Inawahusu wote waliozaliwa...

pe.livinuu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Posts
502
Reaction score
114
Hivi hujawahi kukaa na kufikiria kidogo kuhusu wazazi wako?

Kila wanachokifanya kukuhusu wewe ni kwaajili yako.
Na hata kama kuna mahali wanakukosea au wanakosea bila kujua, kuna haja yoyote ya kuchukia au kuwa na kinyongo?!!
hakuna haja ya kuchukia au kuweka moyoni.
Cha muhimu ni kuweka mambo sawa, kuwaambia kwa uwazi nini unapendelea nini hupendi.
Kwasababu yote hayo wayafanyayo wanayafanya kwaajili ya kujitahidi uwe na amani na furaha na maisha mazuri.
Sikatai kuna wazazi wanatumia nguvu au ubabe au mamlaka waliyo nayo kuwakandamiza watoto wao, lakini wewe kama mwanawao unaweza kufanya kitu kurekebisha.. Hata ikibidi kushirikisha wana familia au ndugu wa ukoo kuhusu hilo. Pia kuna taasisi mbalimbali zinazo husiana jamii na mambo kama hayo zinazo weza kusaidia.
Kwahiyo wewe kama unajitambua unaelewa kabisa kila binadamu ameumbwa na MUNGU na kuwekwa hapa duniani kwa sababu Maalum.

Na kinacho takiwa kufanya ni Kuwaheshimu,kuwapenda na kuwatii wazazi/walezi wako, ili kumpendeza MUNGU.

Na sio wazazi tu au walezi,kila mtu ni vizuri kumheshimu na kuwa na amani naye.

** Hebu tulia na ufikirie kidogo kuhusu hilo.**

‪#‎NAWAPENDA‬ sana wazazi wangu, MUNGU awabariki..

[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=Nawapenda]#Nawapenda [/URL] pia marafiki na ndugu zangu, MUNGU awabariki.
Wote kwa pamoja nawatakia Maisha mema.
 
Kuna mwanasheria moja aliwahi kuniambia hakuna haki atakayokupa mzazi wako zaidi ya kukuzaa, mengine hayo hata aspokupa usimhukumu kama hana uwezo navyo, wewe shukuru mungu amekuleta kupitia wao, Hakkka pepo ipo chini ya nyayo za Wazazi wetu, by the way ujumbe wako mzuri
 

Ah kweli umegusa mahali muhimu sana..
Kuzaliwa tu ni zawadi kubwa sana kutoka kwa wazazi.
Hata kulelewa mpaka hapa nilipofikia au ulipo fikia ni kudhihirisha upendo wa wazazi kwetu.
 
Unasema hayo utadhani hakuna wazazi wanaowabaka watoto wao,au wanafanya hayo bahati mbaya?
Unasema hayo utadhani hakuna wazazi wanao walawiti watoto wao au hayo wanafanya kwa kutokujua?

Unasema hivyo utadhani hakuna wazazi wanaotupa watoto wao,au ni bahati mbaya?

Hivi unajua kumhudumia mtoto ni jukumu lamzazi wala hatakiwi kupewa asante wala hongera yoyote ile?
Uamue wewe kununua gari halafu utake likushukuru kwa kuliosha na kuliwekea mafuta wakati ulilinunua kwa raha zako?

Una hatari sana wewe

Wazazi ni watu wa kuheshimiwa lakini hizi sababu ni za hovyo sana!
 
Ah kweli umegusa mahali muhimu sana..
Kuzaliwa tu ni zawadi kubwa sana kutoka kwa wazazi.
Hata kulelewa mpaka hapa nilipofikia au ulipo fikia ni kudhihirisha upendo wa wazazi kwetu.

Hivi usingezaliwa ungokosa nini?

Kukulea ni jukumu la mzazi atake asitake
Wewe unaona ni hisani?

Kukupenda ni lazima wakupende,si wamekuleta wa raha zao?
Tena wakati wanapanga hayo wewe hawakukushirikisha halafu utake shukrani?
 

Huyo mwana sheria ni mjing.a sana
 
Hivi usingezaliwa ungokosa nini?

Kukulea ni jukumu la mzazi atake asitake
Wewe unaona ni hisani?

Kukupenda ni lazima wakupende,si wamekuleta wa raha zao?
Tena wakati wanapanga hayo wewe hawakukushirikisha halafu utake shukrani?

Ni wajibu na ni haki..
Lakini hujaona tu ile hisani ya kuchagua kukulea na kukupenda badala ya kukutupa au kufanya chochote kile kibaya.!!??.
Ni wajibu wangu na wako pia kuwashukuru wazazi au walezi kwa mema yote waliyo tutendea.
 

Hao walio lawiti au kubaka au kutupa watoto wao au hata ku wauwa ...
Hao wamejichukulia HUKUMU yao wenyewe.. Na SHITAKAlao watajibu kwa MUNGU..

Sasa Eiyer usifananishe kiumbe hai binadamu na kitu kisicho hai (gari)

Kama ni muungwana na unajali ni vyema kushukuru kwa jema lolote ulilo tendewa.
Na hongera au shukrani yako inampa moyo sana mzazi au huyo aliye kulea.
Anajua kwamba unaupendo kwake..

Watu wasiopenda wazazi/walezi wao huwa hawawapi shukrani zozote
 
Last edited by a moderator:
Hivi usingezaliwa ungokosa nini?

Kukulea ni jukumu la mzazi atake asitake
Wewe unaona ni hisani?

Kukupenda ni lazima wakupende,si wamekuleta wa raha zao?
Tena wakati wanapanga hayo wewe hawakukushirikisha halafu utake shukrani?

Hahaaaa tuseme wangekushirikisha ungekataa??
 
Kwanini nimshukuru mtu kutimiza wajibu wake?
 
Ni wajibu na ni haki..
Lakini hujaona tu ile hisani ya kuchagua kukulea na kukupenda badala ya kukutupa au kufanya chochote kile kibaya.!!??.
Ni wajibu wangu na wako pia kuwashukuru wazazi au walezi kwa mema yote waliyo tutendea.

Kuchagua kunilea ni hisani?

Unajua maana ya hisani wewe?

Hicho kibaya wangenifabnyia na wala isingekuwa kitu kwangu na wangeenda kujibu tu
Siwezi kumshukuru mtu kutimiza wajibu wake

Yaani wewe uwashwe umtongoze mwanamke na umtie mimba bila kuomba ushauri wowote ule halafu eti uje udai ushukuriwe kwa hicho ulichokifanya .....!!!!!!!!!!!

Khaaaaa!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…