Inatia moyo sana kuona wanandoa wa muda mrefu bado wanapendana

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Unapokutana na COUPLE yenye miaka takribani 10 wakiwa wanapendana kama wameoana jana, wakitaniana na kucheka pamoja, wakikusimulia kuhusu utamu wa ndoa na jinsi walivyokutana mpaka walipoamua KWA HIARI YAO WOTE WAWILI kwamba they are a perfect match na
wanaweza kulisongesha gurudumu la maisha kwa pamoja.

Inatia moyo, hata kama ulikuwa na moyo mgumu kama Farao, unajikuta unalainika na kutamani kuanza kusaka Mshenga.

INASIKITISHA SANA:
Unapoona Vijana ambao wamekaa pamoja katika
Urafiki na Uchumba kwa Miaka 9 na Mwanaume
'kadinda' kwa sababu anahisi MATCHING CONCEPT
ya Mke na Mme inamiss halafu Bishosti anahisi
'Anapotezewa Muda', na amechoka kusimamia
Send-Off za Wenziwe,akaamua kufanya 'Mchakato wa Kurasimisha Rasimu ya Ndoa kwa kutumia Mimba' kwa Mfumo wa TMU(Tegesha Mimba Uolewe) na kwa presha jamaa akaamua kukuoa

Kweli ili kuiwahi Mimba mtoto azaliwe ndani japo alipatikana nje Maisha ya COUPLE hizi 2 ni tofauti kama usingizi na kifo, na ushauri utakaopewa kutoka kwa COUPLE hizi 2 ni CONTRADICTORY! Hawa wako
EDENI wanachuma matunda, na hawa wengine wako BOKO HARAM CAMP.

Acha penzi likue lizae ndoa automatic, usivundike penzi kabla halijaiva, maembe ya kuvundika huwa si matamu kama yale yaliyoiva yenyewe yakaanguka chini kama VIBWADE.

Acha penzi lizae ndoa nikiona mimba Inazaa ndoa najisikia KUTETEMEKA mpaka nanena kwa lugha, Ohhhh rikabababaataratabakasayahatat
arabarohobositaKANTANGAZEshant ahaymasethkatisharohobosikah

-stunter-
 
Kama unaona sikufai kwanini usiniache mapema? Mimi nimeona unanifaa na madhaifu yako yote ndo mana sitafuti mwingine, nikikutegeshea mimba ukiikataa tu inahamia kwako
 
Kama unaona sikufai kwanini usiniache mapema? Mimi nimeona unanifaa na madhaifu yako yote ndo mana sitafuti mwingine, nikikutegeshea mimba ukiikataa tu inahamia kwako
Mmmmh... Wewe hutokei kigoma lakini?
 
kwa kawaida unaweza ukadumu kwenye uhusiano 'fake' kwa miaka mingi sn. linapo kuja suala la kuo ama kuolewa mwenzako anaona hufikii viwango lkn hakuambii.

anataka aendelee kula tunda (hasa wanaume) ama kufaidi huduma (hasa kwa wanawake). wakati hayo yakijiri anagegeda/anagegedwa na mwingine huku akifanya tathmini ya viwango.

ikitokea viwango vya huyu mpya vikawa juu ndiyo pale mpenzi anakutosa, vikiwa chini ataenda kwa mwingine wa tatu apate tulizo la moyo wake. mapenzi ni sheeeda!
 
Aisee, bora Moyo ubaki kufanya kazi yake tu..
Mapenzi kizunguzungu hatuyawezi waswahili
 
Kudumu kwenye mapenz kwa muda mref haijamaanisha ni upando bali wengi huwa hawapendi kusema ukweli kwa kuhifia kuachwa na wenza wao, kwa mfano ME anaweza kukaa kwenye uhusiano na KE kwa miaka mingi huku akimdanganya atamuoa ingawa yy anafahamu fika huyo KE hana vigezo vya kuwa mke wake ila anajua akimwambia tu atapigwa chini the same pia kwa wadada unakuta anajingiz kwenye uhusiano ambayo bado hawajakubaliana kuoana yy anategesha mimba kwa makusudi ili aolewe wanasahau siku hz mimba haziogopwi tena hata umwambie nina mimba ya mapacha ME atakwambia sina mpango wa kuoa kwa sasa
 
16230049_242557736154770_5994855333883805696_n.jpg
 
Cha muhimu usifikirie ile furaha ulioiona wanayo hao wanandoa ni ya kudumu,unaweza kuta inatokea mara moja kwa miezi 2.Ndoa ni uvumilivu wa hali ya juu,we kurupuka bila ya kumshirikisha Mungu cha moto utakiona.
 
Back
Top Bottom