Akili zetu za watu wa vijijini (isipokuwa wanaotoka moshi, mbeya, bukoba) ni mgando. Hakuna ambaye huwa anaona umuhimu wa elimu. Ila upande mwingine inawezekana huyo dogo anapenda shule pia! Sasa mazingira ya kwa nini aligeuka na kusema hawezi kuishi kwako ndiyo challenge. Nina vyanzo viwili.
- Inawezekana mkeo alimchimba biti au alionesha ukali fulani kwa kijana (kwa sababu mtu akitoka kijijini huwa tuna fikra za kishamba na pia huwa ni washamba wa vitu vingi), au house girl alimtisha kuwa mama wa nyumba ni mkali.
- Inawezekana dogo kakuta labda chakula hamshibi au anawamisi ndugu zake (ugeni wa mazingira)
Jibu kwa no. 1, hilo suala litakuwa gumu sana, na haswa kama hukumshirikisha mkeo wakati unamleta dogo. Lazima mkeo atakuwa alijisikia vibaya na kwa hasira alimuonesha dogo bifu angali bado mgeni. Nakushauri kama hukuwa umeshauriana na mkeo, basi muombe samahani na umueleze kuwa unaomba mkae na huyo mtoto mumusaidie shule. Ila kama mlishauriana, basi inawezekana labda kuna ukali fulani ulitumika au house girl alichangiza. Kwa hiyo wewe muassure dogo maisha ya amani iwapo atakuwa na tabia nzuri na usimpendelee au usifanye kitu aone unampendelea, fanya kama vile ni wajibu wako.
Jibu no. 2. Kaa naye tu umueleweshe juu ya umuhimu wa shule na kwa nini ulimtoa kijijini. Na kwa sababu ni mtoto inabidi umtreat kama mtoto, mpe haki ya kuwa mtoto!