Inawahusu wenye ndoa imara zenye furaha.

Inawahusu wenye ndoa imara zenye furaha.

Glenohumeral joint

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2017
Posts
2,054
Reaction score
2,917
Mm kama kijana wa kiume ambaye ntakuja kuoa miaka si mingi sana kuanzia sasa nawaasa wale wenye ndoa nzuri zenye furaha wawe wanakuja kutoa wosia na kushuhudia ndoa zao huku jf...

Nasema HV kwa sababu ,toka niingie jf na hasa jukwaa LA mahusiano nakutana na mada zilozogubikwa na migogoro sana hasa za wanaume kuwatuhumu wanawake,inafikia time najiuliza HV huku ndani hakuna wenye ndoa zenye furaha nao wakasema,kiukweli inatuvunja moyo sisi mabachela tunapoona mada mbaya tu za ndoa zenu,tunakata tamaa ya kuingia ktk ndoa maana kila mada ni za majanga matupu.....

Nmemaliza..
 
Hata mimi nipo kama wewe ngoja niwasitu na nipige tick hapo juu ili kila neno nilipate
 
Watu wanasemaga MATATIZO mkuu ili kupunguza hasira zao na wakati mwingine kupata msaada na ushauri. Sasa ukiwa na FURAHA unataka nini tena.
 
Mdogo wangu kaa ukijua changamoto kwenye ndoa hazikoseni.
Chamsingi ni kuvumiliana tu ila ikizidi na ukaona hii sasa imezidi hakuna budi kuachana kwa wema tu.
Jihadhari usije ukafikia kutoa uhai wa mtu kisa mapenzi wakati unawezankupata mwingine.
Kwakifupi ndoa zote zina matatizo yake ila wengi inabaki ni siri ya wanandoa tu.
 
Wewe hutakiwi kujifunza kwa mwenzako swala la mahusiano kwasababu moja kuu watu wanatofautiana kitabia na namna watu wanavyochukulia vitu sasa utaiga mpaka hulka za watu, cha msingi wewe anza safari tu, wewe pekee ndiyo mtu mwenye nafasi kubwa kuifanya ndoa yako kuwa bora au kutokua bora ila sio kuiga
 
Nadhani Hakuna ndoa yeye furaha siku zote bali kuvumiliana tu panapotokea tatizo
Hilo nalijua kabisa mkuu,vikombe viwili vikikaa pamoja hugongana stms,lkn migogoro inayoletwa huku sio ya kawaida...yaan balagumu kabisa....kwann
 
Watu wanasemaga MATATIZO mkuu ili kupunguza hasira zao na wakati mwingine kupata msaada na ushauri. Sasa ukiwa na FURAHA unataka nini tena.
Ukiwa na furaha unakuwa chanzo cha kuwasaidia wengne kuipata furaha kama yako....MTU anapokuwa anaona matatzo ya watu kila siku huijengea akili yake kuhis dunia n matatizo matupu....
 
Wanaume wa siku hizi ni walalamishi sana
Nakushauri ujifunze kwa baba yako zaidi kuliko vijana wenzio wa kiume wa ilimwengu huu,jiulize babako aliwezaje?
Sawasawa .....inabid wanaume tupunguze kulialia kindezi
 
Mdogo wangu kaa ukijua changamoto kwenye ndoa hazikoseni.
Chamsingi ni kuvumiliana tu ila ikizidi na ukaona hii sasa imezidi hakuna budi kuachana kwa wema tu.
Jihadhari usije ukafikia kutoa uhai wa mtu kisa mapenzi wakati unawezankupata mwingine.
Kwakifupi ndoa zote zina matatizo yake ila wengi inabaki ni siri ya wanandoa tu.
Duuuh..hatari sana.....kuna time nawaza kwamba hii furaha niliyonayo itaisha tu nitakapooa ...maana sio kwa vilio ninavyoona huku
 
Wewe hutakiwi kujifunza kwa mwenzako swala la mahusiano kwasababu moja kuu watu wanatofautiana kitabia na namna watu wanavyochukulia vitu sasa utaiga mpaka hulka za watu, cha msingi wewe anza safari tu, wewe pekee ndiyo mtu mwenye nafasi kubwa kuifanya ndoa yako kuwa bora au kutokua bora ila sio kuiga
Sawa mkuu...mm simaanishi kuiga bali namaanisha kujifunza....elimu ya kuimarisha ndoa kwa mifano iliyo dhahiri n muhimu japo msimamo wa MTU binafsi ktk kile anachofundishwa n muhimu pia....asante mkuu
 
Wala usiingie kwenye ndoa na mentality kwamba ni ngumu ama huwa hazidumu, na katu usiingie kwenye ndoa kwa kujifananisha na wengine na kuhofia kuwa kama wao.

Ingia kwenye ndoa ukijua unaingia na binadamu mwenzio ambae hajakamilika kama wewe ambavyo una mapungufu ya kwako. Kuishi pamoja kutadhihirisha tabia ambazo huenda zisikufurahishe but have the patience to understand hamkulelewa pamoja so lazima mtofautiane.

Ndoa is a beautiful thing jamani. Having someone to call your own for the rest of your life is something. That feeling when you are lying next to the one you love.... Or the gentle snores.... Or when he finally becomes a Dad and you a Mom acha kabisa.

Fights will be there. Some will be quite bad and will leave you disraught.... but where love leads, both hearts will always find a way home.

Mumtangulize Mungu na mu apply mafundisho muliyopewa ya kidini.

Anything else is simple common sense.
 
Ndoa ni necessary,very important and mandatory devil
 
Back
Top Bottom