Inawahusu Wabunge Wote!.

Inawahusu Wabunge Wote!.

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,200
Reaction score
7,568
Ni kuhusuMapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya (TISS ACT, 1996)

-Ni nani mteja wa serikali na vyombo vyake vyote?
-Ni nini Maana ya Usalama?
-Je wananchi wanaona/wanapata walicho tarajia?
Kimsingi; Mteja (ambaye vyombo vyote huwajibika kuhakikisha vina mridhisha) katika nchi ya ki demokrasia ni Mwananchi. Kwa mfano; Katika katiba ya Tanzania 8 (i) a-c. Inaliweka wazi jambo hili ;Hivyo basi ni jukumu la serikali kuunda vyombo ambavyo vinafanya kazi na kuleta matokeo yale yanayo tarajiwa na wananchi.

Tunaposema Usalama wa Taifa,Kwa haraka wananchi wanaelewa kwamba ni kitengo ambacho ndicho chenye uwezo wa juu kabisa kuhakikisha kwamba nchi iko salama na hakuna mtu yeyote anayeweza kuwadhuru.Katika hali ya uwepo wa Usalama wa Taifa; wananchi hutegemea kuona wakifanya shughuli zao bila wasiwasi wowote ule na bila kudhuriwa na yeyote kwa namna yeyote na kama wakiwa wanadhuriwa au kuishi kwa wasiwasi wajue ni kwa nini, Nani anawadhuru, na kwa nini hakuchukuliwa hatua . Katika hali hiyo ndio maana unaona wananchi wanapopata dhahama inayo sababishwa na wahalifu wakubwa mf. Milipuko, wizi mkubwa, madawaya kulevya, ufisadi, migogoro ya kisiasa n.k Huanza kutaja Usalama wa Taifa.


Swali sasa ni ikiwa wananchi wanapata kilewa nachokitaraji pamoja na kuwepo kwa idara hii? Jibu ni hapana.Hapana kwa sababu wananchi wanalalamikia madawa ya kulevya, uhalifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa vyombo vya usalama vyenyewe, Ujangili, Ufichaji fedha nje yanchi, wananchi Kuuawa kwa makusudi n.k.


Tatizo liko wapi? Tatizo lipo kwenye Sheriaya Uundaji Wa idara hii (TISS Act-1996). Matatizo ya msingi yapo kwenye Muundo na majukumu ya kisheria ya Taasisi ambayo hayakidhi dhamira ya waundaji wenyewe (Wananchi na viongozi waliowachagua). Kwa mfano; Idara imepewa majukumu ya Kuchunguza, Kuchambua taarifa na Kushauri,Sasa cha kujiuliza ni kwa nini Isiitwe " Idara ya Ushauri?", na Kinyume Chake iitwe "Idara ya Usalama? Hapo ndipo tatizo la msingi linapoanzia. Inaonekana dhamira ya watunga sheria na kile walichokifanya vilikuwa ni vitu viwili tofauti na ndio maana hata leo hii matokeo huja tofauti na matarajio ya walio wengi. Kwa mfano; Tanzania kama nchi nyengine; Tuna walinzi wa Rais, na viongozi wengine wa juu. Je? wanao walinda wanatumia sheria hii hii ya (TISS Act-1996)?Kama ndivyo ; sheria hiyo hairuhusu kutumia nguvu kwa namna yeyote bali kushauri tu, je! Kwa mujibu wa sheria hii inawaweka viongozi Wetu salama kweli!; au ili wawe salama wakati Fulani inaweza ikabidi kuvunja sheria?

NINI CHA KUFANYA
SHERIA HII IRUDISHWE BUNGENI NA KUFANYIWAMABADILIKO YAFUATAYO.​

1. MABADILIKO KATIKA MAJUKUMU YA IDARA

[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]WAHUSIKA
[/TD]
[TD]NINI KIBADILIKE
[/TD]
[TD]FAIDA
[/TD]
[TD]HASARA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 81, bgcolor: transparent"]BUNGE
[/TD]
[TD="width: 178, bgcolor: transparent"]Majukumu ya idara yabadilishwe kidogo ili kulingana na matarajio ya wananchi na jina la Idara lenyewe.Badala ya kutafiti, kuchambua na kushauri tu; Mkurugenzi mkuu aruhusiwe Kutoa taarifa kwa wananchi "Whistle Blowing" Ikiwa ushauri uliotolewa hautafanyiwa kazi na wanaotakiwa waufanyie na hali hiyo inahatarisha usalama wa nchi.



[/TD]
[TD="width: 194, bgcolor: transparent"]-Itawafanya viongozi kulazimika kushughulikia masuala yote yanayo hatarisha usalama wa nchi bila kujali kama yana athiri hali yao kisiasa au la kwa kuwa watajua wakiacha wataumbuka.


-Itawasaida wananchi kujua adui yao ni nani hasa ikiwa serikali itaambiwa adui na isichukue hatua yeyote


-Itasaidia kuepusha kesi kama hizi za viongozi kusema wana majina ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya lakini wanawalea.
[/TD]
[TD="width: 106, bgcolor: transparent"]HAKUNA.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 81, bgcolor: transparent"]BUNGE
[/TD]
[TD="width: 178, bgcolor: transparent"]Kitengo cha ulinzi wa viongozi kiundiwe sheria yake peke yake, kwa sababu kama inayo tegemewa ni hii ya (TISS Act 1996) ya kutafiti na kushauri, kuna siku inaweza ikasababisha majanga.
[/TD]
[TD="width: 194, bgcolor: transparent"]Kazi za walinzi wa viongozi wetu zitakuwa zimewekwa na zinafahamika kisheria na hivyo viongozi wetu watakuwa salama zaidi, Kuliko kama walinzi wa viongozi wataendelea kulindwa na sheria ya kutafiti na kushauri.(Kama kuna sheria nyengine naomba kufahamishwa).
[/TD]
[TD="width: 106, bgcolor: transparent"]HAKUNA
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

2 . MABADILIKOKATIKA MUUNDO
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]WAHUSIKA
[/TD]
[TD]NINI KIBADILIKE
[/TD]
[TD]FAIDA
[/TD]
[TD]HASARA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 81, bgcolor: transparent"]BUNGE
[/TD]
[TD="width: 178, bgcolor: transparent"]-Mkurugenzi ateuliwe na Rais lakini lazma Aidhinishwe na Bunge.
[/TD]
[TD="width: 205, bgcolor: transparent"]-Itaepusha uwezekano wa Rais kuteua rafiki yake asiye na uwezo au asiye muadilifu.
[/TD]
[TD="width: 95, bgcolor: transparent"]HAKUNA.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 81, bgcolor: transparent"]


[/TD]
[TD="width: 178, bgcolor: transparent"]-Mkurugenzi awe anawajibika kwenye kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama na si Kwa rais wala waziri
[/TD]
[TD="width: 205, bgcolor: transparent"]-Hii itasaidia Idara hii kutotumika kwa Masilahi ya vyama vya siasa na mwanasiasa mmoja mmoja bali kwa maslahi ya Umma.
[/TD]
[TD="width: 95, bgcolor: transparent"]HAKUNA
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
3. MABADILIKO KATIKA KUAJIRI.
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]WAHUSIKA
[/TD]
[TD]
NINI KIBADILIKE​
[/TD]
[TD]FAIDA
[/TD]
[TD]HASARA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 81, bgcolor: transparent"]VIONGOZI WA IDARA
[/TD]
[TD="width: 160, bgcolor: transparent"]-Waajiriwe watu kutokana na sifa zao na sifa za msingi ziwe zinaainishwa wazi
[/TD]
[TD="width: 156, bgcolor: transparent"]-Itatusaidia kupata watu wenye weledi mkubwa sana, tabia na sifa stahiki wanaoweza kukabiliana na ulimwengu unaobadilika Kila kukicha.
[/TD]
[TD="width: 182, bgcolor: transparent"]Baadhi ya mambo yanaweza kuwa wazi ila si shida sana kwa sababu hata katika idara kama hizi za nchi nyengine, kuna baadhi ya vitu vinavyofahamika na wala havijawahi kuleta matatizo. Mfano CIA hutoa Jarida kila mwaka.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 81, bgcolor: transparent"]VIONGOZI WA IDARA
[/TD]
[TD="width: 160, bgcolor: transparent"]-Kazi ziwe zinatangazwa ila wanaoomba iwe ni siri, usaili ufanyike kwa siri, na wanaopata iendelee kuwa siri.
[/TD]
[TD="width: 156, bgcolor: transparent"]-Hii itasaidi kupatikana watumishi wa Idara wenye uwezo madhubuti lakini wasijulikane wazi ni akina nani.
[/TD]
[TD="width: 182, bgcolor: transparent"]Baadhi huweza kusema walichokiona au kuulizwa kwenye usaili ila hili linaweza kuthibitiwa kama linavyodhibitiwa sasa.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ndugu zangu na wahakikishieni kwamba kama Bunge likifanya mabadiliko haya katika sheria ya (TISS Act-1996) Nchi yetu itakuwa salama zaidi na hizi changamoto za ki usalama zinazo tukabili kwa sasa zita pungua.Tujiulizeni kwa nini kila siku tunasikia wadhamini wa madawa ya kulevya ni watu wa kubwa na wanafahamika lakini hawa chukuliwi hatua na hatupati taatifa ni nani na nani toka kwenye vyombo rasmi ili tukajua adui yetu ni nani hasa ukizingatia kama serikali imeshindwa kumshughulikia? Kwa ninit unasikia watu wameiba hela na kuficha nje ya nchi na hatuoni waki shughulikiwa wala hatu pati taarifa kutoka kwenye vyombo rasmi kwamba ni nani huyo kaamua kutuibia na serikali imeshindwa kumshughulikia? Kwa nini tunaona watu wanalipuliwa na mabomu; mara tunasikia eti ni mambo ya siasa na wahusika hawawekwi wazi na vyombo rasmi? Nina uhakika kama mabadiliko hayo hapo juu yakifanyika, kwa kiasi Fulani tutakuwa tukipata suluhu ya mambo haya.(Ni ushauri tu lakini).

Naomba Mbunge mmoja apeleke wazo hili la mabadiliko ya sheria hii Bungeni ili kwa pamoja tuchangie katika kuipeleka nchi yetu katika hali bora zaidi. Mwenye mawazo zaidi anaweza kuongezea au kukosoa.
Cc; Masanilo Wile GAMBA Tetty Bramo et.al
 
Last edited by a moderator:
Wakuu mbona hamchangii hapa? Au haya ndio yale mambo yasiyopaswa kujadiliwa na yanatakiwa yafanyike kwa siri san'a?.
Tehe! Tehe! Tehe!
 
wengine bado tumelala
Haya; mkiamka mje mchangie huku.Sio tu kila siku mnalalamika kwamba hali ya usalama katika nchi hii imekuwa tete, Mara mbunge fulani au waziri anahusika na madawa ya kulevya lakini chanzo ni barua kutoka gerezani Hong kong, mara........! mara.....! halafu kwenye kutafuta ufumbuzi Kimyaaaa.....!
 
Ni idea nzuri,inayocontradict lakini...Utafiti unafanyika,ila implementation yake ni sifuri kwa maana ushauri haufanyiwi kazi...Nadhani vyovyote hii idara ingeundwa kama wanasiasa hawataingilia utendaji wake kila kitu kitakuwa sawa. Leo ataongea nini bwana Mkubwa ikiwa naye uteuzi wake ni wa kimagumashi,Kurugenzi za mikoa na wilaya ni za kirafiki..ndiyo maana hata walio kwenye vikosi kazi wanakosa support kutokana na wigo wa majukumu...
 
Labda Mzee Judge Warioba ataliona /kulisoma bandiko lako la maana sana.

pia kiongezwe kipengele cha kuwachukulia hatua hao TISS wasipo timiza majukumu yao ya kuhakikisha usalama wa nchi ingawaje neno usalama wa nchi lina mnganganyiko kidogo ; wengine wanaweza sema usalama ni jukumu la wote, au la jeshi la polisi au JWTZ.

Ziwekwe pia taratibu za kuwafukuza kazi maana sio wote walio waaminifu katika kazi zao; hakuna kazi ya maisha au mpaka kustaafu na kulindana lindana kiujanja ujanja...

Majukumu ya TISS yaainishwe na yawekwe wazi maana sio siri ili kila mtu ayajue asije akaja sema alikuwa anachunguzwa kwa set up / kubambikiwa kesi...

Pia namna ya kuwapata ijulikane kama watatoka JKT, polisi au JWTZ au uraiani...

Ni hayo mkuu
 
Huku noma na pia amesema inawahusu wabunge sasa sisi sio wabunge....

Kwakuwa wengi wanataka ichangiwe ....Mi naunga mkono hoja maana kuna matatizo mengi kwenye hii Idara
 
huu ni uchambuzi uliotukuka mkuu big up kwako.
 
Ni idea nzuri,inayocontradict lakini...
Utafiti unafanyika,ila implementation yake ni sifuri kwa maana ushauri haufanyiwi kazi...
Sasa mkuu ndio tunatakiwa tutafute mbinu ambayo itafanya taarifa zilizotafitiwa na kufanyiwa kazi juu ya masuala ya usalama ziwe zinafanyiwa kazi, na kusiwe na mtu mmoja au kundi la watu wenye maslahi fulani ambao ndio wenye mamlaka na hiari ya kufanyia kazi au kutofanyia kazi.Tusipotafuta na kupata suluhu ya jambo hili tutakuwa tukiendelea kuona matukio ya kushangaza ya hapa na pale na tutaendelea kushangaa tu kila kukicha. Hata hivyo ifahamike kwamba inapotokea watu wakawa wanatekeleza mambo yasiyo na utafiti na kuyaacha yale yenye utafiti kwa vyovyote vile mafanikio yatakuwa madogo sana kwa ujumla wake.
Nadhani vyovyote hii idara ingeundwa kama wanasiasa hawataingilia utendaji wake kila kitu kitakuwa sawa.
Sasa ndio tunatakiwa tufikirie mbinu ambayo inaweza kusaidia wanasiasa wasiwe na uwezo wa kuingilia taarifa zilizotafitiwa kwa maslahi binafsi.Ni mimi na wewe sasa.Kila mtu akidhani si jukumu lake hatimae kila mtu ataacha na mwishowe tutakuwa tunazunguka kwenye "Problem Circle"
 
Haya niliyaeleza kwenye tume ya katiba. Tatizo ni historia ya Tanzania, mifumo hii ipo ya namna mbili. Ule wa kikomunisti na ule wa kimagharibi, sasa sera zimejichanganya. Ndio maana bado CCM in nguvu sana kutumia chombo hiki, maana ile ya kikomunisti inaripoti kwa chama. Swala sio Act tu, hata sera mbalimbali ni mbovu au hazipo. Uwigo wenyewe hata haueleweki. Ndio maana kuna Takakuru, Financial inteligence Unit NK. Je hizi sio department za hii idara? Naona kama mambo yetu ni hovyo hovyo kama kwanye soka.

Katika nchi nyingine hawa jamaa hufanya kazi mpaka na magazeti. Mfano mwanahalisi ilivyoandika ile ripoti ya kingolewa meno. Basi bunge lingedaka hii issue kwa manafaa ya umma. akina Raisi Nixin wa Marekani walilipuliwa na idara hii, mpaka akajiudhuru.

Kuna mengi, ila kiburi chetu ndio kaburi letu.
 
pia kiongezwe kipengele cha kuwachukulia hatua hao TISS wasipo timiza majukumu yao ya kuhakikisha usalama wa nchi
Mkuu hapa ndipo tatizo la msingi linalohitaji ufumbuzi lilipo. Kimuundo na kisheria,TISS, hawana uwezo wa kuhakikisha usalama wa nchi unakuwepo.Kwa hiyo kwa hili wala hawapaswi kulaumiwa si kosa lao, ni kosa la kimuundo na kisheria.
hakuna kazi ya maisha au mpaka kustaafu na kulindana lindana kiujanja ujanja...
Kama watumishi wa tasisi fulani wanapatikana kwa mazingira yasiyoeleweka, ni jambo la kulegemewa sana watu kuingia kwa michongo, kulindana kikubwa, kubebana kistaili n.k. Na ndio maana unaweza kukuta Baba ni Polisi, Mke ni Usalama na watoto wao wawili ni usalama halafu wanapita mtaani wanajitapa.Hapo kuna jambo tunatakiwa tulitafakari sana! na ndio maana tunazungumzia kwamba bunge lirekebisha kipengele cha jinsi ya ku ajiri.
Majukumu ya TISS yaainishwe na yawekwe wazi maana sio siri ili kila mtu ayajue asije akaja sema alikuwa anachunguzwa kwa set up / kubambikiwa kesi...
Kimsingi yako wazi kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu lakini kutokana na mianya ya kisheria iliyoachwa na sheria hiyo, na mazoea yaliyobakia toka kipindi ambapo chombo hicho kikiendeshwa bila muongozo wa kisheria (ambapo majukumu yake hayakuwa na mipaka na sana sana ilikuwa ni kuwazima wapinzani) ndio maana unakuta wakati fulani wana diverge kenye majukumu ya kisheria na kufanya mambo mengine ya kutatanisha.
 
Vijana wetu baada ya kumaliza mafunzo ya awali ya jeshi wanapelekwa Ngerengere kwa mafunzo zaidi ya ukomandoo na baada ya kuhitimu wanavua gwanda wanavaa nguo za kijani...ndio hawa hawa wanaorecruit so called green guard na kutekeleza mission za kipuuzi kwa maslahi ya wanasiasa nasi tusiojua upande wa pili wa shilingi tunaishia kuwalalamikia TISS CID's nand likely...
 
Kweli hii inawahusu wabunge wote

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mimi nadhani kwa sehemu kubwa watumishi wa hii Idara wangetokana na jeshi,au huko jkt vijana wanapoenda mafunzo, hata suala la kujiendeleza kielimu kwa watakaochaguliwa liwe jukumu la TISS,nima maana baada ya kuchaguliwa toka JKT gharama za elimu ya juu ziwe za TISS na hapo mwanafunzi ajue kabisa tayari yupo kwenye ajira japo yupo chuo,ajue hivyo na iwe siri yake.....kuhusu mkurugenzi wa hii idara kuteuliwa na rais kisha bunge kumuidhinisha hii imekaa vizuri,japo kwa wabungecwa CCM tulio nao leo sidhani kama wanaweza kumpinga mtu aliyeteuliwa na M/kiti wao hata kama awe na kashfa.
 
Vijana wetu baada ya kumaliza mafunzo ya awali ya jeshi wanapelekwa Ngerengere kwa mafunzo zaidi ya ukomandoo na baada ya kuhitimu wanavua gwanda wanavaa nguo za kijani...ndio hawa hawa wanaorecruit so called green guard na kutekeleza mission za kipuuzi kwa maslahi ya wanasiasa nasi tusiojua upande wa pili wa shilingi tunaishia kuwalalamikia TISS CID's nand likely...
Sasa pengine mkuu utusaidie kitu kama unaweza kuwa na idea.Kama ulivyojaribu kuelezea wazo la green guard, Sasa tukirudi kwa TISS, kwa kuwa recruitment hufanyika kwa siri, wanaofanya ni watu wa siri,standards zinazotumika ni siri, na matendo yao pia ni siri,.Kwa upande mwengine Mkurugenzi huchaguliwa na Rais, Rais ambaye anakuwa ni kiongozi mwanddamizi wa chama, ambaye miongoni mwa majukumu mengine ni kuhakikisha chama kinabaki madarakani kwa jinsi iwezekanavyo; Je! ni ki vipi tunaweza kujiamisha kwama wanaoajiriwa humo sio miongoni mwa ma kada watiifu wa chama? (Nani aulize na kila kitu ni siri isiyotakiwa kuhoji!).Katika mazingira ya namna hiyo, tutegemee kwamba watu hawa watakuwa wanaavitizamaje vyama vya upinzani na watu wenye fikra tofauti kisiasa? Katika mazingira haya tutegemee kweli kwamba watu hawa wataishishia katika mipaka iliyowekwa na sheria ya 1996?
 
Mimi nadhani kwa sehemu kubwa watumishi wa hii Idara wangetokana na jeshi,au huko jkt vijana wanapoenda mafunzo,
Hii inaweza kuwa sawa tu lakini sasa sheria ieleze wazi.Sio kusubiri busara za rais anayekuwepo madarakani kwa wakati.Hata hivyo katika hili, wakati fulani anaweza akawa anahitajika mtu ambaye ana fani ambayo haiwezi kupatikana huko jkt. Kwa hiyo hapo napo ina bidi pawe clear lakini kwa ujumla cha msingi ni kuwepo sheria madhubuti na zinazoeleweka ambazo hazitaacha ma gape.
 
Ninakupongeza kwa ushauri mzuri wa kuboresha idara nyeti ya Usalama wa Taifa ila kuna jambo lingine dogo tu nataka kuongeza.Nashauri aidha Wabunge wetu au Tume ya Katiba Mpya wafikirie wazo la kuanzishwa kwa mashirika binafsi ya kishushushu ili kupanua wigo zaidi wa mambo ya kiusalama hapa Nchini.
FAIDA
Kwa kuwa yatakuwa yanajitegemea yenyewe kwa kila kitu na hayatakuwa chini ya ushawishi wa Serikali iliyoko madarakani nina uhakika yatasaidia kuongeza uwajibikaji na uaminifu miongoni mwa watendaji wa Serikali kwa kuhofia kumulikwa na madarubini haya yaliyoko kila sehemu.Pia mashirika binafsi ya kishushushu yatasaidia kukuza usahihi wa taarifa za kiintelijensia zinazopatikana kwavile zitafanyiwa kazi na taasisi zaidi ya moja.
HASARA
Taasisi binafsi wakati mwingine zinaweza kutumika vibaya kwa malengo ya kisiasa na baadhi ya watu,makundi au vyama vya siasa.
USHAURI
Zitungwe sheria maalum zitakazo hakikisha hizi Taasisi zinafanya kazi zake kwa kufuata maadili,taratibu na kanuni za shughuli za kiusalama.
 
Nionavyo TISS inatakiwa iwe ni idara huru ambayo uteuzi wa viongozi utafanywa na kamati maalumu itakayoundwa na wabunge,Maofisa wa vyombo vingine vya ulinzi wa nchi labda ya kada nyingine kama itaonekana inafaa..
TISS kiwe chombo chenye mamlaka kamili ya kufanya utafiti,kushauri,kuimplement Tna kuchukua action inapobidi..
UWT usifanye kazi kwa kuangalia nafasi ya mtu as long shughuli zake hazitoki nje ya miiko ya kazi..
Nafasi za kujiunga ziwe wazi kwa kuzingatia vigezo vinavyotakiwa ila usahili,walioomba,waliopata,namna ya mafunzo na ethics zibaki under cover.
 
Back
Top Bottom