Inasikitisha sana editing ya pampass

carmercy

Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
91
Reaction score
33
Nimesikitishwa sana na tukio hili la kuedit pampass na kuweka picha ya Mh Lowassa akiwa amevaa pampass.

Mimi si shabiki wa Lowassa lakini napenda kuheshimu utu wa mtu haijalisha kwako hana thaman.

Huyu ni baba mwenye watoto wakubwa na mke pengine na wajukuu(sijui) fikiria familia yake inaumia kiasi gani juu ya hili? Au wewe ndo ungekuwa yy ungefanyaje?

Hujafa hujaumbika,Mungu si Athuman leo wajiona mzima au bora kesho yako huijui,tufikie hatua tufanye kampeni za kistaarabu na si kutoana thaman kiasi hiki.
 
wapuuzi hao vichwa vya nazi ndani machicha just ignore
 
Umesema kweli mkuu kujieshimu ni suala la maana na tukumbuke"kuna maisha baada ya oktoba 25

Wengi hawatambui kuwa baada ya uchaguzi maisha yanaendelea mkuu,hii jamii yetu inahitaji msaada kwa kweli
 
Mwenzako akijamba 'amejamba' ila wewe ukijamba 'nimepumua'.
 
Halafu unaweza kukuta imeandaliwa na yule Waziri wa IT
 
Namaanisha kwamba siasa ni mchezo mchafu...practically kwa waswahili...

Ukiingia kwenye siasa kubali kuchafuliwa
..siasa za maji taka...

Hivyo nanyie react against...kwani mliyaanza wenyewe sasa yamewageukia...take it easy...
 
waache wamchafue Lowassa wetu,sisi tushaamua,nawasikitia pale ambapo anachukua nchi watamtazama vipi?
 
Kaingia mwenyewe kwenye chandimu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…