Inasikitisha: Kama Nondo na mbao (Vitu Tangible) vinachakachuliwa na TBS/TFDA wapo, Nina mashaka sana na usalama wa maji ya chupa!

kwanini bidhaa pungufu inaingizwa sokoni
 
Mkuu hongera sana kwa kupandisha hili bandiko hapa, kwa umuhimu wa hili bandiko naomba lipelekwe Twitter ili mawaziri walione...
 
Kingine zile mbao wanazodai zadawa haziliwi na wadudu sio kweli zinaliwa.
 
kwanini bidhaa pungufu inaingizwa sokoni
Sio kwamba ni bidhaa pungufu, ila wanakupa kitu kulingana na uwezo wako. Sio lazima wakupe nondo ya 40', ile ya 37' pia inatumika, ila ni vizuri wakakuambia bei ya nondo ya 40' na ile ya 37', wasikudanganye.

Sasa hivi wameanza kutoa bati la 20G na 18G lenye 4'x4' coz demand yake ni kubwa, sio lazima wakupe bati kubwa la 8'x4' wakati wanaweza kulikata ukapata nusu kwa bei nusu.
 
kwanini kiwanda kitoe nondo au mzigo uliopungufu? kwanza unene ni mdogo na urefu haujatimia, kwanini was I recycle huko kiwandani mizigo ikawa inatoka iliyokamili?
 
Wew nae ni mkuda unapita kupima urefu wa vifaa kwenye hardware unataka kujenga nin? Ikulu au
 
Ni asilimia 100% mkuu si 95% kwa upande wa nondo.
Hatari sana😡

Toka lini vyuma chakavu vitengenezwe kuwa Nondo kutoka viwanda vya matapeli kule Kibaha utegemee kuwa na quality nzuri na kibaya zaidi jamaa wa TBS wanaidhinisha bila soni.
 
Tulianza na vya wachina na sisi wenyewe waacha tujichakachue wenyewe tu,,, hata mm akija mteja kwangu namchakachua tu
 
Hapo hujaangalia square pipe, flat bar, condult pipe na misumari ndiyo usiseme milaini inapinda kirahisi sana feki tupu
mkuu tena ikipata kutu nzi wanainyea wanajaa kama kuna kinyesi. Misumari ikiyokaa mwaka mmoja ukiitoa ukaiweka hapo inanuka. Yaani maajabu sana
 
mkuu tena ikipata kutu nzi wanainyea wanajaa kama kuna kinyesi. Misumari ikiyokaa mwaka mmoja ukiitoa ukaiweka hapo inanuka. Yaani maajabu sana
Aisee chuma kinanuka? hii inaaply wapi Mkuu au ulichanganya na kitu kinachonuka
 
kwahiyo watanzania wote wakapange foleni kiwandani maduka yafungwe? unazani hizo bodhaa feki hazitoki viwanda hivyohovyo?
Nini maana ya REJECT kupatikana zikiwa dukani?
Viwanda wanazalisha bomba zao, then zinapita maabara zinakidhi viwango zinapigwa lebo na kupelekwa sokoni zile reject zinatupwa sasa baadhi ya wauza maduka wachache wanachukua reject na kupeleka dukani!!

Sasa chagua, ukanunue kwa authorized dealer au utaenda mtaani kisa bei chee!! chaguo ni lako!!
 
Hiyo dealer yupo nchi tofauti na hardware hizi nilizoona?
 
TBS
TBS ni bomu. Udhibiti wao wa bidhaa hauna kiwango hata cha kijiji. Hizo nondo zinavunjika(they are very brittle), matokeo ya kuchanganya vyuma mbali mbali. Usalama wa majengo u hatarini. Unene na urefu wa mbao, nondo, misumari, mabati ni under size. Mabati yana andikwa one gauge under. 32g inaandikwa 30g. Madudu ni mengi. Wanakula na viwanda, si bure. Kifupi ni uhujumi.
 
wewe ni mwongo, maelezo yako haya akisi aina yoyote ya mfumo wa uzalishaji kiwandani, na usambazaji. Unatetea usichokijua.
 
kaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…