Inawezekana CAG alisema wabunge wa CCM pekee ndio dhaifu ila waupinzani sio dhaifu.....

hata kama CAG akiomba radhi kuli please bunge kwamba yaishe (maana ndicho wanachotaka) bado haitafuta ukweli halisi kwamba bunge letu awamu ya tano chini ya Ndugai ni DHAIFU!!!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Udhaifu CIO bunge pkee tatizo in yy mwenyewe SpikaNdugai anaendesha binge km Sacco's yke,mfn.Anglia mijadala mikali inapokuwa upinzani Salina nmkali anavyo ikanyagia n kuipitisha kipuuzipuuzi tu Cku y al' Mc kind cha mswl y pkwpo Pm ikipigwa swl la uhakika n gumu analiyeyusha kijngkjng

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote ni wadhaifu kuanzia Bunge, Assad na Ndugai wote ni wadhaifu tu,

Kama Ndugai au Bunge lisingekuwa dhaifu lingedeal na mambo strong tu na kuacha point dhaifu dhaifu, na au kutaka kujibu mapigo kwamba so dhaifu hapo ndo tunaona ni dhaifu kweli maana tujiulize kwa kina kama so dhaifu kwanini neno Dhaifu linasumbua kichwa cha viongozi wa Bunge?

Nakumbuka Mnyika aliwahi kusema kwamba Rais Kikwete ni Dhaifu, yaan mihimili inapaswa kuheshimiana lakin muimili serikali ulidharauliwa na kwakuwa Jakaya alipuuza neno lenyewe akaonekana strong,


Assad, udhaifu wake kuonekana ni pale ambapo kataja kuwa Bunge ni dhaifu Alafu akaendeleza Malumbano , ilibidi akae tu kimya na ikibidi angefichua yote yale ambayo tunajua na hajayaweka hadharani, hivo naye ni dhaifu

Britannica
 
Wewe ni kiazi kwa mujibu wa Pascal Mayalla. Umemsikia wapi CAG Prof. M.Assad akisema bunge ni dhaifu!?
Wote ni wadhaifu kuanzia Bunge, Assad na Ndugai wote ni wadhaifu tu,

Kama Ndugai au Bunge lisingekuwa dhaifu lingedeal na mambo strong tu na kuacha point dhaifu dhaifu, na au kutaka kujibu mapigo kwamba so dhaifu hapo ndo tunaona ni dhaifu kweli maana tujiulize kwa kina kama so dhaifu kwanini neno Dhaifu linasumbua kichwa cha viongozi wa Bunge?

Nakumbuka Mnyika aliwahi kusema kwamba Rais Kikwete ni Dhaifu, yaan mihimili inapaswa kuheshimiana lakin muimili serikali ulidharauliwa na kwakuwa Jakaya alipuuza neno lenyewe akaonekana strong,


Assad, udhaifu wake kuonekana ni pale ambapo kataja kuwa Bunge ni dhaifu Alafu akaendeleza Malumbano , ilibidi akae tu kimya na ikibidi angefichua yote yale ambayo tunajua na hajayaweka hadharani, hivo naye ni dhaifu

Britannica

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu kiko wazi hakuna haja ya maelezo mengi
tapatalk_1554543540573.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
YAZAMANI KIDOGO HII
Jana tu nilikutana na spika wangu akiwa katika foleni pale Ubungo. Mbele yake kulikuwa na gari linalopiga king’ora. Nikajua anawahi hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya upanuzi na ujenzi wa barabara ya njia nyingi ambazo zinatarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni kuanzia Kimara hadi Kibaha.

Nikatabasamu kumuona spika wangu katika suti maridadi. King’ora mbele yake. Maisha yanataka nini zaidi? Nikatabasamu tena. Nikamsubiri kwa hamu kumsikia akiongea kama miongoni mwa watoa hotuba pale Kimara, jana.

Kuna mambo niliyategemea. Kisaikolojia, mwanadamu anayepishwa barabarani, trafiki anavuta magari katika foleni yake ili yeye apite, nadhani vitu vingi vya kipinzani hawezi kuvipenda. Amezoea kupita katika barabara isiyopingwa, vipi aone mambo yanayopingwa?

Nilimsikia spika akieleza wazi kwamba pale mjengoni kwake watu wanaoitwa wapinzani wanapinga kila kitu. Inawezekana kabisa anasema kweli, lakini kuna wale wa upande mwingine ambao kila kitu wanasema ‘ndiyooo’. Hawa hakuwataja.

Hili ndilo tatizo langu la msingi. Kuna wanaosema ‘ndiyooo’ kwa kila kitu na wasemao ‘hapanaaa’ kwa kila kitu. Kwa nini spika alichagua kuwasema wanaosema hapana tu?

Hawa wanaosema ndiyo kwa kila kitu wamemchanganya hata namba moja wetu. Wakati mikataba ya ovyo ya madini ilipopelekwa mjengoni walisema ‘ndiyooo’ kwa kila kipengele. Wakati namba moja kaingia madarakani akapinga mikataba hiyo hiyo wakasema ‘ndiyooo’. Spika hawa hawaoni kama tatizo?

Kwa mfano, wanaosema hapana mpaka leo hawana nguvu ya kuamua pamoja na hiyo hapana yao. Wanaosema ‘ndiyooo’ wana nguvu ya kuamua. Leo namba moja wa nchi hii anatuambia kwamba nchi iliharibiwa sana, ni kweli, je iliharibiwa na wale waliokuwa wakisema ndiyo kwa kila kitu au hapana kwa kila kitu?

Ukijaribu kuusoma moyo wa namba moja nadhani kimyakimya anawachukia sana waliokuwa wakisema ‘ndiyooo’ kwa kila kitu hata katika mikataba ile ya madini.

Namba moja akifungua makabrasha mbalimbali ya nchi hii ni wazi kwamba anasononeshwa sana na wale wasema ‘ndiyooo’ hasa wa tawala zilizopita. Hawa wasema ‘hapana’ wanamsumbua kwa sasa lakini sio kiini cha matatizo aliyoyakuta katika utawala wake
Time will tell

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What is your weakness and your strength? Actually my weakness is to be very aggressive when some one trying to suppress my image publicly and my strength is to agree every bill as proposed even the law bill can be fake.
 
Hii vita ya Ndugai na CAG naona ina baraka zote muhimu kutoka kwa watu muhimu... Hapa CAG ndiye shujaa aliyeandaliwa

#istandwithCAG
 
Kwa taarifa Yako, Raisi ni sehemu ya Bunge. Hivyo bunge likiwa dhaifu basi na Serikali ni dhaifu. Kwa sababu ya Ego, Hii haiwezekani hata kidogo kua kweli.

CAG anapiga hesabu za Matumizi ya Serikali. Ripoti ile mnayooiita ya CAG sio yake binafsi bali ni ya Serikali. Ni mali halali ya Serikali peke yake.

Serikali yetu tukufu, inao uwezo wa kujitathmini au kutojitathmini kupitia Bunge lake tukufu.

CAG akikabidhi ripoti kwa spika tunaweza kuamua kuijadili au kuchagua kutoijadili. CAG hana cha kufanya.


One More...
CAG ndiye Dhaifu, CAG alikubali mbele ya Raisi kua Trilioni moja nukta tano hazijaibiwa popote na hakuthubutu kufafanua alichosema ndani ya ripoti yake mbele ya Raisi.

Akaenda zake kwenye media kunung'unika kua Bunge ni Dhaifu. Na hii inazidi kumfanya kua dhaifu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Alimjibu Rais kama alivyouliza, Rais aliuliza km 1.5 imeibiwa, CAG akajibu hakuna sehemu kwenye ripoti amesema zimeibiwa na hilo ndiyo jibu Sahihi, sasa km hela imetumika katika miradi iliyo nje ya bujeti na CAG ameyaonyesha hayo na bunge halijachukua hatua, basi huo ni udhaifu wa bunge Katika hilo jumbo.
 
Pumba.
Kwa taarifa Yako, Raisi ni sehemu ya Bunge. Hivyo bunge likiwa dhaifu basi na Serikali ni dhaifu. Kwa sababu ya Ego, Hii haiwezekani hata kidogo kua kweli.

CAG anapiga hesabu za Matumizi ya Serikali. Ripoti ile mnayooiita ya CAG sio yake binafsi bali ni ya Serikali. Ni mali halali ya Serikali peke yake.

Serikali yetu tukufu, inao uwezo wa kujitathmini au kutojitathmini kupitia Bunge lake tukufu.

CAG akikabidhi ripoti kwa spika tunaweza kuamua kuijadili au kuchagua kutoijadili. CAG hana cha kufanya.


One More...
CAG ndiye Dhaifu, CAG alikubali mbele ya Raisi kua Trilioni moja nukta tano hazijaibiwa popote na hakuthubutu kufafanua alichosema ndani ya ripoti yake mbele ya Raisi.

Akaenda zake kwenye media kunung'unika kua Bunge ni Dhaifu. Na hii inazidi kumfanya kua dhaifu.



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote ni wadhaifu kuanzia Bunge, Assad na Ndugai wote ni wadhaifu tu,

Kama Ndugai au Bunge lisingekuwa dhaifu lingedeal na mambo strong tu na kuacha point dhaifu dhaifu, na au kutaka kujibu mapigo kwamba so dhaifu hapo ndo tunaona ni dhaifu kweli maana tujiulize kwa kina kama so dhaifu kwanini neno Dhaifu linasumbua kichwa cha viongozi wa Bunge?

Nakumbuka Mnyika aliwahi kusema kwamba Rais Kikwete ni Dhaifu, yaan mihimili inapaswa kuheshimiana lakin muimili serikali ulidharauliwa na kwakuwa Jakaya alipuuza neno lenyewe akaonekana strong,


Assad, udhaifu wake kuonekana ni pale ambapo kataja kuwa Bunge ni dhaifu Alafu akaendeleza Malumbano , ilibidi akae tu kimya na ikibidi angefichua yote yale ambayo tunajua na hajayaweka hadharani, hivo naye ni dhaifu

Britannica
Mkuu, ukisema Prof. Assad ni Dhaifu. Haitaleta impact yoyote kwasababu yeye kama Mwanadamu ambaye kila mtu atakubali kua hakosi Madhaifu.

Ila ule upande mwingine wa Bunge ndio kuna show-down ya kufa Mtu. Maana ile ni taasisi Kubwa.

Na Ukisema wote (Assad na Bunge) ni wadhaif. Unapunguza uzito wa Udhaifu. Maana unagawa matokeo sare sare. Inakua kama unalenga kujenga maelewano badala ya kusema Ukweli Mchungu bila Hofu.

Wabunge wana hulka ya kulumbana
Kwao sio Udhaifu bali ni strength.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna lolote.
Umesema ya kuwa CAG hajafafanua huo udhaifu wa bunge, je akifafanua na ukaona kweli bunge ni dhaifu utamsafisha CAG kwa sabuni gani.
USILOLIJUA NI USIKU WA KIZA
Na Lusekelo Mwandemange.

Kwanza nianze kwa kuwapongeza wote waliotumia muda wao kutoa maoni na kujadili suala la Bunge kukataa kufanya kazi na CAG (Controller & Auditor General-Mthibiti na Mkaguzi mkuu wa serikali) kutokana na kauli yake tata aliyoitoa akiwa Marekani kwa kuita Bunge lina UDHAIFU.

Binafsi nimejiuliza maswali mengi kama wengine walivyo hoji. Kwanza nilijiuliza CAG ni nani hasa mpaka aite Bunge ni dhaifu hasa anapohojiwa kuhusiana na hoja za kigaguzi zinazopelekwa bungeni kutopatiwa majibu?. Je kuna kosa gani kwa yeye kuita Bunge ni dhaifu? Na je ni kweli Bunge ni dhaifu? Na kama ni dhaifu katika lipi? Na kwanini atamke hadharani wakati ana nafasi ya kukosoa ndani? Na kwa nini akatamke nje ya nchi na sio akiwa hapa Tanzania? Na je Bunge kukataa kufanya kazi na CAG ni sawa? Na madhara yake ni nini? Na kama sio kupitia CAG Bunge watasimamiaje serikali? Pia nikajiuliza Bunge na CAG nani mwenye mamlaka ya juu kuliko mwenzake na nani anawajibika kwa nani? Hakika maswali ni mengi lakini sina nia ya kujadili maswali yote haya. Niseme tu katika hili naamini Bunge na CAG wote wakosaji.

Katika kujijibu maswali nikaona nifanye tafakali juu ya CAG Vs Bunge hasa katika kuangalia msingi wa uwepo wao katika katiba ya Tanzania. Kwanza CAG ndio mthibiti na mkaguzi mkuu wa serikali na amepewa madaraka hayo kwa mujibu wa katiba ibara 143 na katiba imeainisha kazi zake kuwa143(2) a) kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka mfuko mkuu wa Hazina ya serikali matumizi yake yameidhinishwa na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 136 ya katiba hii na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe. Na ibara ya 136 (3) Fedha zilizomo katika mfuko mkuu wa hazina ya serikali hazitatolewa kutoka mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi hayo yawe yameidhinishwa na Mthibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na pia kwa sharti kwamba fedha hizo ziwe zimetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Na Bunge ni mhimili katika JMT. Kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63(2) Bunge limepewa madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali ya JMT na vyombo vyake vyote(akiwemo CAG) katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii.

CAG KAKOSEA NINI?

CAG kakosea kwanza kwa kutotambua wajibu wake wa kikatiba au makusudi. Kwa msingi wa Katiba ni wazi kwamba CAG amepewa wajibu mkubwa sana sio tu wa kukagua mahesabu lakini hasa KUDHIBITI. Na Bunge limepewa wajibu wa kusimamia na kushauri Serikali. CAG ndiye mdhibiti mkuu kutupia lawama Bunge na kuita Bunge dhaifu naona sio sawa ila kinyume chake ni sahihi? Kwa mujibu wa katiba CAG anatakiwa athibiti matumizi ya fedha ya serikali, kama kuna lolote halijaenda sawa kwenye eneo hilo haitoshi yeye kukagua na kuonyesha tu mapungufu bali anatakiwa athibiti hayo yasitokee. Ikiwa katiba inampa CAG wajibu wa kuthibiti fedha isitoke kwenye mfuko wa serikali bila kuanisha matumizi sahihi na kufuata sheria alafu CAG anatuandikia taarifa kwamba kuna fedha 1.5Trn hazionekani zilipo na yeye ndo mthibiti udhaifu hapo unakuwaje wa Bunge?

Sababu ya pili, CAG ni kukosa uungwana tu. Kwasababu hata katika mahusiano ya kawaida ukimtolea ndugu ama rafiki kauli ya maudhi kwake hata kama wewe hukumaanisha kama alivyoelewa yeye na ukaona nduguyo kachukia busara ya kawaida tu inatuongoza kuomba radhi yaishe. Sasa CAG ingetosha tu kutambua kwamba kauli yake imeudhi bunge(chombo cha wananchi) na kuomba samahani yakaisha lakini kuweka msimamo kwamba hajakosea inaweza kuwa kweli kisheria hakukosea lakini ustaarabu wa kawaida tu ingefaa aombe radhi na kusema tu jamani mimi sikumaanisha hivyo mlivyoelewa lakini kwakuwa ndugu zangu mmeudhika na kauli yangu basi naombeni radhi tufanye kazi tusonge mbele. Lakini kukataa kuomba radhi kunazua maswali magumu. CAG katumwa na nani? Anatumika? Anajiamini nini?

Sababu ya Tatu. CAG kutamka mapungufu ya Bunge hadharani tena nje ya nchi. Yeye CAG ana access na Bunge ameshindwa nini kushauri Bunge mapungufu ya Bunge. Tukubali tukatae nje ya mipaka ya Tanzania watu hawajui Ndugai wala Prof Asad bali wanajua Tanzania. Sasa hata kama tuna mapungufu yetu kama taifa na kwa yoyote Yule haifai kutangaza kwa ulimwengu. Na anadhurika sio mtu mmoja au sio Bunge ni sisi wote. Hivyo suala la kujenga utamaduni wa kusemana, kuonyana, kuelekezana na kukemeana ndani ni muhimu sana. Sifurahii mtanzania yeyote wakiwemo akina Lissu kusema mambo ya nchi yetu nje ya nchi. Kwasababu kuna haribu taswira ya Tanzania. Katika hili CAG kakosea tena sana.

Sababu ya Nne: CAG kakosea kutamka Bunge ni dhaifu jumla jumla. Yaani kusema Bunge ni dhaifu bila kusema katika lipi? Hivi ni kweli kwamba mambo yooote yanayo ainishwa na CAG bunge halifanyii kazi? Kama ni hivyo ingewezekana vipi hati chafu zikapungua. Mbona mambo mengi sana yaliyoibuliwa na CAG yanajadiliwa Bungeni na kufanyiwa kazi. Sasa kutamka kauli isiyo na maelezo kama hii hakika ina tatiza. Unapolenga kumkosoa mtu inafaa kumwambia umekosea katika lipi na kama ni udhaifu wa bunge ni katika lipi? Je kutunga sheria? Kushauri serikali? Kusimamia serikali? Au katika lipi?

Kwa maoni yangu haya ndio makosa ya CAG katika hili.

BUNGE LIMEKOSEA NINI?

Bunge Spika naye amekosea katika hili.

Sababu ya Kwanza; Kuita vyombo vya habari na kuutangazia ulimwengu gadhabu yake dhidi ya CAG. Kama nilivyosema CAG ni mtu muhimu kwenye nchi na amefanya mengi mazuri kutoa kauli hii moja ya maudhi isingekuwa lazima kwa spika kuja juu kiasi hicho. Tena sio sawa kwasababu tunajenga tension kwa wengine bila sababu. Hoja kwamba CAG aliongea kwenye vyombo vya habari akihojiwa nje hivyo ajibiwe kwa vyombo habari sio sahihi. Katika hili CAG kakosea lakini spika kakosea zaidi. Ingefaa tu kumuita na kumhoji pengine bila hata media na vitisho. Kuchukia sana huku kunaweza kuthibitisha kauli ya CAG kwasababu mara nyingi watu huchukia wanaposemwa ukweli. Kama Bunge mnajua sio dhaifu kwanini kuchukia sana mnapoitwa dhaifu?

Sababu ya pili: ni kukataa kufanya kazi na CAG. Sasa mkikataa kufanya kazi na CAG wakati mnajua CAG ameshawasilisha taarifa yake kwa Rais mnataka Rais apeleke wapi hiyo taarifa. Na je Rais akiwaletea mtamkatalia?. Je hamuoni kama mnamuweka pabaya ndugu Rais. Na kwa kasi ya kazi ya Rais Ndugu John Joseph Pombe Magufuri hastahili kufanyiwa haya na ninyi nyote Bunge na CAG. Nadhani Bunge ingefaa tu kutoa onyo kwa kuwa CAG ni mara yake ya kwanza kufanya kosa la namna hii. Na hata kama hakuwaomba radhi ingefaa tu kutoa onyo ili akirudia ndio mchukue hatua kama hii. Lakini ndugu Spika umechukua hatua kali sana kwa kosa la kwanza. Na adhabu hii inaleta sintofahamu kubwa sana. Mnamuweka Rais njia panda. Na mpaka hapa tulipofikia watanzania tunasubiri busara za Mhe Rais aamue hatima ya jambo lenyewe.

Hivyo nitoe wito kwa Bunge na CAG kulimaliza hili. Na njia ninazo ziona ni tatu. Mosi Bunge mbadilishe adhabu iwe onyo tu na mtangaze kufanya kazi na CAG ,Pili CAG uombe radhi kwa bunge na wabunge nafsi zao zitulie wafute adhabu, Tatu Rais atumie busara kulimaliza hili kwa kuwa anazo busara nyingi na uzoefu wa kutatua migogoro kama alivyofanya kwa suala la Kikokotoo, Suala la Korosho n.k

Tanzania ni yetu sote tuijenge na kuilinda.

Ahsanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja tena kwa sana
Umejaribu kuelezea kadri ya ufahamu wako, ila binafsi nakuona wewe ni mtanzania halisi ila una mapenzi mengi kwa upande wa Ndugai.
1. Kusema/kutumia neno dhaifu ni kawaida sana ktk ukaguzi.
2. Kutamkia nje ya nchi au ndani ya nchi haiondoi maana halisi ya neno lenyewe. Kwa maelezo ya CAG mwenyewe kuwa ameshasema sana udhaifu wa bunge ndani ya nchi, lakini uliona impact yoyote katika hilo?
3. Ndugai ana chuki binafsi na wasema kweli ambao hawapendi kujikomba komba kwa mtu.
4. Kuomba msamaha kwa mharifu ni sawa na kumpatia jambazi bastola akateke familia yako
5. Kama ingekuwepo sheria ya kumng'oa mara moja huyo Ndugai ningeomba ifanye kazi hapa. Maana anataka kutupeleka shimoni.
Usipende kujadili mada moja ukachanganya na wengine, unaweza kudharaulika au kupotezewa kile unachojadili ingawa kina faida.
Kama wewe upo upande wa Ndugai mimi nipo kwa CAG.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom