Inasikitisha na inatia uchungu sana

Inasikitisha na inatia uchungu sana

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
3,476
Reaction score
2,087

Nikitaka kuzihesabu zinaweza kufika hata jumbe mia sasa kwenye akaunti yangu ya yahoo.
Ni watu wanaonitumia kuelezea aidha matatizo yao,
Wengi wao wakidai kuwa wana matatizo makubwa ya kiafya na hivyo wanakaribia kufa,
Wengine wanasema kuwa wao ni maofisa wa benki huko katika inchi zao aidha wengine wakijinadi kwangu kuwa wao hawana hata nasaba na watu walioacha mapesa ya kumwaga katika mabenki kadhaa hasa afrika ya magharibi huku wakiwa hawana watu wa kuwarithi.,

Lakini wao wanaowasiliana na mimi, Eti, Wakiwa katika nafasi nzuri kuwa wao wakishirikiana na mimi basi tutakula mapesa ya kumwaga na bila ya bughudha.,

Maranyingi wanasema tutumie njia ya wao kuja kuwekeza Tanzania na hapo ndipo itakuwa rahisi zaidi kwangu kutapata mgao wangu tena, Wa-maana hasa'.

Wanasisitiza kuwa unahitajika usiri mkubwa na ushirikiano ili tuzitoe pesa hizo benki na mimi nitapata mapesa yangu pasi na shaka namimi niondoe shaka kabisa juu ya itakuwaje kwani wao wanajua nini hasa cha kufanya kwakuwa wao wanajua mbinu za hufanya mimi nimilikishwe mali hizi kama ndugu wa wahusiak wakuu wa mali hizi.

Yaani wanazungumzia mabilioni kama ya ESCROW.

Nazitamani sana ila tatizo niko bize sana mwenzenu,kiukweli nawahurumia.

Duuuuu!
Yaani ukiyasoma matatizo yao inasikitisha sana,
Inasikitisha na inatia uchungu sana.


 
Huo uchungu unaotiwa na hao watu ukoje?
 
Back
Top Bottom