Passion Lady
JF-Expert Member
- Nov 17, 2012
- 8,694
- 4,646
habarini wana jf
mi mwenzenu kuna kitu kimenikwaza na kimeniumiza sana
mtaani kwetu kuna mwanajeshi kaibiwa laptop,leo siku ya tano
wanapiga watu hovyo,kijana akikutwa barabarani ni kipigo
inasemekana kuna kijana amepigwa baada ya hapo wakampeleka
kituo cha police bahati mbaya amekufa,hajulikani ni wa wapi maana
walimkamata akiwa barabarani na shughuli zake
-hivi ukishakua mwanajeshi unaruhusa ya kupiga
mpaka kuua?sheria inawaruhusu hawa watu kunyaynyasa watu
kiasi hiki?halafu mbaya zaidi wanaenda zile nyumba ambazo ni
za watu wa kawaida sana,wenye mageti yetu hawathubutu,si uonevu huo?
sio siri imeniumiza sana,kama sheria za jeshi zinaruhusu hali hii,nimechoka!!
wanajeshi mtujuze kama sheria inawaruhusu kugeuza mtaa darfur kisa laptop
kaibiwa c ni uzembe wake?mfyuuuuuuuuu hamna haya!!