Inasikitisha naomba ushauri wako mwana JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inasikitisha naomba ushauri wako mwana JF

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Zipuwawa, Oct 11, 2012.

 1. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hili limetokea sasa hivi naomba ushauri wako ili angalau maamuzi yangu yasiwe mabaya.

  Mimi nina ndugu yangu amabaye ni mtoto wa Mama yangu mdogo yeye kwa sasa ni marehemu ambaye alijaliwa kuzaa watoto wanne wakike wawili na wakiume wawili, sasa nilipokwenda liziko mwezi uliopita nilikuta yule mtoto wa mwisho yupo darasa la saba. Nilipomuona hali waliyokuwa nayo hao watoto mimi niliona ni bora nimuhaidi kuwa atakapomaliza darasa la saba nitamsomesha hadi hapo atakapopata mafanikio na kuwa mkombozi wa familia yao.

  Niliona kwa kipindi atakachomaliza elimu ya darasa la saba basi aje nyumbani kwangu Morogoro ili aweze kujiandaa na mitihani ya shule mbalimbali kwa kusoma pre form one ili atakapoanza mipango ya kupata shule basi yeye interview iwe rahisi kwake na aweze kupata shule.

  Jana amekuja kwa kusafirishwa toka Dodoma alipofika mimi kutokana na mihangaiko sikuweza kukaa nae nakumueleza cha kufanya na nini nimemuandalia kwaajili ya masomo yake. Basi leo nilitembelea shule mbili na kuchukua form kwaajili ya kupata nafasi.

  Niliporudi mchana baada ya kupata chakula cha mchana na familia yangu basi walikwenda kulala wote mimi nikiwa nachat alinifuata sebuleni na kuniambia kuwa yeye hawezi kukaa kwangu kwani maisha haya hatoyaweza. Nikamuuliza kunatatizo gani? akasema yeye hawezi kukaa nilishtushwa sana kwani huyu mtoto ni mdogo ana umri wa miaka kumi 13 sasa. Mimi nilijiuliza maswali mengi na kukosa majibu ndipo nikampigia dada yake ambaye mimi ni mdogo wangu na kumueleza yeye alianza kwa kulia na kusema nimwambie akirudi yeye si ndugu yake. Kumbuka huyu mtoto hakuwa anaishi na dada yake yeye ndio anajua maisha anayoishi huko aliko kwa mama yake mkubwa.
  Dada yake akasema nisimruhusu nikae nae mimi naona kama huyu mdogo wangu anaweza kuniletea matatizo mbeleni kwani ameonesha picha mbaya mapema sana.

  Mimi baada ya kufanya mawasiliano na baadhi ya ndugu niliamua kumwambia kesho nitakusafirisha na urudi huko utakakoishi maisha unayotaka . Baadae baada ya kuongea na dada yake akaja na kuniomba msamaha eti anaomba aendelee kubaki mimi nikamuuliza kwanini? hana jibu sasa mimi uamuzi wangu ni kumruhusu aende ili asije leta matatizo katika familia yangu. Mimi hapa ninaishi na mke mtoto mmoja pamoja na mtoto wa kazi hakika Mungu ametujalia maisha ya kuweza hata kubadilisha mboga mara moja moja. Na hata makazi yetu yanaridhisha . Naomba ushuri wako ili niondokane na hili jambo au kwa kusaidia au kutokusaidia kwani mimi naona bora hata nikatafuta mtu baki na mkumsaidia sasa hivi hapa namuangalia yupo mezani anapata chakula.
   
 2. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  kwanza kabisa pole sana kwa hilo maana ni njiapanda kubwa
  ningekuwa mimi, kwanza ningemshawishi aniambie kwanini aliogopa kukaa hapo mara ya kwanza na kwanini amebadili msimamo tena!
  pili kama inawezekana unaweza kumrudisha anakotaka kuishi na kisha ukamsaidia akiwa huko huko kwani dodoma nako shule zipo, labda iwe vijijini sana sijui wapi. lakini cha zaidi inawezekana anamawazo mbadala na kusoma so cha msingi mshawishi kwa upendo mkubwa afunguke, inawezekana aliogopa mazingira tu
   
 3. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni hofu tu ya kuishi mazingira mapya na ukizingatia bado ni mtoto. Mnatakiwa mjitahidi kumfanya ayapende na ajisikie kama yupo kule alipopazoea.
   
 4. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ni mtoto, ni mdogo, ni mgeni wa mazingira... kwanini unakata tamaa mapema? chukua muda kumsoma ukilinganisha mazingira alikotoka na hapo kwako unavyoishi. sasa kama wewe ulipanga kumsaidia na unakata tamaa kiulaini hivi,huoni kuwa hata wewe kuahidi kumsaidia kwako hakukuwa makini?. kumbuka elimu si siku moja, na elimu si darasani tu. hata kukaa hapo kwako na kuona unaishi vipi nayo ni elimu.anapokataa kukaa hapo manake ndo anahitaji kusaidiwa kwani amefungwa gizani , anahitaji nuru, na nuru ndo hiyo unataka kumnyima tena.
   
 5. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Nimempa masharti kuwa aseme kwanini hataki kukaa hapa na nani amemshauri ili nimsamehe amekaa kimya . hivyo ushauri wako wa kumsaidia huko huko ni zuri ila moyo wa kusaidia umekwisha sasa hivi najiuliza maswali mengi. ila asante kwa ushauri wako
   
 6. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,710
  Likes Received: 1,891
  Trophy Points: 280
  ni stress tu za ugeni mkuu, mm niliwah kufika mji mmoja pale bunda kulikuwa kuna kila k2 kwenye ule mji lakin huwez nilishnda nalia tu siku 3 mfululizo non stop, ukiniuliza kwa nn ckujb nalia tu...bt it waz ugeni! nilivyozoea sikutaka hata kuondoka. mia!
   
 7. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mimi nilikuwa nina nia ya dhati kumsaidia ndio maana niliamua kumsafirisha toka Dodoma hadi hapa na leo nimechoma mafuta kutafuta form za kujiunga na kidato cha kwanza kama hatofaulu au akafaulu shule isiyokuwa na matumaini ya elimu basi aweze kusoma. Ila ushauri wako ni mzuri sana Asante
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mtoto anaogopa tv huyo,Mwekee mikanda ya vempaya atakua sugu
   
 9. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Labda mkuu!
   
 10. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ahsante , samahani kwa neno, "kumsaidia kwako hakukuwa makini". halikustahili kuwepo hapo. ila jaribu kumvumilia na kumsoma huyo kijana. nikama tulipokuwa watoto, tukipelekwa shule tunakubali , lakini baadae tunaanza kukataa, pasi sababu za msingi, ndo kama huyo sasa, miaka 13 yake usimuone mkubwa
   
 11. S

  Sangomwile JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,091
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa,siku zote kule unakotoka unaweza kudhani ni bora zaidi kuliko unakokwenda.Ugeni tu ndio unaosumbua,mleta mada mpe muda huyo dogo,utashangaa baadae.
   
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,854
  Trophy Points: 280
  kwanza naomba unipe majibu ya maswali haya
  • ana jinsia gani?
  • kwanini wewe unasema unamsaidia?
  • kipi kilicho kukatisha tamaa zaid? je ni hizi kauli zake kizungumkuti ama anatabia nyingine yyte ile uliyoiona?
  • je kwa siku mbili alizokaa hapo kwako anaonekana kuwa mtoto mwenye hofu au amesha kopu na mazingira?
  ukinijibu haya nitakupa ushauri unaofaa ............
   
 13. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  :lol::lol: na prifomuwani ndio basi tena au?
   
 14. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Jaribu kudadisi tangu siku amefika hapo kwako kitugani kimemkwaza
   
 15. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ngoja niufanyie kazi ushauri huu
   
 16. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Sorry but you sound as if u have problems too. Yaani mtoto wa miaka 13 una m treat kama mtu mzima ? Labda kasome kidogo child developent articles/journals zinaweza kukuamsha.

  Briefly, unaweza kumuongezea matatizo zaidi. Sema umemsamehe, endelea na plans zako huku ukimfuatilia kwa zaidi. Kwa vile umeshamtisha, jitahidi sana kuonyesha upendo wa hali ya juu zaidi, na utakuja kutueleza soon kuwa amefunguka na kusema nini kilimsababisha atake kuondoka hapo. Utashangaa it could be little stupid stuff, for you and me lkn kwa yeye kubadili mazingira kwa haraka na kwa utoto, it was a big deal. Nilishaona watoto ambao hawakuzoea kula milo 3, kuoga kila siku, na kula chakula kizuri bila kufakamia/gombania. Walipoletwa ktk mazingira mazuri at first walikuwa na upweke sana lkn later wakafunguka baada ya adults waliokuwa nao kuwa nao karibu, kuwaongelesha na elimisha kwa nini wana milo 3 na kwa nini wanapakua kidogo kidogo, lazima waoge daily na lifestyles nyingine ambazo kwao hazikuwa normal.

  Again, it's only 13 yrs old, husimuaribu kisaikolojia utakuja juta !!

   
 17. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  .Ni mtoto wa Kike
  .Ninasema ninamsaidia kwani si jukumu langu kumsomesha
  .Kilichonikatisha tamaa ni huyu mtoto kusema hawezi kukaa kwangu kwani mazingira haya yeye hawezi bila sababu ya msingi na swala la tabia nyingine kwakweli sijui japo wakatia anaongea ana confidence ya ajabu. na huyu mtoto ndio anasiku mbili tu kwangu.
  .Hapa kwangu kuna mdada anayenisaidia kazi ndio anakuwa nae na kwakweli nyumbani kwangu ni geti kali ukiigia geti linafungwa . Na kutokana na mizunguko yangu na shughuli sijakaa nae
   
 18. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Note taken
   
 19. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,854
  Trophy Points: 280
  haya ndio majibu yangu kwako-
  • kwa jinsia yake anaweza kuwa ni mjamzito so anahofia kugundulika anapokuwa hapo, istoshe inawezekana pia amezoea uhuru wa manyani so anaona geti kalii linamboa.
  • kuhusu kumsomesha usiseme sio jukumu lako hata kidogo, so lonng ni mtoto wa dada yako na wazazi wake wamefariki basi wewe unawiwa kuhakikisha anakuwa na maisha mazuri kwani wafikir kazi ya mjomba ni ipi? nakwambia angekuwa hakuhusu asingekuwepo hapo kwako. tena ujue humsaidii kwakua unahela nyingi la hasha bali kwasababu ni jukumu lako nakuambia.
  • kasema hawez kukaa, ila si jambio la kukatisha tamaa hata kidogo je kama ni woga wa ugenini? ama ni kutokujua maisha? pia anawezekana kabisa akawa ana maswali mengi kinchwani mwake ila hana wa kumuuliza manake wewe alokuzoea ndo ivyo hauko karibu nae na kimsingi hawez kujua kama uko bize kias kwamba huwez kuongea nae.
  ushauri wangu mweke karibu yako na mfanye amuone shangazi yake kama mama yake yaani gap isiwepo kinidham na hata kihuduma. mweleze ajue maisha ya hapo yalivyo na jinsi ulivyo bize na correspondence zake zipite kwa wife wako.
  ni hayo tu
   
 20. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Asante sana ila la mimba sidhani anamiaka 13 tu
   
Loading...