusiano mshirikishe sana Mungu and don't take too long kwenye uchumba because mnaweza kuchokana ..Halafu kwa mahusiano yako mapya usijaribu to compare between your Ex and your current hii italeta shida .. Nisikuchoshe.. Just take it easy and slow, put God first in everything on your next chapter.. Good luck.. Na pole sana . Thanks..
 
Kim2 Asante ndugu yangu. Kusema ukweli naona giza mbele yangu. Kazi ninayo inayoniwezesha kula na kufanya mambo mengine.
Imakuwaje mtu ambae umemsubilia muda wa miaka minne au mitano anakuja kukutenda bial huruma?

Inauma sana tena sana.. I feel you man. I remember that road.. But everything happens for the good reason .. Mshukuru Mungu...Give yourself a time to heal . Thanks..
 
Huwezi kupenda tena kwa dhati kama umetendwa,utajua ni wale wale

Its true.. But through the help of the Holly Spirit can heal us ( for those Christians ) . uzuri Mungu aliweka kusahau so that helps us a little bit .. Ukitendwa unaweza samehe but kusahau it takes a while , through pain we went through it always makes us stronger and wiser than before .. Thanks..
 
Mapenzi ni mtihani kwetu wengi,wapo wenye supp,carry mpaka nullified.Hio ni supplementary tu Kaka irudie ufaulu uendelee zaidi.Miaka yote hukumtia hata mimba mkuu?? Au ulikuwa humvui ile nguo ya mwisho??
 
Kaka asante sana kwa ushauri. Niseme tu kuwa huyu binti tulianza nae mahusiano tangu akiwa form six mwaka 2011. Mwaka 2012 hakupata chuo alikaa tu nyumbani nikawa nam support kwa kila kitu. ilipofika 2013 Mungu akasaidia akapata chuo cha kozi za afya ambacho nilimtafutia mwenyewe.
Kwahiyo makubaliano ilikuwa akimaliza chuo tu tuonane 2016 na kwamb? anapoianza semester ya mwisho awe amebeba mimba. Sasa ghafla ananiambia am not a decent girl for you. Naomba tuishie hapa sababu Nina mimba ya mtu mwingine na siwezi fanya lolote kwa sasa. Maumivu nilioyapata Nilihisi Duniani nimebaki peke yangu
 
Smart911 Mipango yangu yote inaelekea kuharibika...
Nianze upya mkuu ukizingatia umri haurudi nyuma?

Kwa nini uanze upya wakati umri ndiyo unakwenda. Anzia pale ulipoishia, endeleza kwa njia zilizo bora. Kuumizwa ni kitu cha kawaida sana.
 
Kaka asante sana kwa ushauri. Niseme tu kuwa huyu binti tulianza nae mahusiano tangu akiwa form six mwaka 2011. Mwaka 2012 hakupata chuo alikaa tu nyumbani nikawa nam support kwa kila kitu. ilipofika 2013 Mungu akasaidia akapata chuo cha kozi za afya ambacho nilimtafutia mwenyewe.
Kwahiyo makubaliano ilikuwa akimaliza chuo tu tuonane 2016 na kwamb? anapoianza semester ya mwisho awe amebeba mimba. Sasa ghafla ananiambia am not a decent girl for you. Naomba tuishie hapa sababu Nina mimba ya mtu mwingine na siwezi fanya lolote kwa sasa. Maumivu nilioyapata Nilihisi Duniani nimebaki peke yangu

Dah! Pole sana.Sasa ni wakati utulie kwanza ujiweke vizuri kisaikolojia.Muda utakufanya usahau yote.Dunia ina wanawake Wazuri na wabaya.Sio wote ni wabaya.Yupo atakakufanya useme "the past is over"
 
Back
Top Bottom